Mwizukulu wa Buganda
Member
- Nov 19, 2024
- 94
- 307
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema kuwa serikali imetekeleza madai yote yaliyowasilishwa na vyama vya upinzani, ikiwemo maridhiano, kurejea kwa wanasiasa waliokimbilia uhamishoni, msamaha kwa waliokuwa gerezani, pamoja na kuruhusu maandamano na mikutano ya hadhara.
"Wapinzani wakiongozwa na CHADEMA walisema hali ni mbaya, wakataka maridhiano, wakataka waliokimbia warudi, wakarudi. Wakasema kuna watu 400 walioshtakiwa na kuhukumiwa mwaka 2020, utaratibu ukafuatwa wakaachiliwa kwa msamaha wa Rais kwa mujibu wa Katiba. Hilo nalo wakapata. Wakasema wanataka mikutano na maandamano, wakapewa, walikuja hata hapa Bunda na helikopta yao kwa sababu wanapenda sana show-off. Lakini nyinyi watu wa Bunda mkawasikiliza, hamna kitu!"
"Sasa kila mahali ni Katiba, Katiba, Katiba! Watu wana njaa, wanataka chakula, wanataka hospitali na elimu, wewe kila siku unasema Katiba! Watakula Katiba?" amehoji Wasira.
"Sasa kila mahali ni Katiba, Katiba, Katiba! Watu wana njaa, wanataka chakula, wanataka hospitali na elimu, wewe kila siku unasema Katiba! Watakula Katiba?" amehoji Wasira.