Mzee Wassira ''aenda chaka'' akimjibu Tundu Lissu kuhusu hoja ya mabango ya Samia

Hujafa, hujaumbika. Weka akiba ya maneno mkuu mtanashati.
 
Astakafurah,,,,,t 🀣🀣
Astakafurah 🀣
 
Kwakweli hapa wameingia chaka huyu mzee kumteua hii nafasi
 
Lakini pia hata uwe na IQ kubwa kiasi gani, hata uwe na active mind kiasi gani, kuna spana zingine ni za kuacha zipite tu maana kuna upuuzi ukijaribu kuutetea unaishia kudhalilika tu. Hata air defense systems huwa kuna makombora zinayaacha yanapita tu maana hakuna namna ya kuyamudu.

Sasa kama hiyo spana ya mabango unaanzaje kuipangua wakati unajua kabisa ni unatetea upuuzi wa viwango vya kimataifa. Naamini hata sisiem wote wajikusanye nchi nzima kujibu hoja hiyo wote wataogelea, na hakuna mtu timamu atawaelewa. Hapo njia yenye ahueni kwao ilikuwa kukausha tu kama hawajasikia
 
Mamlaka pia zingemtumia kwenye ku-promote utalii kuliko kwenye siasa. Ni kivutio kizuri sana 🀣
 
Hii imenishtua sana nilipoiona, LISSU aligusia Mabango, Mzee anagusia Ukabila.

Ananikumbusha Mzee Biden.

..Mzee Wassira anasema Tz hatuulizani makabila wakati muda mfupi ametoka kuvikwa mgolole wa kabila la Wagogo na kupewa jina la jamii hiyo.🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…