Pre GE2025 Mzee Wassira, Amani ni matokeo ya Haki, unatangazaje Amani wakati Watu wanatekwa, wanauwawa? Mzee jaribu kua na Busara!!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
25,725
Reaction score
78,589
Hii Amani yako unayoishupalia shingo ni pale tu UHAI WA CCM unapotishiwa na UPINZANI?.

Miaka nenda miaka Rudi ,Hoja kuu ya CCM Huwa ni Amani ,Amani hii ni katika muktadha wa CCM au Taifa??

Kwani Upinzani wakishika NCHI wao ndio wataanzisha vita au nini??.
,
Mzee Wassira danganya watoto , Watanzania wanajua Amani unayozungumzia wewe ni Kwa CCM tu Wala sio Nchi Hofu ya CCM ni kuogopa Nchi kushikwa na Upinzani.

Kwa Amani ya Nchi , wapi watu wanaopaza sauti zao Kila siku juu ya watu wanaotekwa waziwazi, wanaouliwa mikononi mwa Dola.

Mzee Wassira Kuna maswali mengi sana yanayohitaji majibu, acha kujificha kwenye kichaka Cha Siasa za kizee na za hovyooo , hiki kizazi Cha Sasa ni Cha wasomi waloelimika na Vijana wanaojitambua , ACHA KUTISHA TISHA WATU.

Hakuna Cha machafuko Wala nini, hayo machafuko ni Hofu na Woga Ndani ya CCM kwakua ni wazi Keki ya Taifa mmeitafuna kwelikweli nyinyi wenyewe miaka na miaka na vizazi vyenu mkiwaambia Vijana wenye Degree waende Veta !!!! This is a Shame !!.

Mzee Wassira kua MwanaCCM, kusikufanye Kiumri na Kibusara Unashindwa kuwekwa Ndani ya BUS Moja na Akina Prof Shivj, Jaji Warioba n.k.

CHADEMA na ACT hawataki Vita Wala Ugonvi na Dola, wanachotaka ni MABADILIKO YA MFUMO KWENYE UCHAGUZI NA KATIBA MPYA TU.

Na haya sio matakwa ya Vyama vya Upinzani tu, hayo ni matakwa ya WATANZANIA wote Nchi hii tangu Tume ya Jaji Nyalali ,mpaka Kwa Jaji Warioba .

Leta Mabadiliko ya Mfumo wa Uchaguzi, Watu waingie uchaguzini , Mnataka Upinzani kuingia Uchaguzini kama Geresha tu miaka nenda miaka Rudi, Watu wanaongozwa na viongozi wasowachagua?.

Tanzania ya Sasa sio ya 2000 ambako wajinga walikua wengi !!.

Amani Amani Amani sio Hoja na Si kitu, Kama CCM ndio inatawala lkn watu wametekwa, wameuliwa, Ufisadi ndo usiseme, Biashara Haram zimetapakaa, madawa ya kulevya, Ukosefu wa Ajira , Maji na Umeme mpaka Leo ni shida , Kilimo ni Cha Mvua , Baharini bado wavuvi wanatumia Mitumbwi, Matumizi ya Serikali yako juuu , Rushwa ndo usiseme, Maadili yanazidi kushuka, Maofisin hamna Nidhamu Wala uwajibikaji ,bado unaimba Amani tu??.
 
Jambo la kwanza,
hakuna chama cha siasa cha upinzani Tanzania chenye uwezo wa kushika dola, kuunda serikali na kuongoza nchi, ispokua CCM pekee.
Hili uende ukamueleze hadi mwenyekiti wa chama chako Taifa.

Pili,
matukio ya utekaji na kupotea kwa waTanzania wasio na hatia, yanaudhi na kuumiza sana.

Na kwanini matukio haya mabaya ya kifedhuli hutokea kwenye nyakati za uchaguzi wa ndani ya chadema pekee na kuwaathiri chadema wenyewe kwa kiasi kikubwa?

hii ni dalili ya wazi kwamba upinzani hususani chadema wakishika nchi kutakua na matukio ya umwagaji damu wa kutisha huenda ikawa zaidi ya utekaji 🐒
 
NONSENSE!
 
mmoja wao alipouliwa Tegeta kwa Ndevu ndipo wakajitokeza ila sijawai kuona kiongoz wa serikai akitoa kauli yoyote juu ya upoteaji wa wananchi wa kawaida ba wafuasi wa Upinzan , je wao ccmu wanajali hasa kuhusu watu wao ? je wanaongoza serikali ya watu wote au ya ccmu ?
 
Mzee wa busara unamtaka awe na busara, kweli?
 
Wazee wa Maslahi hawajali😅😅😅
 
Mzee wasira ndio uhalisia wa maccm yote yao yawaza kuiba kura ili yaendelee kuiba fedha zetu,raslimali zetu zooote wanaiba wanagawana Mali zetu kama zao za kifamilia ccm nchi sio yenu ni yetu sote acheni ujinga wa kusema amani amani huku watu wanaotekwa kila mahali mfano Mzee Ally kibao alishushwa ktk bus mchana kweupe kauliwa kinyama eti amani acheni ,eti kifo ni kifo,acheni mungu atakuja kuwauliza ccm wote ni moto wa jehanamu
 
😅😅
 
Kwa hiyo umevimbiwa amani? Nenda Sudan. Sikujua ni jinga hivyo
 
Ulitaka atangaze vita?
 
Ngoja utekwe ndo utajua neno amani lipo kama geresha ya maccm zombi eti yanasema utekaji ni DRAMA tu ,kufanya drama uhai wa mtu
 
Yeye mwenyewe ngumi mkononi amani gani anazungumza huyu shetani?
 
Kijana anayepoteza muda kumskiliza Wassira ni wakuonewa huruma😔😔!!!
Wassira angekuwa na akili nzuri angeshajijenga KIMAISHA na asingeng'ang'ania ajira mpaka uzee huu!!
Babu unatumwatumwa na mwanamama alafu unajifananisha na Trump🤣🤣 Trump ni bosi hatumwitumwi na mmama na kuitika "Sawa mama"
Mpaka Leo anatukanana na kina Heche🤣🤣 Wadogozake kina Kinana wameona wapumzike wale pensheni yeye haridhiki, kala mishahara miaka zaidi ya hamsini lkn bado ananjaa Kali sijui alikuwa anahonga helazakehuyu babu?
 
Gentleman,
ikitokea kuna tukio lenye viashiria vya utekaji au upotevu wa binadamu awe mTanzania au sio mTanzania na likaripotiwa kwenye vyombo husika vya kiusalama,

basi,
serikali sikivu ya CCM inawajibika kuanzisha uchunguzi wa kiusalama ili kujiridhisha, kubaini ukweli na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na msako mkali kwa wahusika.

Lakini,
ikitokea mtu kwa siri siri alikua anamendea mke wa mtu akafumaniwa akaumizwa au kupotezwa na tukio hilo likaripotiwa mitandaoni pekee, ni wazi vyombo husika vya ulinzi na usalama vitachelewa kuchukua hatua kwakua ni kazi kubwa kidogo kubaini chanzo mahususi cha uhalifu huo.

Ni muhimu sana wananchi wenye taarifa sahihi za kihalifu kuripoti polisi haraka iwezekanavyo bila kuchelewa ili uchunguzi ufanyike haraka na hatua zichukuliwe 🐒
 
Nasubiri kwa hamu siku mtu/kundi likija na mbinu mbadala ninayoijua mimi zaid ya tu maandamano na migomo.
Kwa tulipofikia, ukizingatia ndoa ya chama, serkali na vyombo vya dola ilivyo, wapenda haki na mabadiriko hawana leverage (nimekosa kiswahili chake).
*Democracy operates properly where people have acquired two significant attributes;
1. WELL KNOWLEDGEABLE.
2.WELL INFORMED*
 
Unataka awe na busara ili afutwe uanachama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…