Tetesi: Mzee Wassira kuhamia CHADEMA

Uzee ni dawa labda katambua madhaifu ya CCM ! Aje tu Mzee Tyson, lakini kama ni jimbo la Bunda Bulaya anaenea na anatosha! Asaidie tu kupambana majukwaani maana ni fundi wa kujenga hoja!
 
Wa nini wakati huu? Akalee vitukuu
 
Poor
 
Kama hii ndo siasa, basi ni dalili za wendawazimu. Kuna mfululizo wa vipindi vya mahojiano ya Wasira na mwana habari ambavyo Wasira muda wote anatukana Chadema na uongozi wake. Haininiingii akilini Wasira kuwa amekaa meza moja na Lisu au yoyote yule wa Chadema. Sihoji umakini na usomi wa huyu mzee. Tatizo hapa ni kupata cheo kwa njia yoyote: halali au isiyo halali. Siyo mapenzi ya sera za Chadema au upinzani. Achilia mbali umri wa huyu mzee, nitawashangaa Chadema hata kuanzisha mazungumzo yoyote ya mahusiano.
 
Aaaa..., wewe! Huko kwa Bulaya ataanzaje? Panya aingie mwenyewe kwenye chumba chenye paka. Japo wanasiasa wote wametuonyesha kuwa ni malay* (Mwl Nyerere pia aliwahi kusema kuwa baadhi yao ni kama malaya) haiwezi kufika huko.
 


Kuna kigogo alisema watakaohamia huko upinzani watawafuata hukohuko na kuwatenda
 
Mzee apumzike tu maana kuna muda umri ukifika na vijana wakakutandika ni bora utulie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…