Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
Habari zilizonifikia ni kuwa mzee William Mbunga mwandishi wa habari mkongwe, aliyepiga picha tukio maarufu uchanganyaji udongo kwenye Muungano wa Tanganiyika na Zanzibar amefariki Dunia tarehe 3/2/2021.
Pia ndiye muanzilishi wa shule ya uandishi wa habari SJMC.
Bwana ametoa, bwana ametwaa
--
Pia ndiye muanzilishi wa shule ya uandishi wa habari SJMC.
Bwana ametoa, bwana ametwaa
--
WILLIE MBUNGA: ALIYEPIGA PICHA YA MUUNGANO WA TANZANIA NA ZANZIBAR NA MWANZILISHI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI CHA SERIKALI NCHINI
Na Dereck Murusuri
O, so sad. Sad indeed. My mentor, Mzee wangu, rafiki na fellow lensman.
Mara ya mwisho tumewasiliana tarehe 19 November, 2020.
Alikuwa akitaka kuwepo na Degree ya upigaji picha na utengenezaji wa documentary za wanyama pori, ili kuboresha eneo hilo.
Alihoji, kwanini tuwe tunatumia zaidi picha za watu wa nje ya nchi kwenye Televisheni zetu, wanakuja wanatupigia na wanatuuzia wakati wanyama tunao hapa hapa kwetu?
Sisi ndio tulipaswa kuwauzia quality documentary.
Alinieleza kuwa SJMC (UDSM) tayari walikuwa wamekubali kuanzisha Programme hiyo na yeye alipewa jukumu la kusaidia kupata funding.
Sijui alifikia wapi, huenda Prof. Michael Andindilile atatueleza. Mzee mwanzilishi, kama alivyoanzisha Chuo cha Uandishi wa Habari, tayari ameshamaliza sehemu yake ya utumishi katika uso wa dunia.
Amekuwa anafanya kazi hadi dakika ya mwisho, kwake umri wake wa zaidi ya miaka themanini, haukuwa kikwazo. Lipo jambo kubwa la kujifunza katika utumishi endelevu.
Mtume Paulo katika maisha ya utumishi anasema, "Kuishi ni Kristo na Kufa ni faida (to gain)."
Ni Mzee Willie Mbunga aliyeipiga ile picha ya MUUNGANO ya kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar. Picha ambayo aliipiga siku moja na itabakia ishara ya Muungano milele na milele.
Amelitumiakia Taifa letu kwa ari, upendo mkubwa na bila kuchoka.
Ndiyo mwanzilishi wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha Serikali nchini.
Nikiwa Afisa Habari Msaidizi pale Idara ya Habari, MAELEZO, chini ya Kaka yangu na Bosi wangu Raphael Hokororo, Mzee Mbunga hakuacha kuja na kututia moyo jinsi ya kuandika na kupiga picha za matukio ya Serikali.
Siku zote alikuwa Mwalimu kwetu na alituchukulia kama Baba kwa wanae.
Chuo alichokianzisha ndio SJMC ya leo, sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
SJMC imetoka mikononi mwa nyota hii iliyozima katika Hospitali ya Mloganzira.
Historia, kama Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha kwanza cha Serikali nchini, nayo imeandikwa kwa kalamu ya chuma.
Hata kama yeye amefariki dunia, historia aliyoitengeneza kwa muda wake duniani haitafutika kamwe.