PreGE2025 Mzee Yusuf Makamba awaomba Watanzania wamuombee Rais Samia ushindi na Afya Njema

PreGE2025 Mzee Yusuf Makamba awaomba Watanzania wamuombee Rais Samia ushindi na Afya Njema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mzee Yusuf Makamba, amewataka Watanzania kumuombea Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ushindi, afya njema umri mrefu kutokana na kujitoa kwake kwa dhati kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya taifa.

Akizungumza katika dua maalum iliyofanyika nyumbani kwake Mahezangulu, Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli mkoani Tanga na kuhudhuriwa na wananchi zaidi ya 1500 kutoka mkoani hapa na nje ya mkoa huo, Mzee Makamba alisema kuwa binadamu wako si kwa ajili ya maisha yao tu, bali hasa kwa maisha ya wengine.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Rais Samia anaishi kwa ajili ya furaha na ustawi wa Watanzania. Ni jambo la heri watu wengine kuwa na amani na furaha kwa ajili yako, na sasa hivi, Watanzania wana amani na furaha kwa ajili ya Mama Samia," alisema Mzee Makamba

Hata hivyo Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba, amesema kuwa umahiri wa Rais Samia uko wazi na unadhihirika kupitia kazi anazofanya kwa Watanzania.
 
Mzee amenusa kuwa bi mkubwa anaweza kulipa kisasi kwa bwana mdogo kutorejea mjengoni.

Baba ukiwa unambeba sana mtoto wako haumsaidii, unamlemaza. Mwisho wa siku anakua akiamini yeye anastahili zaidi kuliko wengine kumbe ilikuwa ni mbeleko ya baba.

Same applies to mzee wa bao la mkono.
 
Back
Top Bottom