Salaam Shalom!!
Mzee wetu ameibuka na Kutoa Pongezi kedekede Kwa Mh Rais Samia Suluhu Hassan Kwa uamuzi mzuri aliofanya kuwabadili baadhi ya mawaziri, mtoto wake akiwemo.
Amemfananisha Rais na Coach jinsi anavyobadili kikosi, Nia ni ushindi.
Ameenda mbali na kuwapongeza waliotumbuliwa akidai pia wanastahili Pongezi Kwa kuwa wamemsaidia Rais Kwa muda waliokuwa mamlakani.
Itoshe kusema kuwa, Mzee huyu naye ni MMOJA wa wazee muhimu waliobaki, tuwatumie.
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Source: Mahojiano, Wasafi media.
Karibuni 🙏
======
Mwandishi: Mzee Makamba bwana, tumeona mabadiliko ya Baraza la mawaziri!
Makamba: Wewe unashangaa nini?
Mwandishi: Sishangai mzee Makamba, naangalia picha yako unavyoangalia na mheshimiwa Rais anavyoboresha
Makamba: Sawa labda nikwambie mambo mafupi tu! Halooo
Mwandishi: Nakusikia Mzee Makamba
Mzee Yusuph Makamba: Hivi kocha wa Simba akimtoa mchezaji unamlaumu? Mambo mawili yanayoweza kumfanya amtoe mchezaji, mwingine anaweza akawa hana makosa lakini amechoka, pumzi zimeisha lakini pumzi zikirudi anamrudisha tena maana hawa ambao leo wametolewa, walikuwemo wakatoka na wamerudi tena.
Kwahiyo usije ukashangaa tena mwingine akarudi baadae, jambo la kawaida tu. Nasema Rais ni kocha, kazi ya kocha ni kuhakikisha kwamba magoli yanafungwa.
Kwahiyo anatazama, je katika kipindi hiki nani mchezaji bora kuliko mwingine anamchukua na hawa anawapumzisha.
Kwahiyo tunampongeza Rais kwa uteuzi alioufanya, tunawapongeza walioteuliwa na tunawapongeza na hata hawa wameondolewa, wanapaswa kushukuru maana si walikuwemo?