Mzee Yusuph Makamba: Nampongeza Rais Samia kwa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, asema isiwe mshangao wakirudishwa

Mzee Yusuph Makamba: Nampongeza Rais Samia kwa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, asema isiwe mshangao wakirudishwa

40 people are here!!

Lucas Mwashambwa tia neno tafadhali.
Mimi sina neno ndugu yangu ,ndio maana unaona nipo kimya kwa sababu kama sina neno huwa siongei hata kama nikipewa nafasi ya kuongea. Mengi yamezungumzwa na wengine, ambapo mimi sioni sababu ya kuzungumza Mengine tena.

Kazi ni kipimo cha utu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Mimi sina neno ndugu yangu ,ndio maana unaona nipo kimya kwa sababu kama sina neno huwa siongei hata kama nikipewa nafasi ya kuongea .Mengi yamezungumzwa na mimi sioni sababu ya kuzungumza Mengine .

Kazi ni kipimo cha utu.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kwahiyo utamlazimisha hata kama amehemewa?
 
Mimi sina neno ndugu yangu ,ndio maana unaona nipo kimya kwa sababu kama sina neno huwa siongei hata kama nikipewa nafasi ya kuongea. Mengi yamezungumzwa na mimi sioni sababu ya kuzungumza Mengine.

Kazi ni kipimo cha utu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Lucas ongea na Mzee, inaonyesha anaweza kukusaidia!!
 
Hahah Jamaa anawachoraga sana wasiomjua 😂

Ila Yote kwa Yote Lucas ni Kada mtiifu🙏🙏🚸🚓
Ninachofurahia saiz Yale mambo ya makada kuteuliwa sifa kuu ikiwa n.i kutukana WAPINZANI yanaenda yanapungua.

Ni muhimu kuelezea na kufafanua na kurudia tena na tena KAZI wanazofanya viongozi, Si kutukana pekee.
 
Salaam Shalom!!

Mzee wetu ameibuka na Kutoa Pongezi kedekede Kwa Mh Rais Samia Suluhu Hassan Kwa uamuzi mzuri aliofanya kuwabadili baadhi ya mawaziri, mtoto wake akiwemo.

Amemfananisha Rais na Coach jinsi anavyobadili kikosi, Nia ni ushindi.

Ameenda mbali na kuwapongeza waliotumbuliwa akidai pia wanastahili Pongezi Kwa kuwa wamemsaidia Rais Kwa muda waliokuwa mamlakani.

Itoshe kusema kuwa, Mzee huyu naye ni MMOJA wa wazee muhimu waliobaki, tuwatumie.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Source: Mahojiano, Wasafi media.

Karibuni 🙏

======


Mwandishi: Mzee Makamba bwana, tumeona mabadiliko ya Baraza la mawaziri!

Makamba: Wewe unashangaa nini?

Mwandishi: Sishangai mzee Makamba, naangalia picha yako unavyoangalia na mheshimiwa Rais anavyoboresha

Makamba: Sawa labda nikwambie mambo mafupi tu! Halooo

Mwandishi: Nakusikia Mzee Makamba

Mzee Yusuph Makamba: Hivi kocha wa Simba akimtoa mchezaji unamlaumu? Mambo mawili yanayoweza kumfanya amtoe mchezaji, mwingine anaweza akawa hana makosa lakini amechoka, pumzi zimeisha lakini pumzi zikirudi anamrudisha tena maana hawa ambao leo wametolewa, walikuwemo wakatoka na wamerudi tena.

Kwahiyo usije ukashangaa tena mwingine akarudi baadae, jambo la kawaida tu. Nasema Rais ni kocha, kazi ya kocha ni kuhakikisha kwamba magoli yanafungwa.

Kwahiyo anatazama, je katika kipindi hiki nani mchezaji bora kuliko mwingine anamchukua na hawa anawapumzisha.

Kwahiyo tunampongeza Rais kwa uteuzi alioufanya, tunawapongeza walioteuliwa na tunawapongeza na hata hawa wameondolewa, wanapaswa kushukuru maana si walikuwemo?
Mawaziri wenyewe waliotumbuliwa Wameshindwa kushukuru nafasi waluzotumikia ndio huyu babu aje kuwasemea?

Hawafai kurudisha barazani
 
Back
Top Bottom