Mzembe, mvivu huona kila kitu anaonewa kwake kulalamika ndio silaha kuu na huyu ndo Mtanzania

Mzembe, mvivu huona kila kitu anaonewa kwake kulalamika ndio silaha kuu na huyu ndo Mtanzania

Street Hustler

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
2,175
Reaction score
4,299
Ndugu Leo tuongee kidogo kuhusu maisha yetu halisi hapa tujiseme, tujitukane hii italeta taswira mpya kamasio sisi basi hata uzao wetu huenda ukawa Bora.

Sisi n hatupendi kufanya kazi lakini tunataka tuwe napesa mfukoni je tutazipata vipi bila kufanya kazi tena sio kufanya kazi tuu bali n kwa kujituma sana je hyo spirit tunayo?

N watu wa kulaumu kila kitu serikali ifanye Ila tunasahau kuwa serikali n watu na watu ndo sisi yaan tunapenda kufanyiwa sasa Kama hukufanya wewe unahisi utapata kile unachostahili ndo mana mtu mvivu na mzembe kulalamika hakutamuisha kamwe eti unategemea Chama Cha siasa ndo kikuletee urahisi wa Mambo yako thubutu hilo haliwezekani, urahisi wa Mambo yako unafanyanywa na pesa na ili uwe na pesa lazima ufanye kazi na ujitume.

Unakuta kijana au hata mtu mzima kapata kazi analipwa vizuri tuu badala ya kusave pesa yeye ndo kwanza anawaza kunywa pombe na pizi Kali, kununua Gari la kustarehe, hujaoa unapanga nyumba nzima eti uishi ki single boy unaacha kuishi kibachela matokeo yake baadae tunaanza kulalamika hoo Kodi nyingi mshahara hautoshi Yan full kulalamika tunasahau kuwa pesa uletwa na pesa Kama huna pesa tumia akili kupata pesa pia tambua akili huishiwa maarifa hvyo n muhimu ukiwa na pesa tumia pesa kupata pesa nasio kutumia pesa kupata vitu.

Uwezo wa kufikiria
Hii kiukweli sisi Ma-slowlearn yan tunachelewa kujua vitu na hatuwezi kujenga hoja kabisa mfano Tanzania insvyuo vikuu zaidi ya 15 na kila chuo kinatoa wahitimu zaidi ya 200 kila mwaka Sasa jiulize kweli wataalamu wetu wameshindwa kutoa elimu jamii kuhusu KATIBA au CHANJO YA KORONA na kuwaacha wanasiasa watoe hyo elimu.

Mpaka Leo kijana anajitimu chuo kikuu hajui anaenda mtaani kuwa Nani kweli?

Mwanao anatakiwa kwenda chuo kikuu na hawezi kujaza fomu za elimu ya juu wazazi mnashinikiza au mnalipa watu wasasaidie watoto wenu jinsi ya kujaza fomu kweli?

Angalia elimu ya muhindi anasomea kweli na kazi anafanya kweli Sasa wewe mtanzania mwenzangu umesoma lakini hujaelimika bado unajua kesho n siku ya kazi unaenda kulewa mpaka saa sita usiku asubuh unafika kaxin sas nne na misamaha kibao unafikiri muhindi au boss wako atakulipa vizuri? Kwanini usiseme anakunyanyasa?

TUJIFUNZE JINSI YA KUJIANDAA NA KUPANGILIA MAMBO YETU.

- Wewe n kijana unasoma basi jiulize au ulizia kwa wanaojua hicho unachosoma kina faida gani kwenye jamii na je unakiweza au unasoma kutimiza wajibu?

- Umepata kazi jifunze jinsi yakuwa mbunifu kazini tena ikibidi siku ya holiday omba jitolee kufanya kazi ofisini kwako bila malipo pia ukipata pesa punguza matumizi ya kijinga iga wahindi au watanzania wenzio WACHAGA mana hawa pia wameiga au wamefundishwa kuishi Kama WAHINDI.

usitegemee mwanasiasa akuletee urahisi wa maisha yako kila kibiashara Ina mtaji na mtaji wa mwanasiasa Ni mtu ambae hajielewi.

Tengeneza pesa, omba MUNGU akupe afya njema, heshimu watu hayo mengine yakatiba, korona, chadema, CCM yote utaona yanakupotezea muda tuu.

Karibu kilingeni.
 
Watanzania huwa tunajua kufuatilia sana umbeya tumesahau kufahamu kuwa teknolojia inakua kwa kasi sana .. ni suala la vijana kujikita kwenye ujuzi na ubobevu wa mambo tafuta ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili jamii toa elimu fasaha kwa watu wanaokuzunguka si wote watakubali ila walau umejaribu kitu (uthubutu) ... Kikubwa zaidi penda ufanyacho kuwa na juhudi
 
Baadhi yetu tunaingia kazini tumechelewa, baada ya muda mfupi tunatoka kwenda kupata chai. Kurudi saa tano. Tunajizungushazungusha ofisini ikifika saa saba lunch time, mtu Akitoka, kurudi ni saa tisa, akikaa nusu saa muda wa kufunga ofisi imefika. Anachomoka huyoooo, halafu anajigamba ametoka ofcn. Kwa hesabu nyepesi, mtu huyo ameonekana kazini masaa matatu tu.

Lakini ndio wa kwanza kulalamika mshahara mdogo, posho, mazingira mazuri ya Kazi nk.

Kifupi TUNAZINGUA SANA ndio maana foreign companies hawana mpango kuwaajiri ngozi nyeusi Kwenye nafasi nyeti.

TUBADILIKE.
 
Kuna vitu inabidi tubadilike kwa kujilazimisha vinginevyo kwenye dunia hii magari yanatumia umeme watanzania tutaumia sana
 
Mkuu naunga mkono hoja.
Ndio maana me kila siku, sururu mkononi, tayari kwa kuitoboa ardhi kujua kilicho chini ya ardhi.
Naamini ipo siku nitampa ajira msomi wa chuo kikuu.

Watu wanadhani kudownload pesa n kazi rahisi Yan anajiwazia kuwa milionea huku amelala kitandani.

Hongera kwa kuchagua njia hyo mkuu hope one-day yes MUNGU akuwekee mkono wake kwenye juhudi zako.
 
Baadhi yetu tunaingia kazini tumechelewa, baada ya muda mfupi tunatoka kwenda kupata chai. Kurudi saa tano. Tunajizungushazungusha ofisini ikifika saa saba lunch time, mtu Akitoka, kurudi ni saa tisa, akikaa nusu saa muda wa kufunga ofisi imefika. Anachomoka huyoooo, halafu anajigamba ametoka ofcn. Kwa hesabu nyepesi, mtu huyo ameonekana kazini masaa matatu tu.

Lakini ndio wa kwanza kulalamika mshahara mdogo, posho, mazingira mazuri ya Kazi nk.

Kifupi TUNAZINGUA SANA ndio maana foreign companies hawana mpango kuwaajiri ngozi nyeusi Kwenye nafasi nyeti.

TUBADILIKE.

Yaan mkuu hatuna adabu ya kazi mtu anajisifia anafanya kazi lakini ukimuuliza kipi mwajiri wako anajivunia kuwa nawewe zaidi ya umbea, majungu hakuna.

Mtanzania idd-mosi ikiwa jumatano, idd-pili ikiwa alhamisi anataka ijumaa iwe holiday pia ili aunge jumamosi na jumapili akitumia pesa kwenye starehe ajui kuwa siku za mapumziko hutumia pesa zaidi kuliko siku za kazi
 
Waajiri hawa hawa wa kibongo! Ded,katibu mkuu/wizara. muhindi, Mwarabu, mchaga nk.
Hukuna motisha ya watu kufanya kazi. Mazingira yapo hovyo. Ofisi nyingine kama magofu. Nikikupigia picha ofisi ninayofanyia kazi wewe huwezi kija kufanya kazi landa kama una njaa kama mimi.
Hata kama una moyo vipi huwezi kuwa consistent katika mazingara mabaya yasiojali haki za binadamu.
Kama kazi binafsi nakuunga mkono ila za waajiri acha zidorore tu.
 
Mabadiliko huanza na wewe Kama hyo ofisi unataka ibadilike lazima na wewe ubadilike kivyovyote vile mkuu.

Funga mkanda mkuu
 
Ofisi ya serikali chovu unaibadilishaje?
Ukimpenda mwanamke mwenye jicho moja utakuwa unamuona Kama anakukonyeza Ila usipompenda utamuona anachongo.

Ofisi kuwa chovu haithiri wewe Kama wewe kuwa +ve na unachofanya Kama umeipenda.

Hata chooni ukiamua uwe unakula humo n sawa tuu muhimu upasafishe pawe pasafi.
 
Mabadiliko huanza na wewe Kama hyo ofisi unataka ibadilike lazima na wewe ubadilike kivyovyote vile mkuu.

Funga mkanda mkuu
Mkuuu kuna watu wanapambana sana kufanya kazi kweli kweli lakini ofisi nyingi hazithamini hasa serikali yetu.Binafsi mm niliamua kujituma kweli kweli kwenye kazi yangu ya ualimu ,nafundisha hisabati mazingira yenyewe yakijijini ,unafundisha mda wote inatumika hadi wekend,unatoka kazini saaa 12 ili wanafunzi waweze hisabu.

Unaangaika kila mwaka upate A na B za hesabu kwa kujila kweli kweli lakini no motisha na asante ,yaani akili yako myingi unaiwekeza kwenye kazi za watu wewe unasubiri ukistaafu ndoo ujenge kwasababu salary ni kidogo.

Sasa nikaamua kuwa kama wengne ambao akili yao muda mwingi wanawaza ya kwao na wanafelisha kweli kwenye masomo yao,mambo yamebadilika kwangu angalau lakini kazini kumekwama hakuna cha A wala B.
 
Lakini tunapenda sana kulalamika na kunung'unika halafu tunasapotiana kwenye manung'uniko hayo

Tupigeni kazi na kupunguza usingizi na uchawi.
 
Lakini tunapenda sana kulalamika na kunung'unika halafu tunasapotiana kwenye manung'uniko hayo

Tupigeni kazi na kupunguza usingizi na uchawi.

Kabisa hapo hatuendi mbele tuache kulalamika tuchukue hatua
 
Mkuuu kuna watu wanapambana sana kufanya kazi kweli kweli lakini ofisi nyingi hazithamini hasa serikali yetu.Binafsi mm niliamua kujituma kweli kweli kwenye kazi yangu ya ualimu ,nafundisha hisabati mazingira yenyewe yakijijini ,unafundisha mda wote inatumika hadi wekend,unatoka kazini saaa 12 ili wanafunzi waweze hisabu.Unaangaika kila mwaka upate A na B za hesabu kwa kujila kweli kweli lakini no motisha na asante ,yaani akili yako myingi unaiwekeza kwenye kazi za watu wewe unasubiri ukistaafu ndoo ujenge kwasababu salary ni kidogo.
Sasa nikaamua kuwa kama wengne ambao akili yao muda mwingi wanawaza ya kwao na wanafelisha kweli kwenye masomo yao,mambo yamebadilika kwangu angalau lakini kazini kumekwama hakuna cha A wala B.

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app

Fanya ofisi yako ikuone wewe n asset
 
Back
Top Bottom