Mzize apata simanzi kubwa dili lake kupeperuka

tyc20

Member
Joined
Feb 15, 2025
Posts
23
Reaction score
59
Huyu Hapa Ndio Mwamba Aliyeharibu Dili la Mabilioni la Mzize Huko Libya

LILE dili la bilioni 3 limeota mbawa. Ndicho unachoweza kusema baada ya miamba ya soka ya Libya Al Ettihad kuachana na mpango wa kumsajili straika wa Yanga, Clement Mzize na badala yake kunasa saini ya raia wa Botswana.

Nyota huyo amejiunga na kikosi hicho akitokea AS FAR Rabat ya Morocco aliyojiunga nayo Januari mwaka jana akitokea USM Alger ya Algeria, ambako tangu ajiunge na miamba hiyo amecheza jumla ya michezo 21 na kufunga mabao matatu tu msimu huu.

Timu nyingine alizowahi kuchezea nyota huyo ni Olympique Khouribga ya Morocco na Township Rollers na Gaborone United za kwao Botswana, huku akishinda taji la Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023 na USM Alger, sawa na CAF Super Cup 2023.

Kitendo cha Tumisang Orebonye, kutua kwa miamba hiyo, kimefanya dili la Mzize kukwama, licha ya kiasi kikubwa cha fedha ambacho Yanga ingekipata, huku ikielezwa viongozi walikuwa tayari kumuuza, ingawa sio kipindi hiki wanachowania taji la Ligi.

Mzize amekuwa na kiwango bora akiwa na Yanga anayoitumikia kwa misimu mitatu sasa ambapo hadi sasa amefunga mabao tisa ya Ligi Kuu akiongoza mbio za ufungaji bora, huku akiasisti mengine matatu kati ya mabao 42 yaliyofungwa na timu hiyo katika mechi 17 za Ligi Kuu Bara.

Mbali na mabao hayo ya Ligi Kuu, Mzize pia amefunga mabao matano na asisti mbili katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Yanga ilitolewa hatua ya makundi na kukwama kutinga robo fainali kwa msimu wa pili mfululizo baada ya msimu uliopita kufika baada ya kupitia miaka 25 tangu ilicheza 1998.

Mzize ambaye ni zao la timu ya vijana ya Yanga, alikuwa akiwindwa na Al Ittihad iliyotenga ada ya uhamisho Sh3 bilioni, huku ada yake binafsi ya kusaini mkataba (sign-on fee), ikiwa ni zaidi ya Sh1.3 bilioni kwa mkataba wa miaka miwili.

Kuonyesha umuhimu na mchango wa nyota huyo, mbali na kiasi chote cha fedha alichokuwa amewekewa na Walibya, pia alitengewa kiasi cha mshahara wa Sh50 milioni kwa mwezi ambao kwa mkataba wake wa miaka miwili angevuna Sh1.2 bilioni, na ilipomkosa wakaamua kumnyakua Orebonye.
 
Kwanini Kibu asiende kuchukua nafasi ya Mzize huko Morocco

Kibu bado anahitajika kwenye club yake michuano ya Caf

Tukiongea kiuzalendo kabisa hili dili ilitakiwa Yanga imuachie Mzize aende huko, kwa maslahi mapana ya mchezaji mwenyewe, Yanga itapata hela na Taifa litanufaika pía kuwa na wachezaji wengi wanaocheza ligi kubwa zenye ushindani

Hersi anasema atauzwa msimu ukiisha, kumbuka msimu ukiisha wachezaji wengi ligi mbalimbali wanakuwa sokoni, hvyo soko linakuwa na ushindani mkubwa
 
Ifikie wakati muwe mnawasaidia kuwajenga hawa wachezaji wetu vijana na wasio na uzoefu wa kutosha wa kwenda kucheza ligi zenye ushindani mkubwa nje ya nchi.

Mzize bado anahitaji kujiimarisha zaidi ndani ya Yanga, kabka ya kwenda kucheza nje ya nchi. Kinyume na hapo, mnaweza kusababisha kiwango chake kikaporomoka kwa sababu tu ya kumjaza upepo.
 
Yaani Yanga imemlea Mzize Toka under 17
Wewe ndo unawazidi maoni juu ya mchezaji wao
Azam walimtaka zamani Kwa million 400 Yanga wanagoma, Leo thamani yake imefika billion 2
What if mwisho wa msimu wakapata 5bilions ?
Yanga wamewekeza kiasi kikubwa hadi Mzize kuwa hivi unavo muona
Wamempa makocha Bora, anazungukwa na wachezaji Bora, miundo mbinu ya mazoezi, chakula, malazi n.k
Na wao wana haki ya kupata thamani wanayohitaji
 
Novatus dismas alijiimarisha na timu gani hapa nyumbn mpaka kwenda nje ya nchi?
Nataka nithibitishe ile kauli ya zungu kwako
 
Ifikie wakati muwe mnawasaidia kuwajenga hawa wachezaji wetu vijana na wasio na uzoefu wa kutosha wa kwenda kucheza ligi zenye ushindani mkubwa nje ya nchi.

Mzize bado anahitaji kujiimarisha zaidi ndani ya Yanga, kabka ya kwenda kucheza nje ya nchi. Kinyume na hapo, mnaweza kusababisha kiwango chake kikaporomoka kwa sababu tu ya kumjaza upepo.

Samatta kacheza nusu msimu tu pale Msimbazi kwa maana nyingne kacheza ligi kuu Tz nusu msimu tu
kisha akauzwa kwenda Tp Mazembe iliyokuwa imesheheni nyota wakali enzi hizo Tp ikisumbua África

Mzize huu ndo muda na umri (20yrs japo ya kufoji) sahihi wa kwenda nje ya nchi, muda haumngoji mtu

Hersi amekosea sana kumbania huyu dogo,
Mzize atakuwa na majonzi sana ndani ya nafsi yake, atawachukia viongozi na ataichukia club kwa kumbania dili ambayo ingezidi kumpa maisha manono

Mwisho ataona bora angekuwa Simba, timu ambayo hainaga hiyana ktk kumfungulia mtu milango ya neema
 
Yaani Yanga imemlea Mzize Toka under 17
Wewe ndo unawazidi maoni juu ya mchezaji wao
Azam walimtaka zamani Kwa million 400 Yanga wanagoma, Leo thamani yake imefika billion 2
What if mwisho wa msimu wakapata 5bilions ?
Yanga wamewekeza kiasi kikubwa hadi Mzize kuwa hivi unavo muona
Wamempa makocha Bora, anazungukwa na wachezaji Bora, miundo mbinu ya mazoezi, chakula, malazi n.k
Na wao wana haki ya kupata thamani wanayohitaji

Na what if mwisho msimu isitokee timu yenye kufika dau hata la 1bn

Au kuelekea mwisho wa msimu akapata injury ya muda mrefu let say miezi 4 au 6 nje ya uwanja, maana yake hakutokuwa na timu yoyote itakayotoa hela imnunue mtu majeruhi

Kumbuka dirisha kubwa wachezaji wengi wanakuwa sokoni
 
Uko pessimistic unaamini tu itatokea negative tu kwenye maisha
Tunaamini atakuwa salama na tauzwa Kwa day kubwa
 
Yaani Yanga imemlea Mzize Toka under 17
Wewe ndo unawazidi maoni juu ya mchezaji wao
Azam walimtaka zamani Kwa million 400 Yanga wanagoma, Leo thamani yake imefika billion 2
What if mwisho wa msimu wakapata 5bilions ?
Yanga wamewekeza kiasi kikubwa hadi Mzize kuwa hivi unavo muona
Wamempa makocha Bora, anazungukwa na wachezaji Bora, miundo mbinu ya mazoezi, chakula, malazi n.k
Na wao wana haki ya kupata thamani wanayohitaji
Kuna watu wanajifanya sasa hivi ndiyo wanamfahamu Mzize kuliko hata yeye Mzize mwenyewe anavyojifahamu.
 
Yaani Yanga imemlea Mzize Toka under 17
Wewe ndo unawazidi maoni juu ya mchezaji wao
Azam walimtaka zamani Kwa million 400 Yanga wanagoma, Leo thamani yake imefika billion 2
What if mwisho wa msimu wakapata 5bilions ?
Yanga wamewekeza kiasi kikubwa hadi Mzize kuwa hivi unavo muona
Wamempa makocha Bora, anazungukwa na wachezaji Bora, miundo mbinu ya mazoezi, chakula, malazi n.k
Na wao wana haki ya kupata thamani wanayohitaji
Mzize hawezi kuuzwa bilioni 5.
 
Ifikie wakati muwe mnawasaidia kuwajenga hawa wachezaji wetu vijana na wasio na uzoefu wa kutosha wa kwenda kucheza ligi zenye ushindani mkubwa nje ya nchi.

Mzize bado anahitaji kujiimarisha zaidi ndani ya Yanga, kabka ya kwenda kucheza nje ya nchi. Kinyume na hapo, mnaweza kusababisha kiwango chake kikaporomoka kwa sababu tu ya kumjaza upepo.
Miaka kadhaa iliyopita kulikuwa na Mtanzania Hasheem Thebeet anang'aa sana kwenye mpira wa Kikapu huko Marekani. Wakati angali chuoni, alishauriwa asikimbilie NBA kwanza ili ajiimarishe lakini ofa za NBA ziliopokuja akaachana na ushauri wote wa akina Mutombo na hata mwalimu wake wa UCONN akakimbbilia NBA. Baada ya hapo hakudumu huko NBA
 
Yaani Yanga imemlea Mzize Toka under 17
Wewe ndo unawazidi maoni juu ya mchezaji wao
Azam walimtaka zamani Kwa million 400 Yanga wanagoma, Leo thamani yake imefika billion 2
What if mwisho wa msimu wakapata 5bilions ?
Yanga wamewekeza kiasi kikubwa hadi Mzize kuwa hivi unavo muona
Wamempa makocha Bora, anazungukwa na wachezaji Bora, miundo mbinu ya mazoezi, chakula, malazi n.k
Na wao wana haki ya kupata thamani wanayohitaji
Endeleni kumjaza upepo wa umuhimu huku mkimpa mshahara wa milion 3 kwa mwezi.
 
Maiaka kadhaa iliyopita kulikuwa na Mtanzania Hasheem Thebeet anang'aa sana kwenye mpira wa Kikapu huko Marekani. Wakati angali chuoni, alishauriwa asikimbilie NBA kwanza ili ajiimarishe lakini ofa za NBA ziliopkuja akaachana na ushauri wote wa akina Mutombo na hata mwalimu wake wa UCONN akakimbbilia NBA. Baada ya hapo hakudumu huko NBA
Hii stori ya Hasheem Thabeet huwa inaniuma sana.
 
Ni kweli; inatuuma sana watanzania wengi kwani ndiye aliyekuwa mtanzania pekee kuingia NBA. Angetulia kidogo akajiimiarisha chuoni mwaka mmja mwingine huenda stori ingekuwa tofauti leo. Marehemu Mutombo alicheza NBA kwa karibu miaka 20, lakini Hasheem hakumaliza zaidi miaka mitano ya kwanza ya draft.

Ni kutokana na kukurupukia ofa bila kujipima sawasawa
 
Back
Top Bottom