Mzize apata simanzi kubwa dili lake kupeperuka

Huyu Hapa Ndio Mwamba Aliyeharibu Dili la Mabilioni la Mzize Huko Libya

LILE dili la bilioni 3 limeota mbawa. Ndicho unachoweza kusema baada ya miamba ya soka ya Libya Al Ettihad kuachana na mpango wa kumsajili straika wa Yanga, Clement Mzize na badala yake kunasa saini ya raia wa Botswana.

Nyota huyo amejiunga na kikosi hicho akitokea AS FAR Rabat ya Morocco aliyojiunga nayo Januari mwaka jana akitokea USM Alger ya Algeria, ambako tangu ajiunge na miamba hiyo amecheza jumla ya michezo 21 na kufunga mabao matatu tu msimu huu.

Timu nyingine alizowahi kuchezea nyota huyo ni Olympique Khouribga ya Morocco na Township Rollers na Gaborone United za kwao Botswana, huku akishinda taji la Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023 na USM Alger, sawa na CAF Super Cup 2023.

Kitendo cha Tumisang Orebonye, kutua kwa miamba hiyo, kimefanya dili la Mzize kukwama, licha ya kiasi kikubwa cha fedha ambacho Yanga ingekipata, huku ikielezwa viongozi walikuwa tayari kumuuza, ingawa sio kipindi hiki wanachowania taji la Ligi.

Mzize amekuwa na kiwango bora akiwa na Yanga anayoitumikia kwa misimu mitatu sasa ambapo hadi sasa amefunga mabao tisa ya Ligi Kuu akiongoza mbio za ufungaji bora, huku akiasisti mengine matatu kati ya mabao 42 yaliyofungwa na timu hiyo katika mechi 17 za Ligi Kuu Bara.

Mbali na mabao hayo ya Ligi Kuu, Mzize pia amefunga mabao matano na asisti mbili katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Yanga ilitolewa hatua ya makundi na kukwama kutinga robo fainali kwa msimu wa pili mfululizo baada ya msimu uliopita kufika baada ya kupitia miaka 25 tangu ilicheza 1998.

Mzize ambaye ni zao la timu ya vijana ya Yanga, alikuwa akiwindwa na Al Ittihad iliyotenga ada ya uhamisho Sh3 bilioni, huku ada yake binafsi ya kusaini mkataba (sign-on fee), ikiwa ni zaidi ya Sh1.3 bilioni kwa mkataba wa miaka miwili.

Kuonyesha umuhimu na mchango wa nyota huyo, mbali na kiasi chote cha fedha alichokuwa amewekewa na Walibya, pia alitengewa kiasi cha mshahara wa Sh50 milioni kwa mwezi ambao kwa mkataba wake wa miaka miwili angevuna Sh1.2 bilioni, na ilipomkosa wakaamua kumnyakua Orebonye.
Sasa wewe umejuaje kama Mzize kapata simanzi
 
Kibu bado anahitajika kwenye club yake michuano ya Caf

Tukiongea kiuzalendo kabisa hili dili ilitakiwa Yanga imuachie Mzize aende huko, kwa maslahi mapana ya mchezaji mwenyewe, Yanga itapata hela na Taifa litanufaika pía kuwa na wachezaji wengi wanaocheza ligi kubwa zenye ushindani

Hersi anasema atauzwa msimu ukiisha, kumbuka msimu ukiisha wachezaji wengi ligi mbalimbali wanakuwa sokoni, hvyo soko linakuwa na ushindani mkubwa
Mkuu watu wanataka wapate Cha juu kikubwa kuliko mchezaji mwenyewe.
 
Hii stori ya Hasheem Thabeet huwa inaniuma sana.
Kwa kipindi kifupi hasheem amekiwa billionea,unafikiri kwa kucheza vikapu vya Pazi sijui Dar City angepata wapi hela za kumnunulia mama yake nyumba Masaki.

Sometimes za kuambiwa ni aheri kuchanganya na za kwako. Lets take chances when they come our way. Japo alishindwa ku maintain kwa muda mrefu ila hela alizopata Marekani ni nyingi sana kwa kipindi kifupi na hadi mwishoni alipokuwa anapocheza timu za mchangani huko Asia still ali meki meki ngawira compare na angebakia kucheza vikapu vya hapa Umatumbini.
 
Samatta kacheza nusu msimu tu pale Msimbazi kwa maana nyingne kacheza ligi kuu Tz nusu msimu tu
kisha akauzwa kwenda Tp Mazembe iliyokuwa imesheheni nyota wakali enzi hizo Tp ikisumbua África

Mzize huu ndo muda na umri (20yrs japo ya kufoji) sahihi wa kwenda nje ya nchi, muda haumngoji mtu

Hersi amekosea sana kumbania huyu dogo,
Mzize atakuwa na majonzi sana ndani ya nafsi yake, atawachukia viongozi na ataichukia club kwa kumbania dili ambayo ingezidi kumpa maisha manono

Mwisho ataona bora angekuwa Simba, timu ambayo hainaga hiyana ktk kumfungulia mtu milango ya neema
Nimeshangaa sana aisee, bilioni 3? Hii ingekua mo dewji angemuita dogo Dubai waagane vizuri ..jamaa Lina roho mbaya sana kumamakeh..Kuna siku mechi ya Simba na Orlando lilivaa jezi ya Orlando .senge mav kabisa, kwaio sishangai yeye kumfanyia roho mbaya mzize , ni roho mbaya na chuki ya wazi anaona sjui hatafaidika mana signing fee inaenda kwa mchezaji, pesa nyingine ingeingia kwenye klabu.
 
Kibu bado anahitajika kwenye club yake michuano ya Caf

Tukiongea kiuzalendo kabisa hili dili ilitakiwa Yanga imuachie Mzize aende huko, kwa maslahi mapana ya mchezaji mwenyewe, Yanga itapata hela na Taifa litanufaika pía kuwa na wachezaji wengi wanaocheza ligi kubwa zenye ushindani

Hersi anasema atauzwa msimu ukiisha, kumbuka msimu ukiisha wachezaji wengi ligi mbalimbali wanakuwa sokoni, hvyo soko linakuwa na ushindani mkubwa
Kwahio ligi ya Libya ni bora kuliko Tanzania?
 
Nimeshangaa sana aisee, bilioni 3? Hii ingekua mo dewji angemuita dogo Dubai waagane vizuri ..jamaa Lina roho mbaya sana kumamakeh..Kuna siku mechi ya Simba na Orlando lilivaa jezi ya Orlando .senge mav kabisa, kwaio sishangai yeye kumfanyia roho mbaya mzize , ni roho mbaya na chuki ya wazi anaona sjui hatafaidika mana signing fee inaenda kwa mchezaji, pesa nyingine ingeingia kwenye klabu.
Huna ulijualo kuhusu football! lini Mo aliuza mchezaji kati kati ya msimu?
 
Ukiacha roho mbaya , hii ndio sababu kuu. Na nakuambia Hilo dirisha kubwa itakuja mezani labda milioni 800 hapo imezidi sana kutoka kwenye 3 billion.
Jitahidi sana ujue vitu kabla ya ku shout kama mjinga! alikwambia nani thamani ya mchezaji inashuka kwenye dilisha kubwa? tupe evidence ya hilo usemalo
 
Huyu Hapa Ndio Mwamba Aliyeharibu Dili la Mabilioni la Mzize Huko Libya

LILE dili la bilioni 3 limeota mbawa. Ndicho unachoweza kusema baada ya miamba ya soka ya Libya Al Ettihad kuachana na mpango wa kumsajili straika wa Yanga, Clement Mzize na badala yake kunasa saini ya raia wa Botswana.

Nyota huyo amejiunga na kikosi hicho akitokea AS FAR Rabat ya Morocco aliyojiunga nayo Januari mwaka jana akitokea USM Alger ya Algeria, ambako tangu ajiunge na miamba hiyo amecheza jumla ya michezo 21 na kufunga mabao matatu tu msimu huu.

Timu nyingine alizowahi kuchezea nyota huyo ni Olympique Khouribga ya Morocco na Township Rollers na Gaborone United za kwao Botswana, huku akishinda taji la Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023 na USM Alger, sawa na CAF Super Cup 2023.

Kitendo cha Tumisang Orebonye, kutua kwa miamba hiyo, kimefanya dili la Mzize kukwama, licha ya kiasi kikubwa cha fedha ambacho Yanga ingekipata, huku ikielezwa viongozi walikuwa tayari kumuuza, ingawa sio kipindi hiki wanachowania taji la Ligi.

Mzize amekuwa na kiwango bora akiwa na Yanga anayoitumikia kwa misimu mitatu sasa ambapo hadi sasa amefunga mabao tisa ya Ligi Kuu akiongoza mbio za ufungaji bora, huku akiasisti mengine matatu kati ya mabao 42 yaliyofungwa na timu hiyo katika mechi 17 za Ligi Kuu Bara.

Mbali na mabao hayo ya Ligi Kuu, Mzize pia amefunga mabao matano na asisti mbili katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Yanga ilitolewa hatua ya makundi na kukwama kutinga robo fainali kwa msimu wa pili mfululizo baada ya msimu uliopita kufika baada ya kupitia miaka 25 tangu ilicheza 1998.

Mzize ambaye ni zao la timu ya vijana ya Yanga, alikuwa akiwindwa na Al Ittihad iliyotenga ada ya uhamisho Sh3 bilioni, huku ada yake binafsi ya kusaini mkataba (sign-on fee), ikiwa ni zaidi ya Sh1.3 bilioni kwa mkataba wa miaka miwili.

Kuonyesha umuhimu na mchango wa nyota huyo, mbali na kiasi chote cha fedha alichokuwa amewekewa na Walibya, pia alitengewa kiasi cha mshahara wa Sh50 milioni kwa mwezi ambao kwa mkataba wake wa miaka miwili angevuna Sh1.2 bilioni, na ilipomkosa wakaamua kumnyakua Orebonye.
Waarabu wakikukubali watakusajili tu huonda huyo mshambuliaji waliomsajili ni wa muda tu wakati wakisubiri target yao ambaye ni Mzize
 
Ukiacha roho mbaya , hii ndio sababu kuu. Na nakuambia Hilo dirisha kubwa itakuja mezani labda milioni 800 hapo imezidi sana kutoka kwenye 3 billion.
Watanzania wanapenda sana kutumia nyota za watu na hawaogopi hata deal yote ikiharibika kabisa.SASA HUU SI UCHAWI.
 
Yaani Yanga imemlea Mzize Toka under 17
Wewe ndo unawazidi maoni juu ya mchezaji wao
Azam walimtaka zamani Kwa million 400 Yanga wanagoma, Leo thamani yake imefika billion 2
What if mwisho wa msimu wakapata 5bilions ?
Yanga wamewekeza kiasi kikubwa hadi Mzize kuwa hivi unavo muona
Wamempa makocha Bora, anazungukwa na wachezaji Bora, miundo mbinu ya mazoezi, chakula, malazi n.k
Na wao wana haki ya kupata thamani wanayohitaji
Bira kusahau Sindano bora.
 
Mzize bado anahitaji kujiimarisha zaidi ndani ya Yanga, kabka ya kwenda kucheza nje ya nchi. Kinyume na hapo, mnaweza kusababisha kiwango chake kikaporomoka kwa sababu tu ya kumjaza upepo.
Sioni shida kiwango kikimporomokea huko huko wakati biashara imeshafanyika. Ni wachezaji wachache sana wanaweza kupata bahati ya kuingiza hela ndefu kama hiyo kwa miaka miwili.
 
Back
Top Bottom