Mzize apata simanzi kubwa dili lake kupeperuka

Mzize apata simanzi kubwa dili lake kupeperuka

Nimeshangaa sana aisee, bilioni 3? Hii ingekua mo dewji angemuita dogo Dubai waagane vizuri ..jamaa Lina roho mbaya sana kumamakeh..Kuna siku mechi ya Simba na Orlando lilivaa jezi ya Orlando .senge mav kabisa, kwaio sishangai yeye kumfanyia roho mbaya mzize , ni roho mbaya na chuki ya wazi anaona sjui hatafaidika mana signing fee inaenda kwa mchezaji, pesa nyingine ingeingia kwenye klabu.
Ni bora hata angemwambia mwanangu Mzize ktk hio hela utayokunja nimegee hata 10% ili turahisishe mambo ukale maisha arabuni, kuliko kumbania hivi huku akidhani dirisha kubwa anaweza kumuuza dau kubwa zaidi ukizingatia Yanga imetolewa group stage CAFcl hivyo inapunguza market value ya mchezaji
 
Kwahio ligi ya Libya ni bora kuliko Tanzania?
Mkuu, japo kwa ubora Tz ipo juu ila Libya wanalipa vizuri sana kuliko Tz

Na kwasasa timu zao hizi kina Ittihad, Ahly Tripoly, Ahly Benghazi wanazidi kusajili watu wa maana ili kujiimarisha zaidi kimataifa next season ya Caf
Dirisha dogo tu wamewachukua Mohamed Zrida kutoka Raja, Gerson Dala foward muAngola, Ismail Belkacemi kutoka USM Alger, Orebonye kutoka FAR Rabat nk
 
Mkuu timu gani inaweza beba garasa la kukaa siku 450 bila goli kwenye ligi? Anazidiwa mpaka na beki Mwenda mechi 3 goli 1
😅😅
Ila hilo garasa limefunga magoli ya maana ktk kufuzu robo fainali Caf

Wakati top players kina Dube, Chama, Aziz, Pacome wamekwamia makundi
 
Huyu Hapa Ndio Mwamba Aliyeharibu Dili la Mabilioni la Mzize Huko Libya

LILE dili la bilioni 3 limeota mbawa. Ndicho unachoweza kusema baada ya miamba ya soka ya Libya Al Ettihad kuachana na mpango wa kumsajili straika wa Yanga, Clement Mzize na badala yake kunasa saini ya raia wa Botswana.

Nyota huyo amejiunga na kikosi hicho akitokea AS FAR Rabat ya Morocco aliyojiunga nayo Januari mwaka jana akitokea USM Alger ya Algeria, ambako tangu ajiunge na miamba hiyo amecheza jumla ya michezo 21 na kufunga mabao matatu tu msimu huu.

Timu nyingine alizowahi kuchezea nyota huyo ni Olympique Khouribga ya Morocco na Township Rollers na Gaborone United za kwao Botswana, huku akishinda taji la Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023 na USM Alger, sawa na CAF Super Cup 2023.

Kitendo cha Tumisang Orebonye, kutua kwa miamba hiyo, kimefanya dili la Mzize kukwama, licha ya kiasi kikubwa cha fedha ambacho Yanga ingekipata, huku ikielezwa viongozi walikuwa tayari kumuuza, ingawa sio kipindi hiki wanachowania taji la Ligi.

Mzize amekuwa na kiwango bora akiwa na Yanga anayoitumikia kwa misimu mitatu sasa ambapo hadi sasa amefunga mabao tisa ya Ligi Kuu akiongoza mbio za ufungaji bora, huku akiasisti mengine matatu kati ya mabao 42 yaliyofungwa na timu hiyo katika mechi 17 za Ligi Kuu Bara.

Mbali na mabao hayo ya Ligi Kuu, Mzize pia amefunga mabao matano na asisti mbili katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Yanga ilitolewa hatua ya makundi na kukwama kutinga robo fainali kwa msimu wa pili mfululizo baada ya msimu uliopita kufika baada ya kupitia miaka 25 tangu ilicheza 1998.

Mzize ambaye ni zao la timu ya vijana ya Yanga, alikuwa akiwindwa na Al Ittihad iliyotenga ada ya uhamisho Sh3 bilioni, huku ada yake binafsi ya kusaini mkataba (sign-on fee), ikiwa ni zaidi ya Sh1.3 bilioni kwa mkataba wa miaka miwili.

Kuonyesha umuhimu na mchango wa nyota huyo, mbali na kiasi chote cha fedha alichokuwa amewekewa na Walibya, pia alitengewa kiasi cha mshahara wa Sh50 milioni kwa mwezi ambao kwa mkataba wake wa miaka miwili angevuna Sh1.2 bilioni, na ilipomkosa wakaamua kumnyakua Orebonye.
Watakuja wengine wenye dili kubwa zaidi, hiyo haikuwa ridhiki, mzize ni chuma!!
 
Samatta kacheza nusu msimu tu pale Msimbazi kwa maana nyingne kacheza ligi kuu Tz nusu msimu tu
kisha akauzwa kwenda Tp Mazembe iliyokuwa imesheheni nyota wakali enzi hizo Tp ikisumbua África

Mzize huu ndo muda na umri (20yrs japo ya kufoji) sahihi wa kwenda nje ya nchi, muda haumngoji mtu

Hersi amekosea sana kumbania huyu dogo,
Mzize atakuwa na majonzi sana ndani ya nafsi yake, atawachukia viongozi na ataichukia club kwa kumbania dili ambayo ingezidi kumpa maisha manono

Mwisho ataona bora angekuwa Simba, timu ambayo hainaga hiyana ktk kumfungulia mtu milango ya neema
Mzize anaondoka mwishoni mwa msimu, kuna dalili ataelekea Ubelgiji.
 
Kwa kipindi kifupi hasheem amekiwa billionea,unafikiri kwa kucheza vikapu vya Pazi sijui Dar City angepata wapi hela za kumnunulia mama yake nyumba Masaki.

Sometimes za kuambiwa ni aheri kuchanganya na za kwako. Lets take chances when they come our way. Japo alishindwa ku maintain kwa muda mrefu ila hela alizopata Marekani ni nyingi sana kwa kipindi kifupi na hadi mwishoni alipokuwa anapocheza timu za mchangani huko Asia still ali meki meki ngawira compare na angebakia kucheza vikapu vya hapa Umatumbini.
Nafikiri hukuelewa point kubwa inayoongelewa. Swala siyo kutopata hela, ila angekubali ushauri wa kujiimarisha kabla ya kujiunga na NBA angekuwa mbali sana kuliko alipoishia. Hebu angalia alikofikia Steph Curry aliyekuwa wa tisa wakati Hasheem akiwa wa pili kwenye draft yao.
 
Ifikie wakati muwe mnawasaidia kuwajenga hawa wachezaji wetu vijana na wasio na uzoefu wa kutosha wa kwenda kucheza ligi zenye ushindani mkubwa nje ya nchi.

Mzize bado anahitaji kujiimarisha zaidi ndani ya Yanga, kabka ya kwenda kucheza nje ya nchi. Kinyume na hapo, mnaweza kusababisha kiwango chake kikaporomoka kwa sababu tu ya kumjaza upepo.
Samata angefuatilia haya maoni Yako asingefikia pale alipo Leo....
 
Wajuaji hawaishi. Tena wajuaji ambao mwanzo walimponda leo wamekua watetezi na wakati kuna mtu amewekeza kwake mpaka leo Mzize anaonekana huyu. Huyu mwekezaji lazima na yeye aangalie maslahi yake na ya mchezaji. Hutakiwi kukurupuka kisa tu umetajiwa offer nzuri.

Mimi naamini lipo jambo jema la Mzize mwisho wa msimu. Tuendelee kula mtori nyama zipo chini
 
Watakuja wengine wenye dili kubwa zaidi, hiyo haikuwa ridhiki, mzize ni chuma!!
Fursa haimngoji mtu mkuu

Mayele alikuwa top player kwelikweli kuanzia ndani ya ligi mpaka Caf championship lakn mauzo yake hayakuzidi 3bn

Simba walishauza Kichuya wakiwa Egypt kwenda kucheza na Al Ahly Cafcl msimu wa 2018/19 dirisha dogo

Yanga wana tabia ya kubania sana wachezaji wazawa kuwauza pindi wanapohitajika
 
Huyu Hapa Ndio Mwamba Aliyeharibu Dili la Mabilioni la Mzize Huko Libya

LILE dili la bilioni 3 limeota mbawa. Ndicho unachoweza kusema baada ya miamba ya soka ya Libya Al Ettihad kuachana na mpango wa kumsajili straika wa Yanga, Clement Mzize na badala yake kunasa saini ya raia wa Botswana.

Nyota huyo amejiunga na kikosi hicho akitokea AS FAR Rabat ya Morocco aliyojiunga nayo Januari mwaka jana akitokea USM Alger ya Algeria, ambako tangu ajiunge na miamba hiyo amecheza jumla ya michezo 21 na kufunga mabao matatu tu msimu huu.

Timu nyingine alizowahi kuchezea nyota huyo ni Olympique Khouribga ya Morocco na Township Rollers na Gaborone United za kwao Botswana, huku akishinda taji la Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023 na USM Alger, sawa na CAF Super Cup 2023.

Kitendo cha Tumisang Orebonye, kutua kwa miamba hiyo, kimefanya dili la Mzize kukwama, licha ya kiasi kikubwa cha fedha ambacho Yanga ingekipata, huku ikielezwa viongozi walikuwa tayari kumuuza, ingawa sio kipindi hiki wanachowania taji la Ligi.

Mzize amekuwa na kiwango bora akiwa na Yanga anayoitumikia kwa misimu mitatu sasa ambapo hadi sasa amefunga mabao tisa ya Ligi Kuu akiongoza mbio za ufungaji bora, huku akiasisti mengine matatu kati ya mabao 42 yaliyofungwa na timu hiyo katika mechi 17 za Ligi Kuu Bara.

Mbali na mabao hayo ya Ligi Kuu, Mzize pia amefunga mabao matano na asisti mbili katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Yanga ilitolewa hatua ya makundi na kukwama kutinga robo fainali kwa msimu wa pili mfululizo baada ya msimu uliopita kufika baada ya kupitia miaka 25 tangu ilicheza 1998.

Mzize ambaye ni zao la timu ya vijana ya Yanga, alikuwa akiwindwa na Al Ittihad iliyotenga ada ya uhamisho Sh3 bilioni, huku ada yake binafsi ya kusaini mkataba (sign-on fee), ikiwa ni zaidi ya Sh1.3 bilioni kwa mkataba wa miaka miwili.

Kuonyesha umuhimu na mchango wa nyota huyo, mbali na kiasi chote cha fedha alichokuwa amewekewa na Walibya, pia alitengewa kiasi cha mshahara wa Sh50 milioni kwa mwezi ambao kwa mkataba wake wa miaka miwili angevuna Sh1.2 bilioni, na ilipomkosa wakaamua kumnyakua Orebonye.
Sijasoma lakini hakujawahi kuwa na dili la Mzize.Zilikuwa propaganda za nyuma mwiko

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom