"Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji

"Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji

Akili ni nywele kila mtu ana zake.
Hivi wewe aliyekuambia kuwa maamuzi ya kamati kuu ni KUWAFUKUZA UANACHAMA ni nani??.
Huo ni umalaya wa uandishi wa habari.
 
Mi nakukumbusha tu kuwa ile mimba ya yule kijana wako uliyemtorosha aliikibali au ndio mkamwacha binti wa watu ajizalie tu mtoto
 
Huu ni msemo wa Kiswahili kuwa Mzoea Vya Kunyonga, vya kuchinja haviwezi! Chadema ilizoea kuwanyonga wanachama wake kwa kuwafukuza kienyeji enyeji na kujinga jinga, nimeisoma taarifa hii kwa faraja.

Halima Mdee ni mwanamke shujaa, msomi na mwanasheria, anaijua katiba ya Chadema, na vikao vya mamlaka ya nidhamu ni kama ifuatavyo.
  • Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa na miongoni mwake ni hizi nitakazo ziorodhesha hapa chini, jee zilifuatwa?
  • Kuandaa Hati ya Mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?
  • Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia. Je, hili lilifanyika? Nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, je huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?
  • Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, je hili litafanyika?
  • Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba na kumwalika mtuhumiwa kwa barua ili kuwapa nafasi ya kujieleza na kumsikiliza kabla ya kufikia maamuzi!. Jee this time Chadema itafuata taratibu?
Halima na genge lake they are very right, Chadema ilizoea kufanya mambo kienyeji, leo imekutana na kisiki cha mpingo!
Chadema sasa lazima ijifunze kufanya mambo kwa kufuata katiba yake, sheria, taratibu na kanuni!, kufanya mambo kwa kienyeji enyeji kwa mtindo wa zimamoto, sasa basi!

Hongera sana Kamanda Mhe. Halima Mdee na makamanda makomandoo wa kike kwa kuifunza nidhamu chama chenu cha Chadema.

Paskali
Membe alifukuzwa kwa kuzoea vya kunyonga toka kwa malaika wa kirundi
 
Umenena logic sana mdogo wangu!
Wenyehekima watayaishi maono yako!
Hao watu ni wazuri kufikisha hoja za wananchi na kujadili mstakabali wa Taifa.

Sisi kama wanachama hatuo sababu ya kuendeleza malumbano yasiyo na tija.
Siasa ni ujira na wao washaula. Tuache roho za korosho
Mlipokuwa mnawaibia kura mlikuwa mmesahau huo uzuri wao? Unafiki huu unazidi kujenga msingi wa kuibomoa nchi
 
Kwani Lissu na Lema Wote wanaanza na herufi (L), walidai wametishiwa maisha hadi wakakimbilia ughaibuni. Je, ni kituo gani cha Polisi walikwenda kuripoti kama wanatishiwa ili wapate ulinzi? kwanini unawakomalia hawa wanawake? au na wewe ulikuwa na mpango wa kupata hata nafasi moja lakini wakakuwahi. Kwa bahati mbaya, hawa makomandoo wa Kike, hata wakifukuzwa uanachama watakwenda mahakani na kesi itakwenda kwa muda wa miaka 5. The business is OVER, Mbowe Ruzuku anavuta, na 10%zake anapata. Utatoa povu sana bila mafanikio. chukua jembe ukalime ndg...
Polisi ya wapi wangekwenda kuripoti ? Mara mia wawe wabunge wa mahakama kuliko kuwa wabunge mamluki kisa mbowe anaitaka ruzuku
 
Chadema wakubali yaishe. Walishiriki uchaguzi ili wapate kura .Wamepata wabunge 20.Si haba wawape ushirikiano wawashe moto bungeni. Waendelee kujenga chama. Na waongee hoja bungeni. Maana huku nje wakiongea wanaitwa wachochezi.

CHADEMA kama chama hawayatambui matokeo ya uchaguzi na yote yatokanayo nao.

Tume inasema ilipata orodha kwa CHADEMA kupitia katibu mkuu anayekanusha hilo.

Kwanini asibainishwe aliyeingilia mchakato huu ambayo kwa hakika ni jinai?

Mtawalazimisha CHADEMA kuyatambua matokeo haya ya wizi?
 
Mkurugenzi wa NEC kasema mnyika alipeleka majina yao tarehe 19, Sasa huelewi Nini tena?
Mkurugenzi wa NEC ni nani, huyo ni uchafu kama uchafu mwingine. Unaleta habari za watu walioratibu wizi kwenye uchaguzi, ndio unaniambia kasema?
 
CHADEMA kama chama hawayatambui matokeo ya uchaguzi na yote yatokanayo nao.

Tume inasema ilipata orodha kwa CHADEMA kupitia katibu mkuu anayekanusha hilo.

Kwanini asibainishwe aliyeingilia mchakato huu ambayo kwa hakika ni jinai?

Mtawalazimisha CHADEMA kuyatambua matokeo haya ya wizi?
Ni lini Chadema walishatambua matokeo ?Ila pamoja na kutokutambua matokeo still wamekuwa wakienda Bungeni.
 
Pascal Mayala kutoka mwandishi na mtangazaji nguli wa kipindi maarufu cha kitimoto mpaka kuwa vuvuzela la chama mufilisi cha kijani kibichi kidichokuwa na sera ,dira na mwelekeo in Horace Kolimba's voice ccm general secretary .
 
Huyo jamaa siku hizi anajitoa sana ufahamu, usipoteze nguvu zako bure
Zamani alikuwa ana akili za kumtosha. Lakini tangu ameitwa mbele ya bunge, amekuwa mtu tofauti kkabisa.Ndio amebadili msimamo wake kiitikadi hadi eti naye akawa kada wa ccm na kuomba kuteuliwa kugombea ubunge wa Kawe. Amekuwa kama zezeta siku hizi. Atafuta attention ya mfalme wao.
 
Ni lini Chadema walishatambua matokeo ?Ila pamoja na kutokutambua matokeo still wamekuwa wakienda Bungeni.

Kwa hiyo mlitegemea kuwa hata mkiiba wasipotambua matokeo watakwenda tu bungeni na maisha kama kawa, kwa sababu pori jipya Ila nyani wale wale?

Sasa imekuwa ndivyo sivyo mnaulizana mbona mwaka huu haijawa hivyo?

Kale ka "sasa basi" mliwahi kukasikia safari hii? Kwanini usidhani hako ndiyo tofauti iliyopo?
 
Kama Halima ni mwanasheria, alitakiwa kujua mwenye mamlaka ya kisheria ya kupeleka majina tume ya uchaguzi ni KM. Huu uzi unakuchoresha tu bro.
Mwenye mamlaka Ni chama sio mtu mfano mnyika angekuwa kafa na mwingine hajateuliwa majina yasingepaelekwa?
 
Back
Top Bottom