"Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji


Siku ambayo paschal mayalla aliamua kutumia real name yake kisa tu zile sifa za kuuliza swali kwa Magu nilimwambia utafurahia sasa tu ila ndo umeuza uhuru wako jumla. Kwassa hana ubavu wa kjandika kama pasco... kilichokua kinamfanya akatae kuwa si yeye pindi alipohusishwa na ID ya pasco ndicho kimemfanya aandike anayoandika sasa.
 
Paskali kuchukua ukada sioni kama ni tatizo, ni haki yake kikatiba. Nilimweleza hilo
Pili, kutoa maoni yake kama kada ya mchambuzi huru, sioni tatizo ni haki yake

Tatizo ni pale anapotoa maoni kikazi lakini akiwa amejificha nyuma ya uhuru wa maoni na haki ya ukada
Kutokana na hilo, mada zake kama hizi zimekuwa na upotoshaji ili ku-fit narratives kuliko ile haki ya maoni

Mfano, Paskali anasema vyama vya siasa ni mali ya umma.
Yes, ni mali ya umma kwasababu vina operate kwa kufuata sheria za nchi.

Vyama ni organization zenye kanuni chini ya sheria na hivyo kuwa mali ya umma kuna limitations na kuwa private entity kuna mipaka pia

Paskali anasema ni lazima CDM wapeleke Wabunge Wanawake ili kutokiuka sheria. Huu ni upotoshaji.

Viti maalumu vipo kwa mujibu wa sheria na ni takwa la kisheria.
Hapa ni kuwa ni takwa la kisheria la uwepo wa viti, si takwa la kisheria Wabunge kulazimika kuwepo.

Ni kwa msingi huo Spika Ndugai alitambua uwepo wa takwa la kisheria , lakini pia akatambua haki ya kutohudhuria, akasema baada ya vikao 3 watapoteza haki.

Wanapoteza haki kwasababu wamekataa takwa la kisheria, si takwa la wao kuwepo Bungeni.

Viti vipo kama takwa la kisheria, kwenda kama mbunge ni privilege inayotokana na takwa.
Kuteuliwa na vyama ni privilege, kuwepo bunge ni privilege inayolindwa na takwa la kisheria

Serikali au Spika wa Bunge havina haki ya kupanga nani aende, ni jukumu la vyama na hapo ndipo hoja ya kundi la wanawake inapoishia.

JokaKuu Mag3 tindo
 
Hun jipya mzee paskali.
 
Hata wakati wa uchaguzi waligombea hawa kina mama mbona hamkuwapigia debe leo ndio hashuo la kina mama
 
Tangu 2016 member ambaye kakosa haya na anayejidhalilisha kuliko memba wote ni huyu mayalla.
Heri tungekuwa hatumjui. Ana kiu lakini maji hanywi ili kumfurahisha mtu mmoja mwenye matendo yasiyo ya kibinadamu
 
MZEE UNAJIAIBISHA SANA .

HESHIMA YAKO ULIYOIJENGA KWA MIAKA 40.inapotea kwa kasi sana.

NAKUPA POLE SANA
NJAA INAKUTESA SANA.
 
Tena Bunge likianza halafu nikisikia mtu anambughudhi Esta Bulaya basi itabidi aitwe bungeni kujieleza kwenye kamati ya maadili.

Wakina Dada wa watu wamepata maslahi manono halafu wanaletewa fitina kinyume cha katiba ya nchi yetu.

Nimecheka kwa nguvu vibaya sana hizi hoja zako. Unasema cdm ifutwe, ni kweli hata mimi nashangaa kwanini haifutwi, unasema cdm wanawanyima fursa akina mama kwa sababu ya uongozi wa kibabe na porojo kama hizo, unasema uchaguzi umeisha sijui na porojo za aina hiyo. Na unataka hao wanawake wakapambana kwa hoja bungeni.

Bunge lipi ambalo kuna mapambano ya hoja? Hilo bunge si ndio hotuba za upinzani zilikuwa zinazuiwa kusomwa? Huyo Halima Mdee si ndio alikuwa anafukuzwa kila siku kwa uonevu kwa kuleta hoja zenye kero kwa serikali? Wapinzani si ndio walikuwa wahanga wa maamuzi ya kiuonevu huko bungeni, ama unadhani tumesahau. Kama umeishiwa hoja piga kimya boss.
 
Nawewe mkuu njaa njaa zako hadi kichefu chefu nisije nikakukosea adabu ngoja nikae kimya.
 
Mkuu Nguruvi3 , naomba uni tag kwenye uzi husika, nikujibu, kiukweli mimi ni mtu wa no stone unturned, ukiona sijajibu kitu, ujue sina jibu.
P
 
Bora umemkumbusha maana nilisubiri kwa hamu majibu yake na nikamkumbusha juu lakini hakutokea! Na sio kwamba hakutokea kwa bahati mbaya, bali ilibidi.
Mkuu tindo , naomba uni tag kwenye uzi husika, nikujibu, kiukweli mimi ni mtu wa no stone unturned, ukiona sijajibu kitu, ujue sina jibu.
P
 
Paskal sku hiz umekua kanjanja hovyo kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…