"Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji

"Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji

Katika suala hili nilimuuliza Pascal maswali takribani 5 mwanzoni mwa mwezi Nov. aliomba 'time out' ilikujipanga hakuwahi kurudi licha ya kukumbushwa na tindo.

Hoja aliyonijibu Paskali ni kuwa yeye kama Raia ana uhuru wa kutoa mawazo, na kwamba ukada si kigezo cha kumpoka haki yake ya msingi. Nilikubaliana naye na kumwambia kuwa 'kuna thin line' kati ya kusimamia mawazo huru na kusimamia ukada hasa nyakati hizi ambapo u-DC unapatikana kwa mayowe.

Napenda kumkumbusha Paskali kuwa katika suala hili yeye si paskali huru, ni mtumishi na kada katika mission.
Hii ni kazi aliyopewa na anaifanya kwa juhudi ingawaje hawa mafedhuli Chadema wanatia mchanga kitumbua.

Namalizia ugali wangu a ngwoge hapa Bondei. karibuni

Siku ambayo paschal mayalla aliamua kutumia real name yake kisa tu zile sifa za kuuliza swali kwa Magu nilimwambia utafurahia sasa tu ila ndo umeuza uhuru wako jumla. Kwassa hana ubavu wa kjandika kama pasco... kilichokua kinamfanya akatae kuwa si yeye pindi alipohusishwa na ID ya pasco ndicho kimemfanya aandike anayoandika sasa.
 
Paskali kuchukua ukada sioni kama ni tatizo, ni haki yake kikatiba. Nilimweleza hilo
Pili, kutoa maoni yake kama kada ya mchambuzi huru, sioni tatizo ni haki yake

Tatizo ni pale anapotoa maoni kikazi lakini akiwa amejificha nyuma ya uhuru wa maoni na haki ya ukada
Kutokana na hilo, mada zake kama hizi zimekuwa na upotoshaji ili ku-fit narratives kuliko ile haki ya maoni

Mfano, Paskali anasema vyama vya siasa ni mali ya umma.
Yes, ni mali ya umma kwasababu vina operate kwa kufuata sheria za nchi.

Vyama ni organization zenye kanuni chini ya sheria na hivyo kuwa mali ya umma kuna limitations na kuwa private entity kuna mipaka pia

Paskali anasema ni lazima CDM wapeleke Wabunge Wanawake ili kutokiuka sheria. Huu ni upotoshaji.

Viti maalumu vipo kwa mujibu wa sheria na ni takwa la kisheria.
Hapa ni kuwa ni takwa la kisheria la uwepo wa viti, si takwa la kisheria Wabunge kulazimika kuwepo.

Ni kwa msingi huo Spika Ndugai alitambua uwepo wa takwa la kisheria , lakini pia akatambua haki ya kutohudhuria, akasema baada ya vikao 3 watapoteza haki.

Wanapoteza haki kwasababu wamekataa takwa la kisheria, si takwa la wao kuwepo Bungeni.

Viti vipo kama takwa la kisheria, kwenda kama mbunge ni privilege inayotokana na takwa.
Kuteuliwa na vyama ni privilege, kuwepo bunge ni privilege inayolindwa na takwa la kisheria

Serikali au Spika wa Bunge havina haki ya kupanga nani aende, ni jukumu la vyama na hapo ndipo hoja ya kundi la wanawake inapoishia.

JokaKuu Mag3 tindo
 
Huu ni msemo wa Kiswahili kuwa "Mzoea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi"! Chadema ilizoea kuwanyonga wanachama wake kwa kuwafukuza kienyeji enyeji na kujinga jinga, nimeisoma taarifa hii kwa faraja.

Halima Mdee ni mwanamke shujaa, msomi na mwanasheria, anaijua katiba ya Chadema, na vikao vya mamlaka ya nidhamu ni kama ifuatavyo.
  • Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa na miongoni mwake ni hizi nitakazo ziorodhesha hapa chini, jee zilifuatwa?
  • Kuandaa Hati ya Mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?
  • Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia. Je, hili lilifanyika? Nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, je huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?
  • Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, je hili litafanyika?
  • Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba na kumwalika mtuhumiwa kwa barua ili kuwapa nafasi ya kujieleza na kumsikiliza kabla ya kufikia maamuzi!. Jee this time Chadema itafuata taratibu?
Halima na genge lake they are very right, Chadema ilizoea kufanya mambo kienyeji, leo imekutana na kisiki cha mpingo!
Chadema sasa lazima ijifunze kufanya mambo kwa kufuata katiba yake, sheria, taratibu na kanuni!, kufanya mambo kwa kienyeji enyeji kwa mtindo wa zimamoto, sasa basi!

Hongera sana Kamanda Mhe. Halima Mdee na makamanda makomandoo wa kike kwa kuifunza nidhamu chama chenu cha Chadema.

Paskali
Update:
Mkuu mode, bila kuingilia uhuru na mamlaka ya mode ku edit bandiko lolote na heading yoyote, ila heading inapotumia tamathali za semi, methali au nahau, neno hilo linapaswa kuwa vile vile lilivyo!. Mode hapaswi kulibadili!. Nimetumia neno
"Mzoea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi", hivi ndivyo neno rasmi lilivyo, ni tofauti na neno "

"Mmezoea vya kunyonga hamviwezi vya kuchinja"​

P
Hun jipya mzee paskali.
Screenshot_2020-11-29-04-18-07-662_com.quoord.jamiiforums.activity.jpeg
 
Mh. Pascal kwa hili kwa kweli ni kipimo halisi cha Demokrasia inayopiganiwa na Chadema. Watuonyeshe sasa kuwa hicho ni chama chenye Uhuru ,haki na maendeleo ya watu.

Kuwafukuza mama zetu na Dada zetu waliokipigania chama kwa miaka na kutoa sehemu ya mishahara yao kukijenga huku wanaume wakiwa waoga na wasaliti ni kuendeleza udikteta na ukatili kwa mama zetu waliojitoa kupigania Uhuru ,haki na maendeleo ya watu.

Atafutwe aliyepeleka majina ya nafasi hizo za ubunge na sio walioteuliwa na tume baada ya kupokea majina.

Wao wameitwa baada ya majina yao kufika kwenye tume. Kosa lao ni nini ?
Maendeleo ya watu ni pamoja na kuheshimu fursa za wakinamama zinazowapa kipato kikatiba.

Mh. Pascal nakuomba sana endapo watawafukuza hao Wakinamama walioteuliwa kulingana na katiba ya nchi yetu na hawakujipendekeza bali majina yao yalipelekwa na mtu asiyejulikana , basi tumuombe Msajili wa vyama akifute hicho chama haraka sana mana sio chama cha siasa na hakifuati katiba ya nchi.

Chama gani hicho cha siasa ambacho hakijali maslahi ya Nchi,wala maslahi ya wanachama wake waliokipigania !
Hicho chama kipo kwa ajili ya nani hasa mana kwa wananchi hakijali maslahi yao,kwa taifa hakijali maslahi mapana kwa taifa letu .
Kwa nini kisifutwe !!
Mbowe abadili mfumo wa kuongoza chama kidikteta na kuwaumiza wanachama na viongozi wenzake waliokipigania chama kwa miaka mingi.

Uchaguzi umepita na walioumizwa na uchaguzi huo hawana sababu ya kuendeleza dhulma inayodhaniwa kuwa ilifanyika kwa kuwaumiza wakina mama ili wakose maslahi yao yatakayowapa nguvu ya kukijenga chama na kuongoza BAWACHA wakiwa na nguvu ya kiredha na heshima kama wabunge. Lakini pia tunataka watu wa kubishana kwa hoja bungeni jambo ambalo wale 20 wanaliweza.
Hata wakati wa uchaguzi waligombea hawa kina mama mbona hamkuwapigia debe leo ndio hashuo la kina mama
 
Tangu 2016 member ambaye kakosa haya na anayejidhalilisha kuliko memba wote ni huyu mayalla.
Heri tungekuwa hatumjui. Ana kiu lakini maji hanywi ili kumfurahisha mtu mmoja mwenye matendo yasiyo ya kibinadamu
 
MZEE UNAJIAIBISHA SANA .

HESHIMA YAKO ULIYOIJENGA KWA MIAKA 40.inapotea kwa kasi sana.

NAKUPA POLE SANA
NJAA INAKUTESA SANA.
 
Tena Bunge likianza halafu nikisikia mtu anambughudhi Esta Bulaya basi itabidi aitwe bungeni kujieleza kwenye kamati ya maadili.

Wakina Dada wa watu wamepata maslahi manono halafu wanaletewa fitina kinyume cha katiba ya nchi yetu.

Nimecheka kwa nguvu vibaya sana hizi hoja zako. Unasema cdm ifutwe, ni kweli hata mimi nashangaa kwanini haifutwi, unasema cdm wanawanyima fursa akina mama kwa sababu ya uongozi wa kibabe na porojo kama hizo, unasema uchaguzi umeisha sijui na porojo za aina hiyo. Na unataka hao wanawake wakapambana kwa hoja bungeni.

Bunge lipi ambalo kuna mapambano ya hoja? Hilo bunge si ndio hotuba za upinzani zilikuwa zinazuiwa kusomwa? Huyo Halima Mdee si ndio alikuwa anafukuzwa kila siku kwa uonevu kwa kuleta hoja zenye kero kwa serikali? Wapinzani si ndio walikuwa wahanga wa maamuzi ya kiuonevu huko bungeni, ama unadhani tumesahau. Kama umeishiwa hoja piga kimya boss.
 
Nawewe mkuu njaa njaa zako hadi kichefu chefu nisije nikakukosea adabu ngoja nikae kimya.
 
Katika suala hili nilimuuliza Pascal maswali takribani 5 mwanzoni mwa mwezi Nov. aliomba 'time out' ilikujipanga hakuwahi kurudi licha ya kukumbushwa na tindo.

Hoja aliyonijibu Paskali ni kuwa yeye kama Raia ana uhuru wa kutoa mawazo, na kwamba ukada si kigezo cha kumpoka haki yake ya msingi. Nilikubaliana naye na kumwambia kuwa 'kuna thin line' kati ya kusimamia mawazo huru na kusimamia ukada hasa nyakati hizi ambapo u-DC unapatikana kwa mayowe.

Napenda kumkumbusha Paskali kuwa katika suala hili yeye si paskali huru, ni mtumishi na kada katika mission.
Hii ni kazi aliyopewa na anaifanya kwa juhudi ingawaje hawa mafedhuli Chadema wanatia mchanga kitumbua.

Namalizia ugali wangu a ngwoge hapa Bondei. karibuni
Mkuu Nguruvi3 , naomba uni tag kwenye uzi husika, nikujibu, kiukweli mimi ni mtu wa no stone unturned, ukiona sijajibu kitu, ujue sina jibu.
P
 
Bora umemkumbusha maana nilisubiri kwa hamu majibu yake na nikamkumbusha juu lakini hakutokea! Na sio kwamba hakutokea kwa bahati mbaya, bali ilibidi.
Mkuu tindo , naomba uni tag kwenye uzi husika, nikujibu, kiukweli mimi ni mtu wa no stone unturned, ukiona sijajibu kitu, ujue sina jibu.
P
 
Paskal sku hiz umekua kanjanja hovyo kabisa

Back
Top Bottom