Mzozo wa Urusi na Ukraine wafukuta zaidi

Mzozo wa Urusi na Ukraine wafukuta zaidi

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827

Je, vikosi vya Urusi vinajiandaa vita nchini Ukraine?​


Urusi inasema haina mipango wa kufanya uvamizi

Ni miaka saba tu iliyopita wakati Urusi ilipomega sehemu ya Ukraine na kuwaunga mkono waasi walioanzisha mzozo sehemu kubwa na mashariki.

Urusi inasema haina mipango kama hiyo, kwa hivyo ni kipi kinaendelea?

Ukraine iko wapi?​

Ukraine iko kwenye mipaka ya Muungano wa Ulaya na Uusi lakini kama sehemu ya iliyokuwa Jamhuri ya Usovieti, ina uhusiamo wa ndani wa kijamii na kitamaduni na Urusi na lugha ya kirusi ndiyo huzungumzwa sana huko.

Urusi kwa kipindi kirefu imepinga hatau za Ukraine kuegemea taasisi za Ulaya na takwa lake kuu ni kwamba isiweze kujiunga na Nato au isiwe na miundo mbinu ya Nato kwenye ardhi yake.

Wakati Ukraine walimtimua rais aliyekuwa anaegemea upande wa Urusi mwaka 2014, Urusi iliteka na kuimega rasi wa Crimea na waasi wanaoungwa mkno na Urusi wakateka sehemu kubwa ya mashariki mwa Ukraine inayofahamika kama Donbas.

Kuna hatari ya uvamizi?​

Mzozo huo wa mashariki umeendelea hadi leo. Ukraine inasena Urusi imeweka vifaru na walenga shabaha mstari wa mbele katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi.

Lakini ni zaidi ya wanaeshi 90,000 wa Urusi karibu na mpaka wa Ukraine wanaozua wasi wasi.

Hakuna tishio au iwapo Rais wa Urusi Vladimir Putin ameamua kufanya uvamizi.

Msemjai wa serikali ya Urusi ametoa wito kwa kila mmoja kutulia. Lakini idira za ujasusi za magharibi pamoja na za Ukraine wanadai kuwa huenda ukatokea mapema mwaka 2022.

Mazoezi ya Urusi huko Crimea mnamo Machi 2021 yalisababisha wasiwasi mkubwa katika nchi za Magharibi

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Wakati ambao uvamaia huo unaweza kuwa tayari ni mwisho mwa Januari, kwa mujibu wa waziri wa ulinzi wa Ukraine Oleksiy Reznikov.

Idara za ujasusi za Marekani zinasema hadi wanajeshi 175,000 wa Urusi wanaweza kushiriki ifikapo mapema Januari na mkurugnezi wa CIA William Burns anaamini Rais Putin anapanga idara za ulinzi za Urusi katika mahala ambapo zinaweza kuchukua hatua kwa pamoja

Kitini cha vyombo vya habari kikimuonesha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwenye mstari wa mbele tarehe 6 Desemba

CHANZO CHA PICHA, EPA

Tumekuwa hapa awali , mwezi Aprili mwaka huu, Lakini wakati huo Urusi ilikusanya idadi ndogo ya wanajeshi kama mazoezi kisha kuwandoa. Kabla ya mkutano kwa njia ya video kati ya Bw Putin na Rais wa Marekani Joe Biden tarehe 7 Desemba viongozi watano wa nchi za magharibi walitoa wito kwa Urusi kuzima misukosuko.

Urusi inasema nini?​

Hapo awali Urusi ilielezea picha za setilaiti zikionyesha kuongezeka wanajehia huko Crimea na maeneo yaliyo karibu na mashariki mwa Ukraine kama uvumi.

Urusi ilijibu kwa kuilaumu Ukraine kwa kupeleka nusu ya wanajeshi wake ambao ni karibu 125,000 mashariki, ikidao kuwa Ukraine inapanga kushambulia maeneo yanayodhibitiwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi. Ukraine inasena kuwa hizo ni propaganda kufukina mipango yake Urusi.

Madai ya Urusi yanaweza kuwa mbinu za kuhalalisha hatua za kijeshi.

Vladimir Dzhabarov, ambaye ni namba mbili katika kamatai inayohusika na masuala ya kimataifa, alisema mapema Desemba kuwa watu nusu milioni katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi kwa sasa wana pasipoti za Urusi. Iwapo viongozi wa waasi wataomba msaada wa Urusi, hatuwezi kuwatelekeza washirika wetu, alisema.

Ni kipi Urusi inataka?​

Rais Putin ameonya nchi za magharibi zisivuke mistari miekundu ya Urusi kuhusu Ukraine.

Kwa hivyo mistari miekundu ni ipi?​

Moja yao ni kuzuia kuendela kupanuka kwa Nato kwenda mashariki na kupelekwa silaha kwenda nchi majirani hali inayoweza kuhatarisha usalama wa Urusi.

Kuna uhasama kufuatia hatua za Ukraine ya kutumia ndege zisizo na rubani za Uturuki dhidi ya waasi wanaoungwa mkono na Urusi mashariki mwa Ukraine na mazoezi ya kijeshi ya vikosi vya nchi za magharibi huko Black Sea.

Julai mwaka 2021 kiongozi huyo wa Urusi alichapisha nakala kwenye wavuti wa serikali ya Uruis akielezea kwa kina historia ya mataifa hayo la kuwataja viongozi wa sasa wa Ukraine kama walio na mradi wa kuipinga Urusi. "Kwa wale wanaoigeukia Urusi kwa njia hii wanaharibu nchi yao," alisema.

Urusi pia imechanganyikiwa kuwa mkataba wa amani wa mwaka 2015 wa Minsk uliokuwa na lengo kuzuia mgogoro wa Ukraime haujatekelezwa.

Nato inaisaidia Ukraine kwa njia gani?​

Nato inaitetea Ukraine na katibu wake mkuu Jens Stoltenberg, ameweka bayana kuwa msaada wowote wa kijeshi uko kwenye misingi hiyo.

Uingereza inatarajiwa kuisadia Ukraine kujena kambi mbili za jeshi la wanamaji, huko Ochakiy Black Sea na pia huko Berdyansk kwenye bahari ya Azov.

Makombora ya Marekani ya kuharibu vifaru pia yamepelekwa Ukraine na mashua mbili za ulinzi wa pwani zimepewa jeshi la Ukraine.

"Ni uamuzi wa Ukraine na washirika wake 30 kuamua iwapo Ukraine iko tayari kujiunga na Nato," Stoltenberg amesema.Urusi haina kura ya turufu, haina haki ya kuingilia mpango huo.

Nchi za magharibi zitaisaidia Ukraine kwa kiwango gani?​

Marekani imeweka bayana kujitolea kwake kuisaidia Ukraine kulinda uhuru wake lakini Rais Biden ameashiria kuwa hatua za kijeshi haziko mezani.

Kwa hivyo hata kama Marekani itakataa kutambua mistari miekundu ya Urusi kuhusu kujiunga na Nato au kitu kingine, itafikia wapi katika kuisaidia Uk unaamuliwa na Ujerumani.

Pia kuna hatua dhidi ya benki za Urusi za kuzizuia kutobadilisha sarafu ya Urusi kwenda sarafu za kigeni
 
“Russia conducts peace-loving foreign policy, but we have a right to provide for our own safety,” he said on Wednesday in Sochi, after meeting with the Greek prime minister. It would be “criminal” for Russia to stand back and watch NATO expand to Ukraine, he added.
====
NATO Wajitafakari.
 
Putin ni mbabe kiuhalisia....EU na US wanalia lia tuu
The last kick of a dying horse. Putin kaona wanataka kumzunguka mpaka nyumbani kwake mwishowe wampige mande. Anachimba biti tu hapo hakuna vita na mwishowe Ukraine itajiunga na NATO.
 
Hapo magharibi watapiga kelele wee, lakini hawana cha kuzuia kama Urusi ataamua jambo lake.

Now Marekani anaonja adha ya kuwa bullied maana kawaBully wengi sana zamani.
That mighty "eagle"on the US flag knows no fear, when it spreads its wings and claws, the "snow bear" suffers diarrhea.
 
The last kick of a dying horse. Putin kaona wanataka kumzunguka mpaka nyumbani kwake mwishowe wampige mande. Anachimba biti tu hapo hakuna vita na mwishowe Ukraine itajiunga na NATO.
Hujaelewa , Ukraine tayari ni member wa nato
 
The last kick of a dying horse. Putin kaona wanataka kumzunguka mpaka nyumbani kwake mwishowe wampige mande. Anachimba biti tu hapo hakuna vita na mwishowe Ukraine itajiunga na NATO.
Wakiendelea anafumuliwa mtu
 
Back
Top Bottom