Mzozo wa Urusi na Ukraine wafukuta zaidi

Kweli we mtaalamu sana wa mambo ya kijeshi!!!
Hao NATO wanaomba ulinzi kwa Marekani.
 

 
What a brilliant comment!! Kelele site za USA kuzuga Dunia kwamba Urusi hiko mbioni kuivamia Ukraine huo ni ukaghai mtupu wenye lengo lla kutafuta kisingizio cha ufunguzi wa mradi wa gesi Nord2 Stream
 
Kwani hiyo gas mrusi anasupply bure,,nadhan analipwa. Kwahiyo akizuia atakuwa anajikosesha mapato ambayo ni muhimu sana kuendwshea vita. Huwezi pigana vita kama huna pesa.
 
Kwani hiyo gas mrusi anasupply bure,,nadhan analipwa. Kwahiyo akizuia atakuwa anajikosesha mapato ambayo ni muhimu sana kuendwshea vita. Huwezi pigana vita kama huna pesa.
Na nchi nyingi za ulaya magharibi zinategemea gesi ya mrusi kwa kiasi kikubwa wakisema waachane nayo alternatives zilizokuwepo ni ghali sana kiasi cha kwamba hata wao wenyewe waweka vikwazo watayumba, wangekua na uwezo huo wangeshatunisha msuli mapema sana,, bila gesi ya mrusi gharama za maisha kwenye nchi zao zitapanda hapo wataanza kupambana na wananchi wao kwanza na pili hata viwanda vyao vitayumba..............bado hawana alternative ya gas ya bei rahisi zaidi ya kwa mrusi
 
Hitler bila mrusi angeshatawala ulaya yote.........jamaa aliwatuliza wote si Muingereza wala mfaransa ila akaharibu alipokichafua na mrusi....na ndo ukawa mwisho wa Hitler
 
Kwamba NATO wanapigana kwa kutumia mawe na mapanga? Urusi hana ubavu kwa NATO.
 
Tuambie vita gani NATO kashinda dhidi ya URUSI ,
Vita Baridi. USSR is no More.

Nawewe tueleze,Kwanini Russia anaogopa Ex-Soviet states kujiunga NATO?

Kwanini Urus inaogopa Ukraine na Goergia zisijiunge NATO? Kwasababu ndio utakuwa mwisho wa Urus kuzivamia Nchi ndogondogo ambazo zamani zilikuwa kwenye muungano wa USSR.

Urus haiwezi kuthubutu kuvamia mwanachama yeyote Yule wa NATO,Hilo inalijua ndio maana Urus Inafanya juu chini Ukraine na Georgia wasijiunge NATO.

Kutokana na Mgogoro wa Ukraine ambao unafukuta hivi Sasa,Tayari Wizara ya Mambo ya nje ya Urus imepeleka mapendekezo yake nchini Marekani ili irudishe majeshi yake Nyuma kwenye Mpaka na Ukraine. Moja ya Mapendekezo hayo Ni NATO isikubali Ukraine na Goergia kujiunga NATO.

Karibu Mkuu wa NATO,Jern Stotenburg ameshaiambia Urus kwamba Jukumu la Ukraine na Goergia kujiunga au kutokujiunga na NATO lipo juu ya wanachama wa NATO na Sio Vitisho vya Urus.
 
Hitler bila mrusi angeshatawala ulaya yote.........jamaa aliwatuliza wote si Muingereza wala mfaransa ila akaharibu alipokichafua na mrusi....na ndo ukawa mwisho wa Hitler
Well said, kwa bahati mbaya ni watu wachache watakuelewa!! Lakini ukweli wa historia ya WW2 ni kwamba ni jeshi la Urusi ndilo lilivunja uti wa mgongo wa jeshi matata la Hitler - mataifa mengine specifically US na UK utumia media zao kupindisha/kupotosha ukweli huo, hivi sasa USA imefikia hatua ya kushawishi nchi za Ulaya kwamba waviondoe kwenye mashelves ya Libraries zinazo tumiwa na: Public, Schools and Colleges yaani waondoe vitabu vya historia ya kweli kuhusu WW2 badala yake wavi - replace na vitabu vinavyo sema kwamba Amerika ndio ilishinda WW2, just imagine - cha ajabu baadhi ya Viongozi wa huko Ulaya wanaelekea kukubali upotoshaji mkubwa wa historia - lengo kuu la upotoshaji huu wanataka vijana wa Ulaya wa amini kwamba bila ya Ulinzi wa majeshi ya USA barani Ulaya basi watavamiwa na Majeshi ya Urusi (Russians are coming!!) ulaghai mtupu wenye lengo la kuhalalisha kuendeleza uwepo wa majeshi ya USA barani Ulaya miaka nenda rudi.
 
Ninachokijua mimi ni kuwa Urusi akiamua jambo lake basi uwa hakuna wa kuweza kumpinga zaidi ya kuishia tu kuweka vikwazo.
 
Ni kweli hwkunq nchi yoyote kumzui urusi kwa jqmbo lolote wanakimbia kwenye vikwazo Ila vikwazo vinaisha vyenyewe
 
Urusi kuogopa ex soviet states kujiunga NATO inaeleweka kabisa. Kwanza kabisa kihistoria vita zote zilizoihusisha Urusi na nchi husika ilikuwa ni kwa mataifa ya magharibi kuivamia Urusi. Napoleone na Hitler ni mfano.

Kwa fikra za kawaida kabisa lazima Urusi wayaogope mataifa ya magharibi ni kama wanatamani kuiteka Urusi hasa kwa ajili ya rasrimali zake so sijui kwa hali hii Warusi watachukuliaje poa nchi majirani zake hasa former soviet states kuendelea kujivuta kwenye sphere ya influence za magharibi.

Kingine NATO ilianzishwa rasmi kwa ajili ya kudeal na SOVIET. Urusi kama mrithi wa soviet anajikuta naturally adui yake mkubwa ni NATO. Hivi hata ungekuwa wewe ungechukulia poa nchi jirani zako kuendelea kujiunga kwenye organisation iliyoanzishwa kwa ajili ya kukuangamiza.

Iweke hata kwenye context ya level ya familia. Kwamba una adui anaekutakia kifo ila yuko mbali halafu uone anaanza uswahiba na jirani yako mixer unashuhudia analeta mzigo wa mapanga, mishale na siraha zingine kwa jirani yako halafu uchukulie poa! Utakuwa hujielewi lazima umuulize jirani bana.

Lakini pia sijui kwanini pro Americans hamuelewi Urusi kukwazwa na majirani kujiunga NATO ila mnaelewa USA kuwa mkali pale nchi za Amerika zinapotaka mahusiano hasa ya kiusalama na nchi kama Urusi na China. Kwanini USA alikuwa mkali during Cuban missile crisis. Sababu si hizo hizo zinazomfanya Urusi leo akose amani?

Taifa lolote kubwa lazima liwe sensistive kwenye mambo ya usalama haijalishi ni Urusi, Usa au China.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…