Mzumbe dons in PhD scam

Ndio maana hata Research hawafanyi, wamekalia kuwadisco watoto wa watu tuu. Hivyi vyuo hata WebCT havina yaani huwezi hata kuprove grade za mwanafunzi. what a mess

Kingine ni AIU [American Intercontinental University] chuo kama sebule yetu pale tabata. Nashangaa ukiingia Ebsco kutafuta publication za Tanzania utashangaa waandishi wengi ni Wazungu, sasa najiulizaga huu uyoga wa vyuo una kazi gani??

Sasa kisha mnalalamika credebility za wanafunzi. Bungeni sasa ndio kumejaa hizo degree za London school of commerce. Yaani it's a mess. Na watoto wao wemekuja huku wamekwenda AIU na kuchukua hizo hizo degree feki kama baba zao, na sasa ndio ma Marketing tycoon huko sijui Voda, tigo and zain ndio maana nashangaa baadhi ya strategy zinazokuwa implimented zinanifanya nijiulize who craft that peace of non sense. Mungu ibariki Tanzania
 
BADO YANAKUJA meeengi. Tunaangalia hawa wanaojiita Dr, Dr au maprofessor. Lakini kuna mwanzo, yaani hata wale wanaotafuta Bachellors. Kuna BSc na BA nyingi feki na ziko maofisini. Pale Kampala kuna Chuo kinajiita Kampala International ... Hapo waganda wanafahamu ni chuo cha wa-Tz na wakenya. Waganda hawasomi kabisa maana wanafahamu cheti cha hapo hakiuziki mtaani kwao. Sisi tumejaza watoto wetu ili wapate degree bila ku-disco eti! Rais wetu kaweka na siasa hivi majuzi akafungua tawi la CCM ndani ya chuo kilico ndani ya Uganda!!!!!

Sasa pale UD pia tuambieni. UDSM pamoja na Mzumbe quality ya hizo MBA executive ikoje??? Nasikia inaitwa yebo-yebo. Ndo mambo ya PWU hayo. Ni hakuna kitu!

UDSM na Muzumbe mumekuwa ni wazalishaji wa masters kibiashara. Kila mtu anaqualify kusoma hizo executives zenu. Stupid!
 



mbona unapaa hivyo, anza na degree kwanza, watu kusikiliza lectures kupitia madirishani! si mchezo
 
PhD za Bongo zimekuwa ni kama fasheni tu, kuna sababu nyingi sana. Kwanza Tanzania ina culture of silence ni hivi majuzi tu watu wameanza kupigia kelele mafisadi na wengine humu kwa majina ya bandia tunapiga kelele kweli huku tukiwa tumejaa woga wa kujulikana.

Utamaduni huu umefanya transparency kuwa ni mwiko kila kitu ni siri, nyaraka za serikali siri, ukitaka information sehemu yoyote ni siri na hata kuipata ni kazi kweliweli na ukiipata imebadilishwa na kupotosha.

Tukirudi kwenye mada PhD ni research training, Yaani ukifuzu kufanya research zenye kiwango kinachokubaliwa basi unakabidhiwa hiyo PhD ili uendeleze Research. Sasa mazingira ya Tanzania Research hazilipi, na nyingi ya research zinakuwa na pre determined results na biasness kama zile za REDET n.k. Upatikani wa data ni mgumu sana hasa secondary data, ambazo huku kwa wenzetu ni za kumwaga na hata ukitaka kila mwezi kutoa paper unaweza. Hilo kwa bongo ni ndoto, watu wanatafuta vyeti ili wapandishiwe mishahara basi. Research hazina incentives.

Pendekezo

Nafikiri kukiwa na Board ya Taaluma ambayo itakuwa na kazi kuwasajili watu wote wenye PhD Tanzania na kuwataka kila mwaka wapublish paper mbili ili PhD zao kuendelea kuwa recognised tutaweza kutenganisha pumba na mchele. usiposubmit paper inayokubalika kwa miaka mitatu whether mfululizo au kuwa na gap basi utatakiwa kuidefend upya thesis yako mbele ya baraza ili uendelee na status ya PhD hapo tutakuwa tumepiga hatua.

Kitu kingine ni kuwa na "pragiarism software", yaani iwe ni lazima kwa kila taasisi ya elimu ya juu kuwa na software hizo ambazo wanafunzi watatakiwa kusubmit kazi zao kupitia software hizo, ili atakaye copy ajulikane.

Kwa jinsi ilivyo sasa ni vigumu kwa mwalimu kugundua kuwa kazi unayosimamia ni original kwani wanafunzi wamekuwa wajanja na wanajifua vilivyo kudefend kazi za watu wengine.
 
mbona fake degree ni nyingi sana na ndugu zetu wakenya wanaongoza afrika mashariki (soma daily news ya leo) jamaa waliapply zaidi ya mia mbili and 12 were shortlisted for the post and only to find that only two held genuine certificate. there one kenyan found with fake degree at St John University at Dodoma. haya ndio mambo yote nasema ya kutafuta njia panda. hata mimi nikitaka hiyo fake degree napata lakini niko busy naandika proposal for PHD ili wakati nikija kusoma na kupata nijisikie furaha kuwa at least i deserve sio kwa kupewa.

Kweli Mzumbe imetia aibu that a perso rose up to Vice Chancelor position with fake PHD certificate. what a shame to all of us. TCU kaza buti.
 

Wakenya wamezidi magilini. Kuna jamaa nilikuwa nao shule kipindi flani huko nyuma, karibu wote waliokuwa na scholarship ukiwauliza watakwambia nafundisha university, kumbe wala si kweli coz wengi wao baadae huja kujikuta wanasema ukweli...."aagh nilisema tu ili nipate scholarship, niko mtaani". Kuhusu Mzumbe namesikia kuwa aliyekuwa VC kaingia tena shule apate PhD ya ukweli. Tatizo la wabongo tunapenda short cut!!!! kila kitu tunataka tukipate fasta bila hata ya kukisotea.... hapo ndipo shida inapoanza!
 

Haya matatizo na msimamo finyu tulionao, Huwezi kuhalalisha uchafu wako kwa kulinganisha na wa mwenzako kwa kusema kuwa mimi nina uchafu mdogo kuliko jirani yangu, uchafu ni uchafu tu ni lazima usafishwe wote hata kama ni kwenye kinibu. Eti umefumaniwa ugoni unasema wewe ndiyo mara ya kwanza kufumaniwa kwani fulani kisha fumaniwa mara kumi. Hii haihalalishi ugoni wako hata kidogo
 
......Kuhusu Mzumbe namesikia kuwa aliyekuwa VC kaingia tena shule apate PhD ya ukweli.

Tatizo kubwa hapa ni cost benefits. Ni haki kumpeleka mtu wa close to the age of 60 kusoma PhD? Anasoma kwa kutumia pesa ya nani na kwa faida ipi? Kama ni pesa ya Serikali, basi ni aibu. Yaonekana wamepania angalau waitwe Drs ki-halali.

Hizo pesa zingetumika kumusomesha kijana wa miaka 25 ili akitumikie chuo kwa miaka zaidi ya miaka 30! That is another leadership failure.
 
Tuwe na mahali pa kuanzia. Wakati wa vitendo ni huu. Tuanzie kwa kuipa meno kisheria TCU (kama bado haina meno hayo) ifanye ukaguzi kwa academic staff vyuo vyote vikuu nchini (public and private) kubaini wahadhiri vihiyo. Tusichelewe zaidi maana kila mwaka tunatoa matunda dhaifu mengi ambayo ni mabomu kwa maendeleo ya taifa. Ukaguzi ukianza, wahadhiri wenye shahada feki watajiondoa wenyewe kuogopa mkono wa sheria. Walau tuanze kuwaondoa vihiyo hao katika system ya ufundishaji vyuo vikuu na tuanze kuwa serious kuunda cream. Utitiri wa vyuo vikuu nchini, na uhaba wa wahadhiri uliopo, na bila ya kuwepo ukaguzi, basi vihiyo wengi watashika chaki vyuo vikuu na kupoteza maana kabisa ya university which is supposed to a centre of academic excellence in research, training and outreach (consultancies). lecturer mwenye PhD au Masters ya copying and pasting atawezaje kukifanya chuo kikuu a centre of academic excellence! Ni aibu kuwa sasa tumefikia mahala hata wakenya wanajazana vyuo vikuu vyetu kufundisha wakati hawana taaluma hizo. Private universities hasa zimulikwe sana. Zimejaa wakenya wasio na taaluma husika kwa kazi wanazoombea. Wanatudanganya kwa kuongoea kiingereza, na kwakuwa VCs au deputy VCs tulionao au afisa utumishi au bodi ya uajili ina vihiyo wa shahada feki kibao, basi wakati wa usaili mkenya huyu akiongea kiingereza (tena kibovu)wanamuona ndiye mtaalamu babu kubwa na kumpa ajira hapohapo. TCU ikiwa na meno kamili na kufanya compulsory (regular) inspections, uchafu huu utakimbia wenyewe.
 
Last edited:

Mkuu,

Hao Mzumbe wote wameambiwa warudi kusoma shule za kweli kweli na wamepewa muda vinginevyo hizo Ph.D zitafutwa.

Hizo shule zetu kwa sasa ni mungu ibariki Tanzania, tusitegemee wasomi walio wengi ambao wanatumia vichwa vyao kufikiri yaliyo ya maana. Ukifundishwa na walimu kama hao unategemea nini?
 
........akishirikiana na MUSHOBOZI..........naye sijui yuko wapi.......

niko masomoni, ninabukua, sikotayari kuunganisha mambo zaidi na mwishowe nikaambulia ukihio. muda ukifika nitarudi. ila ninadharau hadidhi za abunuswi. wewe unaonekana mwanahesabu, hivi, vihio 7 kati ya wazuri 200 inaweza kufanya chuo feki au ni probability inapiga chenga. any way ninachokiona ni ushindani wa kichuo na ushindani huu ni advantage kwa mzumbe kujipanga upya. hata nkunya ni mshindani maana ni walewale waliokuwa wanazibia vyuo vingine kuwa vyuo vikuu akiwa DVC academic pale UDSM.
 

Buana Mushobozi, in fwacti lazima ukubali kuwa hadhi ya Mzumbe imedidimia from bad to worse kwa hii revelation.
Probability yako ya kiMzumbe ina dosari.Vihiyo 7 , tena akiwemo VC,toosha kabisa kuua morali ya kwenda pale, kwa mtu aliye serious na masomo.
Nakubaliana kuwa kuna ushindani ,lakini ushindani huu si wa kupapatikia titles, bukua bwana utoe researches za kuleta matumaini kwa watanzania, sio kujibanza katika vichochoro vya PWU or whatever that stands for.
Pata PHD safi, na hata mtu ukitoa mada wasomi waseme yes, we have gained from this fellow.
 

that's what i do with alot of publications in the web, though by then I had a single degree. the first thing as others have said is what I should do for the purpose of poor citzens, sio what I am with poor citzens.

sitetei uvihio, ila bwana mzumbe is the best to compare, agree with me or not.
 

nO! SIO MATATIZO, huwezi kukaa, kulala na kufikia decision kwenye pandora's box bila kujua wengine wanaishije. ndio maana tunatumia syllubi zilizojaa case studies za nje in order to develop and advance. hatutakaa na kujua kama tumepiga hatua au la kama hatulinganishi maendeleo yetu na maendeleo ya wengine, au na weekness ya wengine. ndio maana tunaweza sema kuwa US is a superpower and Tanzania is a poorest country. All these a comparative analysis. be careful
 
 
 

Well done Masanja, from your contribution one notes that your sort of people is what academic exellence is reffered to!
 
Duh:

Naona mjadala mzima umegeuka kuwa Mzumbe vs UDSM. Ukweli wa mambo unabakia kuwa wanaosoma Mzumbe au vyuo vingine ni watanzania kama wale wanaosoma UDSM. Na wajibu wao kwa taifa ni hulehule.

Vilevile mtu mwenye advance diploma anaweza kwenda kuchukua Masters period.

Nchi nyingi zinatumia credit system. Mtu mwenye Bachelor anaweza kuchukua Masters kwa credit 30 (masomo 10). Na mtu wa Advance diploma credit 36 (masomo 12). Hivyo hakuna tofauti yoyote hile.

Tukirudi kwenye mada. Vyuo vinavyotoa advance diploma ni lazima vifanye transformations za program zao na kutoa Bachelor hili kuwafanya watanzania wawe competitive katika masuala ya kazi na masomo.

Transformation inayofanyika Mzumbe ni ya kuungwa mkono na mtanzania yoyote. Na vitendo vilivyofanywa wa waalimu hawa vinarudisha maendeleo ya nchi na vinaweza kufanyika mahali popote. Hivyo ni lazima transparency iwepo. Hivyo lawama zisiwepo katika kwa Taasisi yenyewe bali kwa individuals wanaotaka kujinufaisha bila kuwa na shahada zinazotakiwa.
 

Watu wanafoji vyeti Tanzania kwa sababu HAKUNA THE RULE OF LAW... Kama kweli tungekuwa na utawala wa sheria wenye kuheshimika then watu wasingethubutu kufanya vitu hivi.

At one time, Rais alimteua waziri wa sheria ambaye alikua ana hiyo fake degree. Kungekuwa na parliamentary scrutiny kama iliyopo US kwa watu wanaoshika nyadhifa kubwa then majamboz kama haya ya kufoji vyeti yangeweza gundulika mumo kamatini, kama tu wajumbe wa hiyo kamati ya ku-scrutinize wateuliwa wangekuwa wawazi na wakweli na kama hiyo kamati ingejumuisha wajumbe kutoka katika vyama vyote vya siasa na pia sisi akina yakhe wa mitaani (lay person).
 

Naongezea: Dr. D. Kamala; Dr. Z. Gama; (Msc) Lukuvi, (MA) Lyatonga Mrema n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…