I stand to be corrected. Taasisi tangulizi ya TCU, yaani HEAC -High Education Accredation Council, ilikwishapiga chini chuo hiki kisiwe chuo kikuu kutokana na mapungufu mengi ikiwemo academic staff chovu isiyokidhi mahitaji ya kitaaluma na mitaala isiyokubalika kitaaluma katika hadhi ya chuo kikuu. Zengwe likapikwa na chuo kikaanzishwa kupitia Act of the Parliament (siasa) badala ya mchakato wa kawaida wa tathmini (taaluma). Matokeo yake ndiyo hayo kuwa copying and pasting ya thesis zimekithiri chuoni hapo. Wanafunzi wake wamekuwa less challenging academically na hata socially. Hata masuala yanayohusu maslahi yao wenyewe wanafunzi wanashindwa kuhoji. Chuo kipo kama kimemwagiwa maji. Kimelowa. Chukulia sakata la vyuo vikuu hivi majuzi vilivyoelekea vyuo karibu vyote vya serikali kufungwa, umesikia nini kutoka MU? Kimyaaaaaa. kisingizio eti wanafunzi wana tabia nzuri!!!!. But it could be they are incapacitated to analyze and raise their demands at the right time of need. Unapokuwa na academic staff ya online PhDs (or masters acquired based on advanced diplomas!!!) unategemea output ya aina gani kwa wanafunzi![/QUOTE]
Mzumbe! Hii aibu, ila ninajiuliza mambo yafuatayo.
1. hivi mgomo ni standard ya kufanya watu wajione wao wanamapinduzi, ambao hawagomi ni mazezeta? na kuwa watu wanaoenda vyuo vya UDSM na vingine na kugoma wametoka shule tofauti na wale wanaokwenda MU? hata hilo ninalipinga maana 1st year akiwa na miezi miwili hana tofauti na yule 1st year wa miezi miwili MU. ninakumbusha kuwa qualifications hazina tofauti mpaka sasa hivi kuingia vyuo vyote hivi.
2. hivi kama syllabi hazina tofauti, mfano sheria kwa vyuo vyote, unadhani mwaka huu UDSM watasema wamesoma kisawasawa na hii fukuza fukuza kulinganisha na MU kitivo hicho hicho? maana sasa hivi UDSM habari nilizonazo kutoka kwa Lecturers wenzangu ni kuwa wametoka nyumbani walipokuwa baada ya migomo, sasa hivi wanafanya test baadaye 1st semieter exam, na kufunga huku wengine ndio wanafanya registration. migomo hii haina msaada wowote kwa maendeleo ya inchi na kwa mtu mwingine. ila vijana wa MU wako darasani.
3. migomo mara nyingi huwa inaanzishwa na watu wasiokuwa na chakufanya"the idol mind is the workshop of Devil" wangekuwa na la kufanya wasingekuwa na migomo,
4 niambie chuo yaani UDSM kina watu zaidi ya 16 elfu, ni lini kwenye maandamano na migomo ukaona angalau watu 4000. hamna. ni vitisho tu na viboko na kejeri zinawafanya watu wabaki nyumbani kwa kuogopa kudharirishwa na wanafunzi wachache. au kama waligoma kutolipa, mbona walipotakiwa kulipia na kujiregister kama kweli mgomo haukuwa upepo fuata bendera ni wanafunzi 2000tu hawakujaa formu na wengine waliapologize. je unaweza kuita huo mgomo? la hasha! hata hao 2000tayari wamelipa tayari na sasa wanarudi chuoni.
5. can we say UDSM students walikuwa na upeo wa juu kuhusu madhara, matokeo, na hatima ya mgomo kuliko wale wa MU.
6. VC UDSM; Mkandala aliwahi toa sababu za migomo pale UDSM kuwa ni pamoja na poor management na ndio maana MU management yao inaepuka migomo kwa utaratibu mzuri waliojiwekea na hivyo kuahidi kufuata mfumo huo huo.
7> tuwe waangalifu na hoja zetu vinginevyo zinatia wasiwasi wa fikra zetu. Ila Mzumbe kwa hili ni aibu sana.
Mkuu Mushobozi, karibu tena jamvini na pole kwa shughuli nzito ya kisomo uliyonayo.
NAPENDA SANA UNAVYOITETEA MU, that shows a passion you have for your alma mater.
Hivi Mushobozi tuwe wakweli..hivi kweli kwa Tanzania yetu..ukipata admission ya MU na UDSM...where are you likely to go? (ceteris peribus). Ukweli ni kwamba MU is also a good University, lakini is not all that glamorous as you would want us to believe. Chukulia publications za walimu wa Muzumbe na UD? can you even compare? Wewe umeshasema ni lecturer...unajua kabisa tunapima ubora wa vyuo kwa kuangalia input za walimu..I have ample example..walimu wa MU bado kabisa...ni wachache kama wapo wame publish kwenye international journals zenye academic credibility) ( I stand to be collected). This however does not imply kwamba hawana strength maeneo mengine. Mfano MU ni wazuri katika management (whatever that means), lakini ukweli unabaki pale pale, na madudu ya UD akina Mkandala (By the way Mkandala ana PhD ya Berkeley contrast na WARIOBA ana PhD ya Pacific Western University) Hapa tofauti ni kubwa hata kama Mkandala is not living to the expectations za wengi. Ukichukulia hata publications za Mkandala..WARIOBA au hata Kuzilwa...is no where! Please...Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Au mwanafunzi aliyefundishwa Constitutional Law na Shivji pale UD...can you ever compare him na mtu aliyefundishwa somo hilo hilo MU na mtu kama Binamungu? (hata kama jamaa ni kiazi..lakini uwezekano wa kuwa na uelewa mpana ni mkubwa)
MU hawawezi kushindana na UD..bado sana. Ila haina maana kwamba hawawezi kufikia standards za UD....wanaweza kufika na wakasurpass. Cha kufanya:
1. Waanze kuajiri walimu walioenda shule "ndefu" ukiangalia majorities wana masters..ni wachache wenye PhD. na wengi ni hizo hizo za kuunga unga..Tofauti na fani nyingi..academics lazima mtu awe kichwa hasa..na siyo hizi shule za kuunga unga...
2. Waanze kutafuta academic exchange na vyuo vikubwa vikubwa huko duniani (and you can also help kama uko nje ;-) wafanye exchange..kusudi wajulikane. Ukienda huko nje wengi wanajua University of Dar Es Salaam. Ni kitu ambacho inabidi wakifanyie kazi.
3. Wawatake walimu wao kufanya publications kwenye "referred journals" internationally.
4. wawa-encourage waalimu wao kuomba admission kwenye vyuo makini. Maana walimu ni kioo...kama ulisoma Pacific western University..usitegemee mwanafunzi wako unayemfundisha ataomba shule Yale au Cambridge (just an example). Ni vyema walimu wakasoma shule makini..siyo hizi shortcut, za ilmradi kuwa na PhD.
5. MU wajue kabisa wana weakness kuattract the best and the brightest. Waweke scheme ya kuattract vijana wenye exposure na shule nzuri. Wasiwe conservative na GPA factor kama ya UD, ofcourse GPA ni kigezo safi..lakini waangalie mtu kaaccomplish kitu gani ndo wampe ajira.
6. Wafanye collaboration na UD..they cant dispense UD. Wajifunze kula na adui yao..and in the process they can learn alot. Infact sasa Iam happy naona wameanza kuwa creative kuwa na course mbali mbali ambazo hata UD hawana. They should concretize this by hiring smart dons.
7. UD is still the best University in our country (whatever that means). Ila improvement is always needed. Na haina maana kwamba vyuo vingine haviwezi kuwa bora kuliko UD..only right strategy.
8. By the way hata internationals wanapita humu......hivi unafikiri watu wakiona kashfa kama hizi..VC wa chuo anatuhumiwa kupata "diploma mill" unafikiri watu wata bother hata kuomba exchange ya semister? wanajua kabisa hapa hakuna kipya...na I can assure you hawa watoto wanaokuja mfano kama Africa kwenye exchange wanakuwa wameshafanya thorough research kuhusu hivi vyuo. Kuliko wewe na mimi tunavyofikiria. Credibility ni muhimu sana. Hata University of Dodoma....hii kashfa ya wakenya itawasumbua sana...maana watu wanakuwa na walakini tayari. So MU bado..pull up your sleeve!
Hivi unafikiri Harvard wanafundisha nini? Au Oxford wanafundisha nini? hakuna kitu extra ordinary, kuna vyuo wanafundisha na wanatoa elimu nzuri sana perhaps kuliko wao....lakini ile reputation yao iko solid, kiasi kwamba by mere having that name on your certificate..will make a difference and certainly it will pull your applications ontop of the heap!