Mzumbe University wanawezaje fundisha wanafunzi elfu 3 wa degree ya sheria kwa mwaka mmoja?

MU? Hamna kitu pale. Na kwa sababu ya uduni wa elimu inayotolewa pale, wahitimu ni mbumbumbu wa kutupwa, wakiajiriwa Wasumbufu Kwelikweli kuficha udhaifu wao. Ni sawa na wahitimu wa OUT.
Ubora wa elimu huenda sambamba na idadi ya wanafunzi ktk darasa. Darasa linakuwa na wanafunzi 3,000?!
 
Mleta thread ana point, ila watanzania hawawezi muelewa. Si kwa kozi hii ya Mzumbe tu, ni vyuo vyote na kozi karibia zote. Unaweza linganisha na vyuo vikongwe duniani kwa nyanja husika. Nadhani hii ndio huleta aina ya graduates ambao tumehitimu kwenye vyuo hivi vyetu.

Hii issue inafanana sana na uzazi wa mpango.
 
Ubora hapo itakuwa hakuna.
 
Niongeze Tu hapo!

Walimu wasahihishe homework kila siku, kama shule, wakague miandiko n.k
Watoe test za wiki na kusahihisha, test za mashindano ya kata, wilaya mpaka kanda!

Haaahaaahaaa!
 
Nakumbuka wakati vyuo vinaongeza udahili wakati wa mkapa mwishoni na JK mwanzoni kuna hoja zilikuwa zinatolewa na vyuo husika kukinzana na matakwa ya wanasiasa waliokuwa wanataka udahili uongezeke maradufu. Hoja za uwiano wa wanafunzi na wahadhiri na miundombinu wezeshi ilikuwa ni hoja kuu toka kwa DVCs.
Hivyo usiseme uwiano huo na miundombinu haina mashiko.
Unajua mziki wa kufunza na kusimamia research (proposal na dissertation) kwa mwanafunzi mmoja? Saa uwe na wahadhiri 30 na wanafunzi elfu moja, mwanafunzi atafunzwa vyema kweli??
Binafsi ninakuwa na mashaka.
 
Upo kizamani zaidi. Miundombinu ya kisasa, elimu kiganjani, hivi upo dunia ipi wewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…