Mzungu mwenye moyo wa kibongo

Mwadime

New Member
Joined
Oct 5, 2021
Posts
4
Reaction score
5
ndugu zangu,

Kwanza nijitambulishe kwa kuthibitisha mimi ndiye mzungu wa asili ya Kimarekani. Jina langu ni Riley (kifupi 'Rai') au pia watu wa kabila Taita huniita Mwadime - uchague lile unalolipendelea kuniita.

Kabla ya janga la UVIKO 19 niliwahi kuishi Afrika Mashariki haswa Tz takriban miaka miwili. Kusema ukweli nazipenda sana utamaduni za eneo hilo, lugha ya kiswahili, na mtindo wenu wa maisha unaonivutia hadi leo. Siku hizi niko njiani mwa kupata shahada yangu ya pili (uzamili) hapa USA lakini najua ni lazima nirudi kwenu punde nikiwa na nafasi.

Nikisubiria nafasi hiyo nimekuwa najipanga mambo ya baadaye ili niwe tayari kuhamia Tz. Suala linalonisumbua zaidi ni lile la mauzaji ya ardhi ikiwa mnunuzi ni mgeni kama mm. Nataka ardhi ya kujenga nyumba tu, lakini cjui kama nitakatarajiwa na mamlaka husika kuendesha biashara huko kwenye ardhi.

Naomba msaada wa mtaalamu kunielezea kidogo jinsi ya wageni kununua ardhi na nini vitahitajika.

Ahsanteni jamaani
 

Nunua ardhi Marekani na ubaki huko huko. Wamarekani wazuri tu wakitaka kitu kwako ila ni manyang’au, wabaguzi, walafi na wabinafsi sana.
 
We maliza masomo halafu njoo bongo.utapata ardhi.tunajua huwezi hamisha ardhi,itaendelea kuwa ya bongo.hapa kwetu kuna wageni kibao wengine hawajui hata neno moja la kiswahili wana miliki mieneo mikubwa ya ardhi
 
Unamfahamu sabaya na Don nalimison? Hao ndio wanahusika na kuuza ardhi kwa wageni.
 
Mzungu katika pitapita zako utakuwa ulifika Tanga!

Mzungu moyo wako wa kibongo vipi roho yako nayo ni ya korosho?
 

Wewe unajuaje nipo bongo? Mpaka nimesema hayo unauhakika gani kwamba sijaishi Marekani?

Nakuambia sasa kama mtu ambaye nina uzoefu nao, hawa siyo watu.
 

Ungejua mzungu anavyokuzungumzia wakati haupo usingesema huu upuuzi. Mzungu anatudharau sana hususani wa Marekani, wewe washobokee tu ila mimi toka utotoni nimecheza nao, tena wa kanisani, nikaishi nao, nikaenda na kwao.

Wasikie tu
 
Parabora with new ID

Jf raha sana wakuu nawakumbusha msishangae badae mkiambiwa Mwadime anapatikana kilima nyege daresalam
 
Nunua ardhi Marekani na ubaki huko huko. Wamarekani wazuri tu wakitaka kitu kwako ila ni manyang’au, wabaguzi, walafi na wabinafsi sana.
Nakuonea huruma ndugu kwani bayana una mtazamo finyu sana. Kubaguliwa ni kitu kibaya sana kwako na nimesikitishwa kusikia hiyo. lkn usiseme wazungu wote wawe manyang'au, bora ukague tabia na vitendo ya kila mtu mwenyewe. Nilikuwa ninauliza msaada tu.
 

Sina time kabisa na Mmarekani, manyang’au sana ila ni wanafiki kama CCM tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…