Wala sii kweli..Ramadhani watu hupotea kabisa appetite hasa huku majuu ndio kabisaaaa!Hebu acha hizo Bob. Wewe mwezi mzima ulikuwa unafuturu na ulikuwa inashindilia kisawasawa. Na hiyo ilikuwa mwezi tu. Kwa wenzako hiyo ni daily occurence.
Tanzania pamoja na njaa watu wanafukanya kishenzi yaani portion ya msosi wa huyo Companero tunayemwona hapo juu pamoja na wembamba wake ni chakula chako kwa siku mbili...Bongo kuna chakula wala usithubutu kusema na mkulima hana shida hiyo..Umaskini wa Mtanzania ni fedha! watu wanakonda kutokana na fikra za fedha, maradhi ya wazungu.. tunarudi palepale Ulimbukeni..maskini wote Tanzania vijijini wanafuga kuku, mbuzi na shamba la mahindi, maharage lakini watalala njaa kama Mmasai mwenye ng'ombe 1,000 lakini mtazame kwenye picha!
Njaa ipo mijini na huko kila siku watu wako kazini ktk mission town wenyewe huziita. Ni njama ambazo huwezi kuzifanya ukiwa na shibe!