Mkurugenzi mtendaji wa benki ya maendeleo
Aidha kutokana na mzunguko wa fedha kuwa mdogo umesababisha biashara nyingi kudorora, na hivyo baadhi ya wakopaji kwenye mabenki kushindwa kurudisha mikopo, na hivyo kuongeza idadi ya mikopo chefuchefu kwenye mabenki.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa benki ya maendeleo, wakati anaongea na vyombo vya habari kuelezea kampeni waliyoanzisha ya maendeleo benki pamoja na wewe ambayo lengo lake kubwa ni kuendelea kujenga hamasa kwa watanzania kujiwekea akiba.
Bwana Mwangalaba amesema benki yake inaamini kuwa kadri siku zinavyokwenda mzunguko wa besa utarudi kama kawaida, kufuatia watanzania walio wengi kuanza kuelewa serikali ya awamu ya tano inataka nini, hasa kwenye masuala ya ulipaji kodi stahiki.
Amesema toka benki hiyo ianzishwe miaka minne iliyopita hadi sasa tayari wameshatoa mikopo yenye thamani ya sh billion 26, mingi ya mikopo hiyo ikiwa imeelekezwa kwenye sekta ya kilimo na elimu.
Chanzo: Channel Ten