Mzunguko mdogo wa fedha changamoto taasisi za kifedha; biashara zimedorora, mikopo hairudishwi

Mzunguko mdogo wa fedha changamoto taasisi za kifedha; biashara zimedorora, mikopo hairudishwi

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
fedha.jpg

Mkurugenzi mtendaji wa benki ya maendeleo
Mzunguko mdogo wa fedha uliopo nchini kwa sasa unaendelea kuzipa Taaasisi za kifedha nchini changamoto ya idadi ndogo ya watu wanaoweka amana kwenye mabenki yao, na hivyo mabenki kujikuta uwezo wake wa kutoa mikopo ukipungua.

Aidha kutokana na mzunguko wa fedha kuwa mdogo umesababisha biashara nyingi kudorora, na hivyo baadhi ya wakopaji kwenye mabenki kushindwa kurudisha mikopo, na hivyo kuongeza idadi ya mikopo chefuchefu kwenye mabenki.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa benki ya maendeleo, wakati anaongea na vyombo vya habari kuelezea kampeni waliyoanzisha ya maendeleo benki pamoja na wewe ambayo lengo lake kubwa ni kuendelea kujenga hamasa kwa watanzania kujiwekea akiba.

Bwana Mwangalaba amesema benki yake inaamini kuwa kadri siku zinavyokwenda mzunguko wa besa utarudi kama kawaida, kufuatia watanzania walio wengi kuanza kuelewa serikali ya awamu ya tano inataka nini, hasa kwenye masuala ya ulipaji kodi stahiki.

Amesema toka benki hiyo ianzishwe miaka minne iliyopita hadi sasa tayari wameshatoa mikopo yenye thamani ya sh billion 26, mingi ya mikopo hiyo ikiwa imeelekezwa kwenye sekta ya kilimo na elimu.

Chanzo: Channel Ten
 
Magufuli kafanya mengi sana. Hapa kazi tu 😵😵😵
 
Tunaandamana lini kumpongeza mheshimiwa raisi?
 
Nashusha pumzi kuuubwa maana nikisikia kitu kinachoitwa mkopo naona maruweruwe
 
Huyo ataitwa mchochezi kwa kudanganya umma kuwa uchumi umedorora.
 
Kwani serikali imechukua mitaji ya mabenki? Tatizo ni kwamba benki nyingi ziliconcetrate kufanya kazi na hela za serikali zikasahau kubuni mbinu za kuongeza wateja na packages za kibiashara kwa wateja wao. Matokeo yake serikali imeuondoa fedha yake kwenye mabenki binafsi wanaanza kulalia tu. Wawe wabunifu wawajali wateja wao siyo kuilaumu serikali hata siku moja serikali haijawahi kulazimishwa kufanya biashara na benki hasa hizi benki za binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom