Huhisi mzunguko huu kwa sababu kila kitu kwenye uso wa dunia, pamoja na atmosphere, vinazunguka kwa mwendo huu.
Chukulia mfano wa sisimizi aliye katika gari linaloenda kasi. Sisimizi anakuwa na "kinetic energy" ya gari, na kama gari linaenda 90 km/hr, madirisha yamefungwa, hata hewa iliyo katika gari inakwenda kwa speed hiyo na sisimizi anakuwa hajui kwamba gari lina mwendo
Sasa wewe na dunia unakuwa mdogo mara nyingi sana zaidi ya sisimizi alivyo ndogo kwa gari.
Ndege haijatoka duniani bado, ipo katika atmosphere inayozunguka na mwendo wa dunia. Mfano mzuri wa kuona dunia inavyozunguka ni kwenda kwenye satellite zilizotoka nje ya atmpsphere ya dunia na zinazoweza kuiona dunia kwa mbali. Mfano ni "International Space Station"
Swali lina assume ndege imetoka nje ya dunia. Tumeona hapo juu kwamba hewa ya dunia ni sehemu ya dunia na ndege haitoki nje ya dunia.
Again, ndege yenyewe ipo katika dunia na inasukumwa na speed ya dunia. Ni sawa na wewe ukae nyuma kwenye pickup, halafu pickup iwe inaenda kasi, halafu uchukue kitenesi na kukirusha juu kidogo halafu ujaribu kukidaka. Unaweza kufikiri kwamba kitenesi kitadondoka nje, lakini kama hakuna upepo na hujakirusha juu sana utaweza kukidaka kama mtu ambaye kasimama, kwa sababu wewe, gari na kitenesi wote mna kinetic energy.
Ndege haitoki nje ya dunia, hivyo ni sehemu ya vyote vinavyokuwa moved na dunia vilivyo ndani ya dunia.
Nimejibu kutoka kichwani tu sijaangalia reference book kama nimekosea tujadili.