Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 652
- 1,058
Ndugu yangu aliyeshiriki vikao vya Chama changu Dodoma akitokea Shinyanga ametamba kwa majidai ya KiSukuma kuwa CCM walifanya kweli Dodoma. Walianza na kuwaita wafanyabisahara wote wa Hoteli na Loji wakaamrisha kuwa kuanzia Tarehe 10 hadi 12 Julai vyumba vyote vya Hoteli na Loji zao wasipokee watu. Wakaamrishwa watakaokiuka wasije kulaumu huko baadaye.
Na kweli ilipofika siku hiyo mtu hata kama ulikuwa unakusudia kuwepo Hoteli au Loji husika kwa siku hizo na hata km ulikuwa umelipia walikuwa wanakurudishia njuru zako na unaambiwa utajijua kwani wao hawataki kukwaruzana na Serikali. Baadhi ya Hoteli na Loji wamiliki wake waliombwa wasaidie Chama bure na wakakubali kwa shingo upande.
Hata hivyo Hoteli na Loji hizo zilitunza nafasi hizo kwa wanaCCM lakini baadhi ya hizo waliofanyiwa booking hawakutokea na kusababisha hasara kwa wenye Hoteli na Loji hizo kwani CCM pia hawakuwa tayari kulipia vyumba ambavyo havikulaliwa. Baadhi ya Hoteli na Loji wale waliofanyiwa booking wakisaidiana na wahudumu wa Hoteli au Loji husika waliamua kuuza vyumba vyao na kuhamia kwenye loji au gesti za bei ya chini ili wanufaike zaidi na wengine waliamua kwenda kwa ndugu.
Hicho kilifanyika na kwa mabasi pia. Wamiliki wa baadhi ya mabasi walikataa kubeba abiria wao wa kila siku kwa kisingizio kuwa mabasi hayo yalifanyiwa booking na CCM yangu. Asilimia 60 ya mabasi ambayo huja na kutoka Dodoma yaliwakataa abiria wao wa kila siku na kusababisha taharuki kubwa kwani ilibidi watu kubadili tarehe za kusafiri bila kupenda.
Kwa kweli sio kwamba watu wamiliki wa Hoteli na Loji walipenda CCM walivyofanya isipokuwa wamefanya kwa mashinikizo makubwa sana na hofu papo!