KRISTIAN P
JF-Expert Member
- Feb 16, 2013
- 352
- 57
Habari wadau, nimekuwa na idea kichwani kwangu muda sana ila nashindwa sijui nianzie wapi. Nimepata bahati ya kusafiri nje ya nchi kila mwaka mara mmoja na kaa uku miezi sita (Denmark), nikapata wazo la kuwa na nunua vitu used na kutuma Bongo. Kutokana na mtaji wangu ni mdogo nimeona nianze na vitu vidogo vidogo kama simu, computer,Playstation; flat screen na vingine.. ila nataka niwe natuma kupitia posta, nimeshafungua p.o.box kwa ajili ya kutuma mizigo. Tatizo linakuja pale posta wana ushuru mkubwa sana. Je akuna connection yoyote naweza pata au njia yoyote kutokana ndio na anza sina huwezo wa kutuma kontena. Ata mbuyu ulianza kama mchicha. Natanguliza shukurani.