Na tuifanye nchi yetu kuwa ya kijani tupande miti kwenye makazi yetu

Kyambamasimbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
762
Reaction score
1,597
Kuna baadhi ya jamii au Kaya huamini kuwa miti Ni Kama adui wa usalama wao lakini kumbe miti Ina faida nyingi kuliko hasara. Jamani tumeona mabadiliko ya Hali ya hewa na tabia ya nchi. Jamani tubadilike tupande miti angalau mti mmoja utakuwa umechangia kutunza Mazingira yetu.
 
Natamani ingepitishwa kabisa Sheria kila Kaya angalao iwe na miti angalao mitano, ambayo itakuwa inagawiwa bure na Serikali.

Hii ingesaidia sana kuboresha hali ya hewa na kuweka kivuli katika nyumba, vilevile miti mingine ingesaidia kwenye lishe, hasa miti ya matunda.
 
Natamani ingepitishwa kabisa Sheria kila Kaya angalao iwe na miti angalao mitano, ambayo itakuwa inagawiwa bure na serikali.

Hii ingesaidia sana kuboresha hali ya hewa na kuweka kivuli katika nyumba, vilevile miti mingine ingesaidia kwenye lishe, hasa miti ya matunda.
Miti sio gharama, Kuna Miche inauzwa kuanzia mia mbili 200/= tu
 
Kuna baadhi ya jamii au Kaya huamini kuwa miti Ni Kama adui wa usalama wao lakini kumbe miti Ina faida nyingi kuliko hasara. Jamani tumeona mabadiliko ya Hali ya hewa na tabia ya nchi. Jamani tubadilike tupande miti angalau mti mmoja utakuwa umechangia kutunza Mazingira yetu.
Serikali na taaisisi za matapeli Wa MAZINGIRA wanampango Gani?
Leo hii mche mmoja Wa MTU ni Sh.3000 /- mpaka Sh.5000/- Miche mia Moja ni Sh. 300,000/- .Pesa mfukoni hakuna, Bei za vyakula juu, mafuta juu. Kama MTU SIO fisadi utaupanda Huo mti kweli ? Na ukiupanda utaumwagilia na Maji ya mgao au ya kununua dumu sh.1000/-?

Zamani Kabla Shetani hajaimarisha ukaribu Wake na NGOs na taasisi za MAZINGIRA palikua na miradi mingi ya kuotesha Miche AMBAYO ilikuwa inatolewa Bure Kwa wananchi. Na ilikua ni Lazima Kila mwanafunzi apande mche shuleni na Nyumbani. Kwa Sasa Zile pesa wanakwenda kuwalipia wototo wao pesa za kwenda kupanda midoli ya farasi Kule Beach. Na kumwagilia mioyo Yao Kwa pombe na uasherati. Wanasema watu wasimwagilie mazao Yao Kwa kumtumia pampu Lakini hawaoni kuwa patakua na uhaba mkubwa Wa chakula kutokana na ukweli kwamba kilimo cha umwagiliaji kimewasaidia sana wanyonge kujikwamua kimaisha na kuongeza chakula kwenye maghala. Maziwa yamejaa Maji Lakini njaa ,ukosefu Wa huduma ya Maji na Ukame unazidi na mvua inapotea mwisho Wa Siku watawaachia Watoto wao ukame na Nchi yenye Njaa na ukame mkubwa
wakwao wakiishi Maeneo maalumu yasiyo na shida.

Miti ni muhimu lakini Maendeleo yasiposimamiwa VIZURI nchi itageuka jangwa la Kalahari.
 
Miti sio gharama, Kuna Miche inauzwa kuanzia mia mbili 200/= tu
Acha kupotosha watu hakuna MTU anayeweza kuotesha Miche halafu Auze Kwa sh.200. Hata kimfuko cha kupandia hakitoshi achilia Mbali mbolea na muda wake na ulinzi muda wote. Miche Ili iwe rahisi ni Lazima pawe na NGOs au Serikali igharamikie.
Vinginevyo hakuna mche chini ya Sh. 2000/ na Miche ya matunda mpaka 5000/-
 
Upo wapi mkuu nikupeleke mkono kwa mkono, Mimi nipo Arusha-Arumeru huku nimenunua miti 15 @Tsh.200/=. Kabla ya ku jump to conclusion uliza kwanza mkuu..
 
Kuna nyumba zinanishangazaga sana....unakuta nyumba nzuri,eneo la kutosha ila hamna mti hata mmoja...huwa najiuliza hivi huyu mwenye nyumba anaakili gani?
Kabisa mkuu ajabu sana
 
Kuna nyumba zinanishangazaga sana....unakuta nyumba nzuri,eneo la kutosha ila hamna mti hata mmoja...huwa najiuliza hivi huyu mwenye nyumba anaakili gani?

FB_IMG_16659060553570353.jpg
FB_IMG_16658087755113046.jpg
FB_IMG_16656773691348857.jpg
FB_IMG_16655641650669451.jpg
FB_IMG_16655893835182514.jpg
 
Hii ni kutoka kwa Wakala wa Misitu TFS, inawezekana mtu kununua miti kadhaa na kupanda eneo la nyumbani kwako kama linatosha. Kwa Mfano maeneo ya Dar Kila nyumba ikiwa na mti mmoja sio mbaya.
Lakini pia Serikali iweke mpango wa Taifa wa upandaji miti ili kunusuru nchi na ukame.
Screenshot_20221113-072554.jpg
 
Nzuri saana mkuuu watu wahamasishwe
Hii ni kutoka kwa Wakala wa Misitu TFS, inawezekana mtu kununua miti kadhaa na kupanda eneo la nyumbani kwako kama linatosha. Kwa Mfano maeneo ya Dar Kila nyumba ikiwa na mti mmoja sio mbaya.
Lakini pia Serikali iweke mpango wa Taifa wa upandaji miti ili kunusuru nchi na ukame.View attachment 2415035
 
Nzuri saana mkuuu watu wahamasishwe
Kabisa viundwe vikundi vidogo vidogo, viwezeshwe mbegu na TFS baadae Taasisi za Serikali na binafsi zinunue Miche kwa bei nafuu kutoka kwenye vikundi hivi hii itaboresha mazingira pia itatoa ajira kwa vijana
 
Kuna nyumba zinanishangazaga sana....unakuta nyumba nzuri,eneo la kutosha ila hamna mti hata mmoja...huwa najiuliza hivi huyu mwenye nyumba anaakili gani?
Kila sehemu imesilibwa na kuwa kama jangwa.
 
naona tunaingia kwenye mtego wa viongozi wapumbavu walioshindwa kuplan vizuri na Taifa likawa na maji kila kona baadala yake wanasingizia ukame uliosababishwa na ukataji wamiti.

Uarabuni hakuna miti ila akili imefanya kazi kupata maji na kuwa na constant supply.
Ulaya na America walishafyeka sana mapoli kujenga miji na maviwanda lakini husikii shida ya maji.

Maana ya kuwa kiongozi nikuonyesha njia na ufumbuzi wa matatizo kwa watu wako na sio kulalama na kulaumu watu wako kwenye kila tatizo wakati unapaswa kuset mifumo na watu waifuate na usimamizi wako kwa manufaa ya watu hao hao.

Leo hii Watanzania zaidi ya 60% wanatumia mkaa unaotokana na kukata miti, wakati tunaoption ya kupunguza makodi kwenye gas na kuifanya bei ya gas sawa au karibu na bei ya mkaa huku tukihahakisha wakazi woote wanaoishi kwenye miji na wilayani watumie gas.
Tuna option ya makaa ya mawe ni issue tu ya kufanya utaratibu yaweze kutumika domestically na watu kuachana na hizi wood charcoal.
 
Mawazo chanya kabisa happy kwenye matumizi ya gesi Ni sahihi sana
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Upo wapi mkuu nikupeleke mkono kwa mkono, Mimi nipo Arusha-Arumeru huku nimenunua miti 15 @Tsh.200/=. Kabla ya ku jump to conclusion uliza kwanza mkuu..
Arumeru wanapata wafadhili .
Bila wafadhili hakuna Mti Wa sh.200 Labda nyasi.
Yani MTU anunue mbegu ,aweke mbolea ,amwagilie Maji Kwa miezi halafu Auze mche sh. 200/( mia mbili)
 
Mkuu mimi sikubishii ipo hadi miti ya 10,000/= inategemea unataka mti wa aina gani? Kuhusu wafadhili Mimi nimenunua miti kwa mtu tu wa kijijini Hana hata mfadhili tena nimenunua sababu Sina muda wa kutafuta porini na kuamishia shambani unless ningeafuta mwenyewe. Hapa Kuna chama cha wakulima wa kahawa na hakina ufadhili wa Serikali wala mtu binafsi lakini wanauza mche mmoja wa kahawa 1,000. Pia kama unauhitaji wa kupanda miti kwako huwezi kukosa hiyo 2,000, kwani unapanda shamba la miti!?

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom