naona tunaingia kwenye mtego wa viongozi wapumbavu walioshindwa kuplan vizuri na Taifa likawa na maji kila kona baadala yake wanasingizia ukame uliosababishwa na ukataji wamiti.
Uarabuni hakuna miti ila akili imefanya kazi kupata maji na kuwa na constant supply.
Ulaya na America walishafyeka sana mapoli kujenga miji na maviwanda lakini husikii shida ya maji.
Maana ya kuwa kiongozi nikuonyesha njia na ufumbuzi wa matatizo kwa watu wako na sio kulalama na kulaumu watu wako kwenye kila tatizo wakati unapaswa kuset mifumo na watu waifuate na usimamizi wako kwa manufaa ya watu hao hao.
Leo hii Watanzania zaidi ya 60% wanatumia mkaa unaotokana na kukata miti, wakati tunaoption ya kupunguza makodi kwenye gas na kuifanya bei ya gas sawa au karibu na bei ya mkaa huku tukihahakisha wakazi woote wanaoishi kwenye miji na wilayani watumie gas.
Tuna option ya makaa ya mawe ni issue tu ya kufanya utaratibu yaweze kutumika domestically na watu kuachana na hizi wood charcoal.