Kyambamasimbi
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 762
- 1,597
Anawaza atafute pesa ashushe mjengo mwingine hayo mambo ya miti kawaachia nemcKuna nyumba zinanishangazaga sana....unakuta nyumba nzuri,eneo la kutosha ila hamna mti hata mmoja...huwa najiuliza hivi huyu mwenye nyumba anaakili gani?
Miti sio gharama, Kuna Miche inauzwa kuanzia mia mbili 200/= tuNatamani ingepitishwa kabisa Sheria kila Kaya angalao iwe na miti angalao mitano, ambayo itakuwa inagawiwa bure na serikali.
Hii ingesaidia sana kuboresha hali ya hewa na kuweka kivuli katika nyumba, vilevile miti mingine ingesaidia kwenye lishe, hasa miti ya matunda.
Serikali na taaisisi za matapeli Wa MAZINGIRA wanampango Gani?Kuna baadhi ya jamii au Kaya huamini kuwa miti Ni Kama adui wa usalama wao lakini kumbe miti Ina faida nyingi kuliko hasara. Jamani tumeona mabadiliko ya Hali ya hewa na tabia ya nchi. Jamani tubadilike tupande miti angalau mti mmoja utakuwa umechangia kutunza Mazingira yetu.
Acha kupotosha watu hakuna MTU anayeweza kuotesha Miche halafu Auze Kwa sh.200. Hata kimfuko cha kupandia hakitoshi achilia Mbali mbolea na muda wake na ulinzi muda wote. Miche Ili iwe rahisi ni Lazima pawe na NGOs au Serikali igharamikie.Miti sio gharama, Kuna Miche inauzwa kuanzia mia mbili 200/= tu
Upo wapi mkuu nikupeleke mkono kwa mkono, Mimi nipo Arusha-Arumeru huku nimenunua miti 15 @Tsh.200/=. Kabla ya ku jump to conclusion uliza kwanza mkuu..Acha kupotosha watu hakuna MTU anayeweza kuotesha Miche halafu Auze Kwa sh.200. Hata kimfuko cha kupandia hakitoshi achilia Mbali mbolea na muda wake na ulinzi muda wote. Miche Ili iwe rahisi ni Lazima pawe na NGOs au Serikali igharamikie.
Vinginevyo hakuna mche chini ya Sh. 2000/ na Miche ya matunda mpaka 5000/-
Kabisa mkuu ajabu sanaKuna nyumba zinanishangazaga sana....unakuta nyumba nzuri,eneo la kutosha ila hamna mti hata mmoja...huwa najiuliza hivi huyu mwenye nyumba anaakili gani?
Kuna nyumba zinanishangazaga sana....unakuta nyumba nzuri,eneo la kutosha ila hamna mti hata mmoja...huwa najiuliza hivi huyu mwenye nyumba anaakili gani?
Hii ni kutoka kwa Wakala wa Misitu TFS, inawezekana mtu kununua miti kadhaa na kupanda eneo la nyumbani kwako kama linatosha. Kwa Mfano maeneo ya Dar Kila nyumba ikiwa na mti mmoja sio mbaya.
Lakini pia Serikali iweke mpango wa Taifa wa upandaji miti ili kunusuru nchi na ukame.View attachment 2415035
Kabisa viundwe vikundi vidogo vidogo, viwezeshwe mbegu na TFS baadae Taasisi za Serikali na binafsi zinunue Miche kwa bei nafuu kutoka kwenye vikundi hivi hii itaboresha mazingira pia itatoa ajira kwa vijanaNzuri saana mkuuu watu wahamasishwe
Kila sehemu imesilibwa na kuwa kama jangwa.Kuna nyumba zinanishangazaga sana....unakuta nyumba nzuri,eneo la kutosha ila hamna mti hata mmoja...huwa najiuliza hivi huyu mwenye nyumba anaakili gani?
Mawazo chanya kabisa happy kwenye matumizi ya gesi Ni sahihi sananaona tunaingia kwenye mtego wa viongozi wapumbavu walioshindwa kuplan vizuri na Taifa likawa na maji kila kona baadala yake wanasingizia ukame uliosababishwa na ukataji wamiti.
Uarabuni hakuna miti ila akili imefanya kazi kupata maji na kuwa na constant supply.
Ulaya na America walishafyeka sana mapoli kujenga miji na maviwanda lakini husikii shida ya maji.
Maana ya kuwa kiongozi nikuonyesha njia na ufumbuzi wa matatizo kwa watu wako na sio kulalama na kulaumu watu wako kwenye kila tatizo wakati unapaswa kuset mifumo na watu waifuate na usimamizi wako kwa manufaa ya watu hao hao.
Leo hii Watanzania zaidi ya 60% wanatumia mkaa unaotokana na kukata miti, wakati tunaoption ya kupunguza makodi kwenye gas na kuifanya bei ya gas sawa au karibu na bei ya mkaa huku tukihahakisha wakazi woote wanaoishi kwenye miji na wilayani watumie gas.
Tuna option ya makaa ya mawe ni issue tu ya kufanya utaratibu yaweze kutumika domestically na watu kuachana na hizi wood charcoal.
Sio maeneo yote mkuu kutokana na gharama za kuzalishia miche kuanzia kiriba, udongo na mbegu. Samahani mkuuMiti sio gharama, Kuna Miche inauzwa kuanzia mia mbili 200/= tu
Arumeru wanapata wafadhili .Upo wapi mkuu nikupeleke mkono kwa mkono, Mimi nipo Arusha-Arumeru huku nimenunua miti 15 @Tsh.200/=. Kabla ya ku jump to conclusion uliza kwanza mkuu..
Mkuu mimi sikubishii ipo hadi miti ya 10,000/= inategemea unataka mti wa aina gani? Kuhusu wafadhili Mimi nimenunua miti kwa mtu tu wa kijijini Hana hata mfadhili tena nimenunua sababu Sina muda wa kutafuta porini na kuamishia shambani unless ningeafuta mwenyewe. Hapa Kuna chama cha wakulima wa kahawa na hakina ufadhili wa Serikali wala mtu binafsi lakini wanauza mche mmoja wa kahawa 1,000. Pia kama unauhitaji wa kupanda miti kwako huwezi kukosa hiyo 2,000, kwani unapanda shamba la miti!?Arumeru wanapata wafadhili .
Bila wafadhili hakuna Mti Wa sh.200 Labda nyasi.
Yani MTU anunue mbegu ,aweke mbolea ,amwagilie Maji Kwa miezi halafu Auze mche sh. 200/( mia mbili)