Naachaje kuchepuka ?

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
3,134
Reaction score
3,584
Kama kichwa kinavyojieleza!
Mimi ni kijana nipo katikati ya miaka ya 30's na nina mke na watoto wawili.

Nikiri yakuwa mke wangu ni mzuri sana na mwema sana kwangu, mishahara yetu tunaiweka kwenye acc moja kwaajili ya maendeleo yetu na wanetu, haendi wala kufanya chochote bila kuniambia, kwa kifupi ni mwema sana kwangu!.

Na mimi pia kama baba ndani ya nyumba najitahidi kadri ya uwezo wangu kuwa mwema na uchafu wote ninaoufanya hajawahi hata kuhisi mimi ni msiri mno na ninaochepuka nao ninawaambia nina mke sitaki usimbufu home time!

Najitahidi sana nisitumie rasilimali tunazochuma pamoja kula na michepuko hivyo nafanya kila namna/manuva nipate extra money kwaajili ya michepuko out of our normal earnings!

Baada ya ndoa niliweza kukaa 3 years without to cheat but baada ya kukutana na ex wangu wa o level nikajikuta naanza uchafu ambao nilishaungama/kutubu.
Nikiri tu kabla ya ndoa nilikuwa kicheche nisiyepitwa na sauti mpya ila niliamini nikioa nitaacha.

Nikaoa nikajitahidi but now ndio kama nimechokoza yani nimekuwa kicheche kuliko ambao hawajaoa japo nafanya kwa siri sana hakuna anayeweza jua zaidi yangu na ninayemla mbaya zaidi ninaofanya nao kwa uzuri hawamfikii mke wangu hata robo.

Kinachoniuma sio rasilimali ninazozitumia, magonjwa wala mda ila naumia sana kuona nashindwaje kuacha uzinzi, naisaliti ndoa yangu na namsaliti mke wangu ambaye ninampenda sana!
Nikiri ninampenda sana ila namsaliti bila huruma.

Nakosea wapi wakuu!
Naomba ushauri utoke kwa waliooa na walioolewa tu!
Madogo kuweni myaone.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Unachokosea ni Kumsaliti mkeooo...!! Pia suala la kuacha uzinzi ni la mtu binafsi kuamua tuu... Ridhika na mkeooo maana hakuna aelikamilikaa...utatamani mwenye matako hajui kitu zaidi ya kuspend hela tu...
 
Rikaboy umeoa?
 
Halafu wanasema ukiwa mwema mume atatulia. Wapi bwana kama umeolewa na binamu yake shetani hata ungekuwa mdogo wake malaika Gabriel hakuna kitu unaweza kufanya
Kwani mke si anamwona huyu jamaa mwema?

Haya, mke naye anaonekana mwema kwa huyu jamaa.

Hapo unadhani mke naye katulia tu? Analijua mwenyewe...huenda yeye kakosa pa kuanzishia uzi anachepuka kumzidi huyu.
 
Unatudhalilidha wanaume, wenzako wanachepuka kama mwanamke haeleweki hvyo wanakuwa na stress na upweke, sasa wewe ndugu hauna sababu ya kuchepuka zaidi ya kuwa tu ni tabia binafs uliyojizoesha ya uzinz, sasa kama ulijiona mzinzi ni heri ungeoa mzinzi mwenzako kuliko kumdhalilisha mkeo

Unaweza kusema ni siri lakin iko sku atajua....

Ebu jiulize, yeye akichepuka utajiskiaje?
 
Kwani mke si anamwona huyu jamaa mwema?

Haya, mke naye anaonekana mwema kwa huyu jamaa.

Hapo unadhani mke naye katulia tu? Analijua mwenyewe...huenda yeye kakosa pa kuanzishia uzi anachepuka kumzidi huyu.
Nyie si mnasemaga wanawake hatuna uwezo wa kuwa na wanaume zaidi ya mmoja bila kukamatwa? ( teh hivi sahihi ni mwanaume zaidi ya mmoja au wanaume zaidi ya mmoja?)
 
Nyie si mnasemaga wanawake hatuna uwezo wa kuwa na wanaume zaidi ya mmoja bila kukamatwa? ( teh hivi sahihi ni mwanaume zaidi ya mmoja au wanaume zaidi ya mmoja?)
Mimi sijawahi kusema...

Ila huwa nasema mwanamke anaouwezo wa kulificha jambo usijue miaka nenda.

Maana nyie mkikaa mnawaza mambo elfu kwa wakati mmoja ila mie nikishakaa nawe nasahau nilikuwa wapi mchana hadi niulizwe.
 
Me mke wangu sioni sababu ya kumsaliti kabisa ndo maana nimetuliaa..tukigombana nafanya namna mpaka tupatanee..Tunda ananipa kila nikihitaji so sina mizukaa kabisa...
Niombee na mimi nitulie aisee natamani sana ila nashindwa
 
Hahaha ingekuwa hivyo ulivyosema msingekuwa na uwezo wa kuhendo wanawake saba kwa mpigo
Mimi sijawahi kusema...

Ila huwa nasema mwanamke anaouwezo wa kulificha jambo usijue miaka nenda.

Maana nyie mkikaa mnawaza mambo elfu kwa wakati mmoja ila mie nikishakaa nawe nasahau nilikuwa wapi mchana hadi niulizwe.
 
Mkuu njia uliyotumia awali kwa miaka 3 ukafanikiwa kutokuchepuka itumie hiyohiyo sawa, ila ukishindwa bado mshirikishe mkeo atakushauri ucjal maana ninyi ni mwili mmoja..
Sio kama nitakuwa ninampa taarifa ya upuuzi ninao ufanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…