Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
WanaJF: Tumeingia ngwe ya pili ya kampeni na sasa tunaona jinsi shujaa wetu, mkombozi wetu, Dr W. Slaa alivyoanza kutumia ile mitutu mingine katika mashambulizi yake kwa kikundi cha kifisadi kinachoongozwa na JK, RA,EL, Makamba na Kinana. Siwataji wengine ambao ni walamba ukoko tu.
Naambiwa mashambulizi haya ya sasa hivi –wizi wa sh 155 bilioni wa Meremeta na Sh 1.7 trilioni katika hela zilizotengwa kukabiliana na mtikisiko wa uchumi duniani – ni rashrasha tu (small arms fire).
Inatarajiwa ifikapo tarehe 20 mwezi huu mkombozi wetu huyo atakuwa anatumia mitutu yote (firing from all cylinders) tena kwa kutumia ile ya mizinga mikubwa (heavy artillery, howitzers etc) na hapo ndipo kikundi hicho cha wezi kitajua kuwa maharage si mboga, bali ni dawa ya tumbo tu!
Katika hiyo final straight, tunaomba wananchi tuungane pamoja tumpeleke Dr Slaa Ikulu. Tukifanya makosa tena miaka mitano ijayo tutakuwa tumekwisha – JK hawezi kutimiza ahadi zozte anazotoa kwa sababu akimaliza ile ngwe hatakuwa tena Ikulu na hivyo hakuna mtu atakaemuuliza.