Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Kwa kweli hilo ni jambo lingine la msingi kabisa ambalo linahitaji ufafanuzi wake kutoka kwa hawa wanaojiita wanathiolojia wa Mungu Mpya.

Na inabidi waje hapa waelezee.

Lakini kabla hiyo imani ya Mungu mpya kuletwa, historia inaonesha kuwa Mababu zetu (Waafrica Weusi) walikuwa na imani zao kabla hata hizo za Mungu mpya kuletwa.

Na imani hizo za kale za Mababu zetu, zimekuja kuitwa kuwa ni za kimizimu/kishetani.

Lakini ninachoshangaa ni kwamba hizo imani inaonekana zilikuwa zinawasaidia, yaani walikuwa wakiomba chochote kwenye mizimu yao walikuwa wanapata.

Lakini baada ya kuwasili kwa Imani za Mungu mpya (aliyeletwa na wakoloni) ikaonekana hiyo imani ya mababu zetu ilikuwa ni kichawi na ni haramu/chukizo kwa Mungu.

Sasa mimi nauliza, wale mababu zetu waliokufa kabla ya kuwasili kwa imani za Mungu mpya, hukumu yao siku ya kiama itakuwaje ?
Ulianzisha Uzi mzuri lkn ulikuwa hujaisoma vizuri biblia. Hilo ndo tatizo la atheist wengi.
 
Simlaumu mtu anayepinga imani kwa sababu Ni lazima apinge kutokana na utitiri wa imani mbalimbali zilizokwisha jitokeza.

Kutoka mwanzo wa mjadala huu Kuna hoja ambazo kimsingi mtu wa dini bila imani thabiti huenda akasalia kuwa mpagani.
Na hasa wale wale wakristo ambao hawajawahi kupata neema yakumuona Mungu. Nimejaribu kufikiri kwamba, Kama Mimi nimetetereka kwenye imani yangu hali yakuwa tayari nmeona neema na miujiza lukuki Tena ya wazi wazi. Inakuwaje kwa mtu ambae Ni mkristo na ambaye hajaona neema Kama Mimi?

Nimeenda mbali zaidi kwakuanza kupitia kumbukumbu za baadhi ya matukio yangu ambayo yalitokea ili kuona Kama kweli Ni Mungu alitenda au Ni wenge langu tu. Kuna tukio moja ambalo hadi leo hii nikilitafakari huwa nasema hapana haikuwa wenge Bali Ni Mungu kabisa.
Baada ya kuchukua uamuzi wa kumfuata yesu niliweza kuishi maisha ya utakatifu usio na doa. Jioni Kama saa tatu hivi, nilisoma Sana biblia na kutafakari kwakina Sana huku biblia nimeiweka kifuani nikiwa nimefumba macho, ghafla nikasikia watu wawili wakipiga stori pembeni yangu lakini kwakusikia sauti tu. Ilikuwa ktk hali yakupeleka taarifa kwa Mungu kutokana na hali ya usafi wa moyo wangu uliowastua watu wale wawili ambao baadae nilikuja kudhani walikuwa malaika. Baadae kidogo Mungu mwenyewe alifika hapo kati yetu na kuwaagiza wale malaika kuchukua dhabihu. Sikuwa nikijua maana ya neno dhabihu.
Basi wale malaika walianza kukata katikati ya kifua changu lkn kwa ndani, na maumivu yakukata nilikuwa nayasikia lkn sio makali, Ni mfano Kama wa mtu anayeshonwa wakati ganzi ikikaribia kuisha. Nilitulia tuli. Malaika akasema; dhaabihuuu! Baada ya hapo Mungu Kuna neno ambalo alitamka na sintoweza kuliandika hapa Kisha akaondoka.

Ndipo wale malaika wakabaki wakitafakari neno alilotamka Mungu. Na walikuwa wakiongea Kama washkaji tu. Mmoja akamwambia mwenzake kwamba; alilosema Mungu inawezekana kweli? Basi mwenzake akasema; yawezekana maana jicho la Mungu...! Baada ya hapo waliondoka. Nami nikainuka moja kwa moja hadi kwa mchungaji wangu kumweleza na kumuuliza dhabihu Ni Nini? Akanijibu pia alinieleza kuwa ninabahati Sana.

Chakushangaza maumivu kwenye kifua yalidumu takribani masaa 24 japo sio makali Sana lkn Hadi mwili wangu ulipungua kutokana na maumivu hayo.
Najaribu kujiuliza kutokana na utetezi wa watu ambao sio waamini kwamba huenda Mungu hayupo, na kwa miujiza mingi Sana nmeiona ambayo naweza sema labda Ni wenge langu tu, sawa! Lakini hii ya Mungu kushuka na kuchukua dhabihu na maumivu kubaki kifuani kwangu. Hapana kwakweli Mungu yupo tuacheni masihara.
Mimi eti leo nije niwaambie watu kuwa hakuna Mungu nitakuwa mnafikiri wakwanza kuwahi kutokea.
 
Hatari sana
 
Back
Top Bottom