Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri tuu! , Ila...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi,
Rais Magufuli ni rais wetu, japo rais halazimishwi kufuata ushauri wowote kutoka kwa yeyote, kwa mujibu wa ibara hii ya katiba yetu, " 37.-(1) Apart from complying with the provisions contained in this Constitution, and the laws of the United Republic in the performance of his duties and functions, the President shall be free and shall not be obliged to take advice given to him by any person, save where he is required by this Constitution or any other law to act in accordance with the advice given to him by any person or authority", lakini rais kama rais wetu, anapaswa kusikiliza ushauri wetu na sii lazima aufuate, hivyo sisi wana JF kazi yetu iwe ni kushauri tuu, na lazima atasikia tuu, au yeye mwenyewe, au kupitia sikio lake linalosikia kila kitu kutoka kila kona ila sii lazima afuate ili siku ya siku yakitokea ya kutokea, tuibuke na kutoa mrejesho kuwa kuhusu hili, tuliwahi kushauri hivi na hivi.

Kuna mtu alileta bandiko humu kutaka kuwafahamu washauri wa rais ni kina nani ila pía alitaka kujua hao washauri wanamshauri nini rais wetu ili kila anachosema na kila anachofanya tujiridhishe kuwa, alishauriwa.
Kuna haja ya kuwafahsmu wanaomshauri rais.
Tazama yanayoendelea bandarini
Tazama yanayoendelea katika hotuba zake.
Tazama yanayoendelea bungeni
Tazama yanyoendelea kuhamia Dodoma
na mengine mengi sn.
wananchi tunahaki kuwajua washauri wa raisi
Mkuu assadsyria3, kuna vitu kumhusu rais wetu ambayo ni vya public, sisi Watanzania tuna haki ya kuvijua, hivi ni vitu vinavyoitwa public affairs, na kuna vitu kumhusu rais wetu ambavyo ni vya kitendaji ambayo ni official, vinaweza kuwa confidential, secret or top secret ambavyo sisi raia wa kawaida, hatupaswi kuvijua zikiwemo kazi za operations za ile idara ya wale 'jamaa' iliyochini yake, lakini pia kuna vitu rais anavyovisema na kuvifanya ni personal or private ambavyo hatupaswi kuvijua kwa heshima ya kitu kinachoitwa "the right to privacy", ambayo rais kama raia mwingine yoyote wa JMT, anayo his right to privacy ambayo haipaswi kuingiliwa na mtu au taasisi yoyote.

Miongoni mwa vitu public kuhusu wasaidizi wake, public ni kuwajua tuu baadhi ya wasaidizi hao ni kinanani, lakini kujua wanamshauri nini au wamemshauri nini, haya sasa ni mambo ya kiofisi na ni confidential kati yake na wasaidizi wake, washauri wake na mambo yake binafsi ambayo hayatuhusu! . Hili la kutaka kujua mshauri gani wa rais amemshauri nini ni over and above public reach. Kitu ambacho sisi Watanzania tunataka kuona ni kuna rais wetu akisema the right things na akifanya the right things. Pale inapotokea rais anatoa matamshi ya kiajabu ajabu, au kufanya mambo ya kiajabu ajabu au mambo ambayo ni makosa ya wazi, then tunakuwa na haki ya kuhoji kama kwenye hili au lile, hivi rais wetu ameshauriwa vizuri?. Vitu vinavyoashiria au rais ameshauriwa vibaya, au umeshauriwa vizuri, ila hakufuata ushauri. Hivyo kuuliza kama rais ameshauri vizuri kwenye any specific issue, ni swali valid na sio mshauri gani amemshauri nini rais. Ungesema unataka kuwajua wasaidizi na washauri wa raisi ni kina nani, hao tunawajua kwa sababu wote wanateuliwa kwa kitangazwa na kuapishwa wazi or privately.

Kuwajua ni sawa ila kuujua ushauri wowote unaotolewa kwa rais ni confidential sasa wewe unataka kujua ili iweje?!. Kitu unachoweza kujua ni ushauri wa bure unaotolewa kwa rais in public kama humu jf. Kuna ushauri kibao tunatoa humu na unatekelezwa!.

Katiba yetu imeweka wazi kabisa kuwa rais atashauriwa na wasaidizi wake lakini halazimishwi kuupokea au kuukubali ushauri wowote!.

Japo mimi sio mtu wa kule ila logic inanieleza kuwa Rais wetu Magufuli huenda ana washauri wazuri tuu na wanamshauri vizuri tuu ila kwa vile halazimishwi kufuata ushauri wowote wa yeyote, then baadhi ya anayoyasema na kuyatenda, he is the man himself , yaani ni yeye mwenyewe ndio kaamua kufanya kazi differently kwa kuwa mkweli daima kutoka ndani ya nafsi yake, kwa kupokea ushauri na kuupuuzia hivyo naamini anapokea kila ushauri hadi huu wa humu jf ila sio lazima aufuate kila ushauri, mwingine anapokea na kuupuuzia, hivyo tunamshuhudia rais wetu akifanya makosa fulani na kuyayarudia tena na tena na huku tumemshauri the right thing to do.

Hili la kuhutubia bila kufuatisha Hotuba alizoandikiwa, japo naliunga mkono kwa rais wetu kuwa huru kwa asilimia 100% chini ya 100% kuzungumza lolote toka ndani ya nafsi yake, lakini lazima awe na uwezo wa kupima, anazungumza nini, wapi na matokeo ya matamshi hayo!, yaani awe na uwezo wa kufikiri kabla ya kusema au kufikiri kabla ya kutenda, ili rais rais wetu asiseme maneno ya hovyo, au kutenda matendo ya hovyo.

Magufuli sio rais wa kwanza kuandikiwa hotuba, na kisha kuweka pembeni Hotuba za kuandikiwa na badala yake kutoa maneno yake mwenyewe kichwani. Hata Mwalimu Nyerere mara kibao alihutubia kutoka kichwani, alikuja na talking notes only.

Pia sio hotuba zote ni lazima ziandikwe, hotuba nyingine huibuka tuu impromptu, na hazijapangwa. Ila pia pamoja na uhuru wa raisi wetu kuongea chochote popote, yeye kama rais anawajibu wa kuchunga sana kauli zake kwa sababu huyu sasa sio Magufuli tuu bali ni Magufuli na ni rais Magufuli. Anapozungumza, lazima awe na uwezo wa kutenganisha ni wakati gani anazungumza kama mtu binaadamu anayeitwa John Pombe Joseph Magufuli, na ni wakati gani anazungumza kama rais wa JMT, ambaye ni John Pombe Magufuli.

Hawa ni watu wawili tofauti. John Pombe Magufuli ni mtu ni binadamu hivyo ana uhuru wake kuzungumza lolote, popote na kwa yeyote. Huyu ni mtu kama mtu mwingine yeyote na anao uhuru wa kuongea chochote kama ulivyotolewa na kipengele cha freedom of speech and expression kwenye katiba yetu.

Lakini Magufuli anapoongea kama rais wa JMT, hapa hawezi kuongea chochote kwa sababu urais ni taasisi na mamlaka, hivyo kauli yeyote ya rais ni amri yenye mamlaka, authority. Hivyo hawezi tuu kujisemea chochote na popote na hapa ndipo anapohitaji wasaidizi wa kumsaidia aseme nini na wapi.

Hata hivyo naamini baadaye mwaka huu, Rais Magufuli atasoma hotuba ya kuandikiwa neno kwa neno bila hata kuongeza neno moja, siku atakapolihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kule New York nchini Marekani wakati wa kikao cha UN General Assembly, kwa sababu Hotuba hiyo ni lazima iandikwe kwa moja ya Lugha 4 za UN na hairuhusiwi kuongezea maneno toka kichwani. Kwa vile Tanzania tunatumia Kingereza, then hotuba hiyo itakuwa katika lugha ya Kiingereza! .

NB. Tanzania tukiamua rais wetu anaweza kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa lugha ya Kiswahili halafu wakalimani wakatafasiri kwa zile lugha 4 za UN! . Hata akihutubia kwa Kiswahili bado atasoma Hotuba rasmi na sio kutoa kichwani, hili likifanyika la rais kuhutubia kwa kutumia hotuba aliyoandikiwa, kama kutatokea maneno ya hovyo katika hotuba hizo za kuandikiwa, then tutajua kumbe hili la rais kutamka baadhi ya maneno ambayo sio, tatizo sio la rais Magufuli, bali ni la waandishi wake wa hotuba. Lakini akisoma hotuba aliyoandikiwa na kusisikike maneno ya hovyo hovyo, then hapa mtakubaliana na mimi, tatizo litakuwa wapi!.
Paskali
 
"....Hata hivyo baadaye mwaka huu, Rais Magufuli atasoma Hotuba ya kuandikiwa neno kwa neno bila hata kuongeza neno moja, siku atakapolihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kule New York nchini Marekani wakati wa kikao cha UN General Assembly, kwa sababu Hotuba hiyo itakuwa katika lugha ya Kiingereza! ."

Hahahhhahaha Mungu atupe uhai tuione hiyo siku.
 
Hotuba ya kiingereza hawezi kupiga freestyle. Huko wamekaa magwiji umoja wa mataifa,
Akina kabwe na Masamaki hawapatikani huko.

Umoja wa mataifa kuna matetemeko ya kipimo cha 300 na pale ndio kambi ya fitna duniani,kila neno wanalitafakari

Mimi nashauri zile coca cola za msisimko zipigwe marufuku

Ila pasco mbona mshauri wa uchumi alimtangaza hadharani?
 
Ntanunua bando la mwezi nisikilize anavyotengua uteuzi wa obama na kumsimamisha kazi vladmir putin
 
Siyo lazima Magufuli wetu aende New York, na mama yetu Suluhu Makamu wetu wa Raisi kazi yake ni ipi? Hiyo ndiyo kazi yake kama ukiniuliza mimi, hivyo hata New York pia ataenda Makamu wetu Raisi kama hauupendi huwo utaratibu basi pole, na jipangeni mbadilishe Serikali 2020 muweke Eurocentric people kama Membe, fisadi Lowasa au sijui Rostam Aziz lkn mpka 2020 Magu wetu runs the show!
 
NB. Tanzania tukiamua rais wetu anaweza kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa lugha ya Kiswahili halafu wakalimani wakatafasiri kwa zile lugha 4 za UN! . Hata akihutubia kwa Kiswahili bado atasoma Hotuba rasmi na sio kutoa kichwani! .
Pasco
Atashindwa kusema "fyokofyoko" kwa kiingereza...
"Atakayeleta fyokofyoko basi fyokofyoko itamrudia yeye" Rais JPM, 3 Septembe 2016, Zanzibar.

Hii kwa kimombo sijui atasemaje...
Labda: If you bring bullsh.t, I will sh.t on you in return...
 
Kabisa Mkuu nakubaliana na were 100%...asiende tu kutusitiri aibu ya karne...au akienda hotuba yake iwe kwa kiswahili (ingaweje kiswahili nacho kwake bado ni changamoto (kama miugiza, kipeuo cha kwanza) ila kwa vile wasikilizaji walengwa watakuwa hawajui kiswahili basi haitakuwa na shida) na akishamaliza arudishwe hotelini haraka sana asipewe Muda wa kujichanganya na marais wenzake

 
Nadhani hoja muhimu ni maamuzi na matamko ya Raisi yenye utata na ambayo hayajatafitiwa vizuri kwanza ambayo yanaweza kuitia nchi hasara au dosari.

Kumbukeni kawaida maamuzi na matamko ya Raisi huchukuliwa moja kwa moja kumaanisha msimamo wa serikali na nchi.
 
Jamani mbona mnakuwa na roho kuntu,rais hajasafiri kwenda ng'ambo tumuache aitumie platform hiyo kujitambulisha kwa jumuia ya kimataifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…