Haipaswi kufuata ushauri wa yeyote!. Wanabodi,
...Katiba yetu imeweka wazi kabisa kuwa rais atashauriwa na wasaidizi wake lakini halazimishwi kuupokea au kuukubali ushauri wowote !...
Hili la kuhutubia bila kufuatisha Hotuba alizoandikiwa, naliunga mkono kwa rais wetu kuwa huru kwa asilimia 100% chini ya 100% kuzungumza lolote toka ndani ya nafsi yake! .
Magufuli sio wa kwanza kuweka pembeni Hotuba za kuandikiwa na badala yake kutoa maneno yake kichwani, Hata Mwalimu Nyerere mara kibao alihutubia kutoka kichwani! . Sio Hotuba zote ni lazima ziandikwe. Hata hivyo baadaye mwaka huu, Rais Magufuli atasoma Hotuba ya kuandikiwa neno kwa neno bila hata kuongeza neno moja, siku atakapolihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kule New York nchini Marekani wakati wa kikao cha UN General Assembly, kwa sababu Hotuba hiyo itakuwa katika lugha ya Kiingereza! .
NB. Tanzania tukiamua rais wetu anaweza kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa lugha ya Kiswahili halafu wakalimani wakatafasiri kwa zile lugha 4 za UN! . Hata akihutubia kwa Kiswahili bado atasoma Hotuba rasmi na sio kutoa kichwani! .
Pasco