Naanza biashara ya kuku, wapi nipeleke kati ya Dar es Salaam na Dodoma?

Naanza biashara ya kuku, wapi nipeleke kati ya Dar es Salaam na Dodoma?

Burn the bridge _Tz

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2021
Posts
2,319
Reaction score
6,878
Habari...

Nipo mkoa wa Tabora nataka kufanya biashara ya kuku na kupeleka Dar es salaam au Dodoma je wapi ni sahihi?

Faida za Dodoma
Bei inaweza kuwa juu kutokana na nature ya watu wanaoishi huku(Target costumer ni mostly employed)

Ukaribu na Tabora kwa usafiri wa roli.

Faida ya Dar es salaam,
Faida za ni uhakika wa wateja.
Changamoto ni safari ndefu lakini pia usafiri kuku kuibiwq nk

Je nipeleke kuku wapi?
 
Usha toka Zanzibar mkuu
Unafatilia maisha ya wanaume wenzio?
Jitahidi kuwa na tabia za kiume japo mjomba wako ameshakuharibu tangu standard 7


Muda mwingine unapatwa na mithiani kwasababu ya kufatilia maisha ya watu haya unaniuliza mimi kuhusu Zanzibar kwanini usijiulize kuhusu Tukio lako la kuibiwa Hela kizembe
Watu kama nyie kuwajibimu ni kama nawapa brand ty nitokeee
 
Unafatilia maisha ya wanaume wenzio?
Jitahidi kuwa na tabia za kiume japo mjomba wako ameshakuharibu tangu standard 7


Muda mwingine unapatwa na mithiani kwasababu ya kufatilia maisha ya watu haya unaniuliza mimi kuhusu Zanzibar kwanini usijiulize kuhusu Tukio lako la kuibiwa Hela kizembe
Watu kama nyie kuwajibimu ni kama nawapa brand ty nitokeee
Mbona kama hajauliza vibaya mkuu?
 
Ustaarabu wa hali ya juu, Weka namba uokote!
Kaka sijakuuliza kwa Nia mbaya nashangaa unaanza Kuni attack masikini, Sasa mambo ya mjomba wangu yameingiaje hapa? Mi niona nyuzi zako zamani ulikua unahamasisha vijana waende Zanzibar Kuna fursa nikashanga Leo unaleta habari za kuku, kaka nikaona nikuulize kiundani sikujua kama utalipokea tofauti nisamehe ka nmekukera bro ishi sana.
 
Sasa wewe inakusu Nini??
Unashangaa Nini unanilipia Kodi au unanilipia Hela ya kula mpka ushangae mimi kuondoka sehemu mmoja kwenda sehemu ingine?
Uniulize kiundani mimi nani yako??
Hizo tabia za umbea TU nitokee

Na huna huo ustarabu ambao una pretend kuwa nao shame on you
Unatangaza biashara na kuomba ushauri bado unafokea unaowaomba ushauri. Kweli wabongo wengi tuna changamoto ya afya ya akili.


Anyway kwa dodoma soko la kuku lipo tena zuri sana lakini je target ya soko lako ni hipi. Mahotel au waranguzi Ili nao wakauze kwingine?. Kwa mahoteli hakikisha una connection Moja kwa Moja ya hayo mahoteli.

Kwa waranguzi hapa kubali kula panga kuku kuanzia buku 10k mpaka 13k ili naye apate buku au buku mbili na hii ndio soko la uhakika hukai na mzigo, sio hayo mahoteli makubwa ambayo yanahitaji connection nzito na uvumilivu mkubwa.
 
Back
Top Bottom