Na hakuna asiejua kwamba hizi timu mbili zote simba na yanga zina kamati maalum za wataalam wa mambo ya kiroho ila simba huwa inafanya wazi.
Tetesi zilizopo ni kwamba katika marekebisho ya uwanja, Yanga walitumia mwanya huu kupenyeza wataalam kubaini na kuziondoa ndumba za Simba, magreda yalitumika kuzifukua zilizofukiwa uwanjani ikiwemo ndumba mama ambayo ni kubwa kuzidi zote, power driller zilitindua sakafu kuzitoa za vyumbani, n.k.
Kamati ya ufundi ya Simba walistukia mchezo ila hawakuwa na la kufanya, wataalam wao hawakuruhusiwa kuingia hata kwa gia ya vibarua wa kusaidia kazi.
Kilichofanyika ni kuitoa ndumba mama ya Simba na kuweka ya Yanga tena yenye nguvu zaidi, imefukiwa na kusakafiwa vilivyo. kwa sasa ni kwamba zile ndumba za simba za wachezaji kuvaa viunoni, kuweka golini, mashabiki kuingia nazo, wachezaji kutumwa kuziweka kabla ya mechi, n.k. zitadidimizwa na ndumba mama mpya.
Kuzitoa hizi ndumba sio suala la siku 1, yaweza chukua hata wiki nzima na kibali inabidi kiwepo cha kuingiza greda kubwa chimba na kuanza kutindua zege nene, hapa ndipo penye shida.