Taifa la Irani linaongozwa kwa utaratibu wa dini ya KISHIA.
Usahihi 1 : Taifa la
Iran linaongozwa kwa kufuata misingi ya
dini ya
kiislamu lakini chini ya mwamvuli wa
dhehebu la
shia.
Usahihi 2 : Hakuna
dini ya shia ila kuna dini ya
kiislamu yenye
madhehebu mbalimbali
shia ikiwa ni miongoni mwa madhebu hayo.
Muasisi wa USHIA alikuwa MYAHUDI.
Usahihi: Hakuna
myahudi aliyeasisi dhehebu la shia. Dhehebu la
shia lilitokea kupitia
mgogoro wa
kugombea madaraka kati ya
wafuasi wa mtume pamoja na
wanafamilia wa bwana mtume.
Chanzo kikuu cha mgogoro:
Mara baada ya mtume kufariki, huku nyuma kulitokea
mgogoro mkubwa wa kugombea madaraka hali ambayo ilipelekea kuchelewesha
mazishi yake.
Mtume hakuwa ameandaa
mrithi wake, hivyo kulitokea makundi makuu
mawili ambayo ni:
a) Wafuasi (umma) pamoja na Wafuasi wake wakuu ( Maswahaba), hawa walimpendekeza
Abu Bakr na
alikubali kupendekezwa.
Hoja zao:
1) Uongozi inabidi uachwe kwa umma na siyo kwa familia.
2) Abu Bakr inaaminika ndiye alikuwa
msiri na
rafiki mkuu wa mtume.
3) Abu Bakr inaaminika alikuwa na
hekima na
busara kutokana na utu
uzima wake.
4) Abu Bakr ndiye
aliyechaguliwa na mtume
kuendesha sala wakati yeye anaumwa.
5) Ali alikuwa kijana.
b) Kundi la wanafamilia (wanandugu) ,hawa walimpendekeza
Ali na
alikubali kupendekezwa.
Hoja zao:
1) Alikuwa na elimu kubwa.
2) Inasemekana kuwa mara nyingi mtume alikuwa akimtaja na kumsifia kama ni mtu mjuzi, mwerevu,hekima, maarifa na mwenye busara sana.
3) Alikuwa kipenzi cha mtume.
4)Alikuwa binamu wa mtume.
5) Alilelewa na kukulia kwa mtume.
Mshindi: Baada ya mjadala mzito hatimaye
Abu Bakr alichaguliwa kama kiongozi
(Khalifa) mkuu wa kisiasa baada ya kifo cha mtume, kisha Ali akaingizwa kwenye baraza kuu la uongozi,ingawaje alijitoa baadaye.
Baada ya hapa ndipo ukatokea ule msemo kuwa
'uislamu ulienea kwa upanga', ilitumika nguvu kubwa sana kuleta ushawishi mpya mara baada ya mtume kufariki.
Ukimtoa Abu Bakr, viongozi wote (makhalifa)
waliuawa wakiwa madarakani na hawakumaliza uongozi wao.
Hivyo Shia wanaamini:
Mtume alimchagua mrithi wake na mrithi huyo ni Ali.Sababu zao:
1) Hija ya mwisho ya mtume
Hapa
hadithi zote zinaikubali hii
kauli
Wakati wa hija ya mwisho , wakati wanarudi mtume alisimamisha msafara kisha akatoa kauli hii:
"man kuntu mawlāhu fa-ʿAlī mawlāhu"
Kwa lugha ya
kiingereza:
"He of whom I am the mawla, of him Ali is also the mawla"
2) Hadhi (Status) :
Hapa wanasema familia za
mitume na
manabii zimepewa nafasi ya
upendeleo na Mungu kwenye mambo mengi na
uongozi ukiwemo.
Kuhusu Quran:
Shia wanaamini :
Quran katika
mfumo wa maandishi (mpangilio wa
vitabu) ulianza enzi za mtume na siyo wakati wa utawala wa
Uthman.
Nb:Uthuman ndiye aliyefanya maboresho ya Quran kutoka njia ya masimulizi kwenda njia ya maandishi. (Abdullah ibn Saba hapa ndipo utaukubali mziki wake)!!
Nb: Samahani kama kuna mtu atakwazika kiimani kwa uchambuzi wangu.
Nb: Hii ni kozi niliisoma miaka mingi kidogo iliyopita na niliipenda na kuielewa!
Nb: Baada ya hii kozi niligundua kuwa dini zote zimeundwa na kutengenezwa na watu.
Nb: Mungu hana dini.
Nb: Huwezi kutenganisha dini na utamaduni wa jamii husika.
Ni mtazamo wangu!