Naanza kujawa na mashaka. Yawezekana haya mambo ya Iran/Israel ni michongo tu, tunachezewa akili na wakubwa

Hiyo yako ni conspiracy theory iliyoibuka kwenye mtandao baada ya watu kuona mazayuni hawarudishi mapigo.

Ukweli ni kuwa mazayuni mavi debe.
Hawa jamaa huwa wanawasiliana kupitia channel maalum ambazo taarifa zake haziji maa nyingi kwenye mainstream media.
Mfano kabla ya shambulizi la Urusi Syria enzi zile za IS, US na Russia walikuwa wanawasiliana na kupeana mipaka ya maeneo yq mashambulizi.

Hata Iran imewasiliana sana na US kabla ya shambulizi lake kupitia Misri na Uturuki.
 
Shia wamefundishwa kuwa watiifu kwa Iran.

Salafi/Answar Sunna wamefundishwa kuwa watiifu kwa utawala wa Saudi Arabia.

Hao wote jinsi walivyo ni kama jeshi la akiba kwa hao watawala wa hayo mataifa.
Unamaanisha dini maeneo hayo zinatumiwa kisiasa zaidi
 
Yup!

Wanazitumia kisiasa.

Ukitaka kuliona hili kwa wazi jiulize kwa nini Saudi Arabia ime normalise mahusiano yake na Israel lakini na Iran tofauti?

Huku mwengine anakuambia wairan ushia umeanzishwa na wayahudi hao wote ni wamoja.

Swali litakuja; kama wote ni wayahudi kivipi uhusiano kwa Israel kwa upande wa Saudia ni sawa ila kwa upande wa Iran kwa Saudia si sawa?
 
Ni kweli, Kuna kipindi Iran na Israel walikuwa na ukaribu sana, na tenda nyingi za majengo makubwa walifanya kazi jamaa kutoka uyahudi. Ila nmnimeona Saudia imekuwa ikitimika kukusanya taarifa za kiintelijenisia iran na kushare na wayahudi. Hawa jamaa wote naamini kuna layer flani wanàwasiliana na wanajuana ukiacha layer hii ya taarifa tunazopewa.
Hata viongozi wakubwa wa kidini huko sitashangaa kama sio sehemu ya majasusi wa mashirika wakubwa duniani.
 
Taifa la Irani linaongozwa kwa utaratibu wa dini ya KISHIA.
Usahihi 1 : Taifa la Iran linaongozwa kwa kufuata misingi ya dini ya kiislamu lakini chini ya mwamvuli wa dhehebu la shia.

Usahihi 2 : Hakuna dini ya shia ila kuna dini ya kiislamu yenye madhehebu mbalimbali shia ikiwa ni miongoni mwa madhebu hayo.
Muasisi wa USHIA alikuwa MYAHUDI.
Usahihi: Hakuna myahudi aliyeasisi dhehebu la shia. Dhehebu la shia lilitokea kupitia mgogoro wa kugombea madaraka kati ya wafuasi wa mtume pamoja na wanafamilia wa bwana mtume.

Chanzo kikuu cha mgogoro:

Mara baada ya mtume kufariki, huku nyuma kulitokea mgogoro mkubwa wa kugombea madaraka hali ambayo ilipelekea kuchelewesha mazishi yake.

Mtume hakuwa ameandaa mrithi wake, hivyo kulitokea makundi makuu mawili ambayo ni:

a) Wafuasi (umma) pamoja na Wafuasi wake wakuu ( Maswahaba), hawa walimpendekeza Abu Bakr na alikubali kupendekezwa.

Hoja zao:

1) Uongozi
inabidi uachwe kwa umma na siyo kwa familia.

2) Abu Bakr inaaminika ndiye alikuwa msiri na rafiki mkuu wa mtume.

3) Abu Bakr inaaminika alikuwa na hekima na busara kutokana na utu uzima wake.

4) Abu Bakr ndiye aliyechaguliwa na mtume kuendesha sala wakati yeye anaumwa.

5) Ali alikuwa kijana.

b) Kundi la wanafamilia (wanandugu) ,hawa walimpendekeza Ali na alikubali kupendekezwa.

Hoja zao:

1) Alikuwa na elimu kubwa.

2) Inasemekana kuwa mara nyingi mtume alikuwa akimtaja na kumsifia kama ni mtu mjuzi, mwerevu,hekima, maarifa na mwenye busara sana.

3) Alikuwa kipenzi cha mtume.

4)Alikuwa binamu wa mtume.

5) Alilelewa na kukulia kwa mtume.

Mshindi: Baada ya mjadala mzito hatimaye Abu Bakr alichaguliwa kama kiongozi (Khalifa) mkuu wa kisiasa baada ya kifo cha mtume, kisha Ali akaingizwa kwenye baraza kuu la uongozi,ingawaje alijitoa baadaye.

Baada ya hapa ndipo ukatokea ule msemo kuwa 'uislamu ulienea kwa upanga', ilitumika nguvu kubwa sana kuleta ushawishi mpya mara baada ya mtume kufariki.

Ukimtoa Abu Bakr, viongozi wote (makhalifa) waliuawa wakiwa madarakani na hawakumaliza uongozi wao.

Hivyo Shia wanaamini:

Mtume alimchagua mrithi wake na mrithi huyo ni Ali.Sababu zao:

1) Hija ya mwisho ya mtume

Hapa hadithi zote zinaikubali hii kauli

Wakati wa hija ya mwisho , wakati wanarudi mtume alisimamisha msafara kisha akatoa kauli hii:

"man kuntu mawlāhu fa-ʿAlī mawlāhu"

Kwa lugha ya kiingereza:

"He of whom I am the mawla, of him Ali is also the mawla"

2) Hadhi (Status) :

Hapa wanasema familia za mitume na manabii zimepewa nafasi ya upendeleo na Mungu kwenye mambo mengi na uongozi ukiwemo.

Kuhusu Quran:

Shia wanaamini :

Quran katika mfumo wa maandishi (mpangilio wa vitabu) ulianza enzi za mtume na siyo wakati wa utawala wa Uthman.

Nb:Uthuman ndiye aliyefanya maboresho ya Quran kutoka njia ya masimulizi kwenda njia ya maandishi. (Abdullah ibn Saba hapa ndipo utaukubali mziki wake)!!

Nb: Samahani kama kuna mtu atakwazika kiimani kwa uchambuzi wangu.

Nb: Hii ni kozi niliisoma miaka mingi kidogo iliyopita na niliipenda na kuielewa!

Nb: Baada ya hii kozi niligundua kuwa dini zote zimeundwa na kutengenezwa na watu.

Nb: Mungu hana dini.

Nb: Huwezi kutenganisha dini na utamaduni wa jamii husika.

Ni mtazamo wangu!
 
Utaumiza kichwa hapo 😅😅tena sana ,hao wanacheza na roho za watu ...Vita hapo haitoisha ila kwa ground wachache wanakufa kwa uzembe wa viongozi.

Ukitaka kujua hamna vita ni utapeli chukua media mbili BBC na Aljazeera ,then angalia wanavyofanya coverage kweny kuripot vita.

Bahati mbaya ,wabongo nao wanajifanya wachambuzi wa vita ,huku Tz unakuta mtu anachambua mambo ya huko Middle east kama sio umbea ni nn!?
 
Unaweza kuzungumziq kuanzia kwa caliph uthman. Maana baada yake ndio tifu lilikuwa kali zaidi. Ali aliendelea kudhurumiwa upngozi
 
Utaumiza kichwa hapo 😅😅tena sana ,hao wanacheza na roho za watu ...Vita hapo haitoisha ila kwa ground wachache wanakufa kwa uzembe wa viongozi.

Ukitaka kujua hamna vita ni utapeli chukua media mbili BBC na Aljazeera ,then angalia wanavyofanya coverage kweny kuripot vita.

Bahati mbaya ,wabongo nao wanajifanya wachambuzi wa vita ,huku Tz unakuta mtu anachambua mambo ya huko Middle east kama sio umbea ni nn!?
😆 acha tuchambue bhana. Wanadamu wote ni ndugu
 
King Faisal (1906-1975), who ruled the Kingdom between 1964-75, confirmed Jewish ancestry of Saudi Royals. In an interview to Washington post on September 17, 1969, King Faisal is reported to have said “We, the Saudi family are cousins of the Jews.
Nimecheka sana, kwahiyo hapo ndio ushahidi wa kuwa yeye au wao ni Wayahudi ?

Hili nilikuwa tu ya kuwa lazima utakuwa hauna ushahidi. Hapa nataka uje na ushahidi kuonyesha wao ni Mayahudi, kusema "Cousins" sio ushahidi ya kuwa wao ni Mayahudi, kama vile Wakristo wanavyodai Waislamu ni watoto wa mama mdogo, hii haimaanishi ya kuwa Wakristo nao ni Waislamu.

Au kama wanavyotuita Wakristo.
 
Hiyo janja ya Iran, uongo huo wa Iran, yaani hapo Iran anajua kabisa Myahudi anaenda angamiza kizazi chao, wataangamizwa vibaya sanaaaa na Iran anajua pia USA and allies wanawanyemelea sana, sasa sbb kubwa imepatikana ya kuipiga Iran, Iran italia sana, watulie wasubirie kipigo na hofu kubwa kwa Iran ni baada ya kupiga mabomu na drones jumla 385 na zilitunguliwa zoteee na 7 tu zilifika Israel na kukosa targets, yaani hapo wanajua kabisa wao hawana mfumo mzuri wa ulinzi wa anga, watafumuliwa vibaya, sasa wanaanza kulia lia kabla ya kipigo

Hivi ukiwa na akili huo si uongo wa wazi, yaani uambiwe eti wacha au kubali upigwe usijibu, uongo mkubwa huo, Iran hadi hapo tumbo la kuhara tayari, Ayatollaah hapati usingizi wala choo siku ya 4 leo hofu imemjaa sanaaa
asa hivi sio zama za kukariri flan ni mkali wanyonge wa sasa wamepiga hatua hakuna anae taka kukurupuka na iran wanajua kashaota pembe
 
Wewe nani ukatae? Wakati wenyewe waliyo kwenye huo ukoo wanakiri hili kwamba wao ni wayahudi.

Bado nasubiri ulete ushahidi ya kuwa familia ya Saudi ni Mayahudi.
Sasa unachopinga ni nini?
Kama inavyofahamika kuwa Shia wanafuata attribution za imamu wawili 2. Vitabu wanavyovifuata ni vinne (4):

1)Al Kahf
2)Man la Yahduruhu Al Faqih
3)Al Istibsar na
4)Attahdhib

Halafu sanadi za vitabu kama Usual al Kahf na Furu'u yake zilivyo jaa uzandiki.

Mnajua kama nyinyi Mashia hamna hata elimu ya Rijali, kwa zama hizi huku mkidai ya kuwa Al-Khui ndio mwanazuoni wenu wenu wa elimu ya Rijali.

Mbona hujakiweka "Biharul an-War" ?
Asilimia 90% ya ripoti za hivi vitabu vinatokana na maimam wawili.

1) Imam Jaafar Al Sadiq na
2)Imam Muhammad Al Baaqir

Na kuna watu ambao wananukuu kutoka kutoka kwa hao maimam, watu hao ni wanne:

1) Abou Basir
2)Hishan ibn Al Hakam
3) Hisham ibn Salim na
4) Zurarah ibn Ayyun

Na wenyewe sanadi yao inaishia kwa hao wawili ? Hao kina Jaafar na Muhammad Baqir mapokezi yao wameyatoa wapi ? Maana sanadi zenu zimekatika.
 
Hiyo janja ya Iran, uongo huo wa Iran, yaani hapo Iran anajua kabisa Myahudi anaenda angamiza kizazi chao, wataangamizwa vibaya sanaaaa na Iran anajua pia USA and allies wanawanyemelea sana, sasa sbb kubwa imepatikana ya kuipiga Iran, Iran italia sana, watulie wasubirie kipigo na hofu kubwa kwa Iran ni baada ya kupiga mabomu na drones jumla 385 na zilitunguliwa zoteee na 7 tu zilifika Israel na kukosa targets, yaani hapo wanajua kabisa wao hawana mfumo mzuri wa ulinzi wa anga, watafumuliwa vibaya, sasa wanaanza kulia lia kabla ya kipigo

Hivi ukiwa na akili huo si uongo wa wazi, yaani uambiwe eti wacha au kubali upigwe usijibu, uongo mkubwa huo, Iran hadi hapo tumbo la kuhara tayari, Ayatollaah hapati usingizi wala choo siku ya 4 leo hofu imemjaa sanaaa
Leo siku ya nne Israel kimyaa
 
Unaweza ukayaelewa zaidi haya mambo ukisoma sana mambo ya consiprancy utauelewa ulimwengu.
Wakuu wa Dunia wote sio maadui kwani mungu wao ni mmoja na wote Wana ajenda moja.
Hata wakuu wa magaidi wote ni wanachama.
Wanatuchezea TU drama wanafanya kitu inaitwa chao order chao.
Kuchafua Dunia kuvuruga Dunia ili kupitisha ajenda moja
Kwenye uzi wangu wa Undugu wa Mwisrael na Muajemi nimeandika haya.

Pia niliwahi kuwambia watu kuwa US, Russia, China, Irani, Japan hawa watu ni marafiki wazuri sana tu.

Wala hawana ugomvi kama ambavyo wanalaimisha tuamini.

Ndio maana US haiwezi kuishambulia China wala Russia kwa namna yoyote.

Umeniongezea pointi kuwa mungu wao ni Mmoja na agenda yake ni moja tu.
 
Usahihi 1 : Taifa la Iran linaongozwa kwa kufuata misingi ya dini ya kiislamu lakini chini ya mwamvuli wa dhehebu la shia.

Shida sio dhehebu, hakuna ibada anayo fanya Muislamu ambayo inafanana na ibada wanazo fanya Mashia.

Ukipata muda jifunze maana ya neno "Dhehebu".
 
Unaweza ukayaelewa zaidi haya mambo ukisoma sana mambo ya consiprancy utauelewa ulimwengu.
Wakuu wa Dunia wote sio maadui kwani mungu wao ni mmoja na wote Wana ajenda moja.
Hata wakuu wa magaidi wote ni wanachama.
Wanatuchezea TU drama wanafanya kitu inaitwa chao order chao.
Kuchafua Dunia kuvuruga Dunia ili kupitisha ajenda moja
hivi wewe mambo ya wakuu wa dunia unayafahamu na mpaka dini zao?!
Wacha utoto huu
 
Kama inavyofahamika mwanzilishi wa shia ni myahudi inafahamika vilevile kuwa utawala wa saudia asili yao ni myahudi vilevile. Ni babu yao Mkuu, anaitwa Murdakhai Bin Abraham Bin Moshe Al Dounami, kwa jina jingine anaitwa Merkhan. Babu yao ni myahudi wa kabila la Anza ambaye alikuwa akiishi Basra nchini Iraq na baadaye kuhamia Najd na makazi yake akayaweka Diriya

Katika ukoo wa Saudia hakuna damu ya Kiyahudi, na wao asili yao inarudi kwa Banu Amir.

Unajua hizo story unazo leta hazina asili katika Historia bali ni matokeo ya watunzi wa uongo ili kuwasema vibaya Watawala wa Saudia
 
Back
Top Bottom