Bado nasubiri ulete ushahidi ya kuwa familia ya Saudi ni Mayahudi.
Halafu sanadi za vitabu kama Usual al Kahf na Furu'u yake zilivyo jaa uzandiki.
Mnajua kama nyinyi Mashia hamna hata elimu ya Rijali, kwa zama hizi huku mkidai ya kuwa Al-Khui ndio mwanazuoni wenu wenu wa elimu ya Rijali.
Mbona hujakiweka "Biharul an-War" ?
Na wenyewe sanadi yao inaishia kwa hao wawili ? Hao kina Jaafar na Muhammad Baqir mapokezi yao wameyatoa wapi ? Maana sanadi zenu zimekatika.
Nakujibu kiujumla.
Mimi ni sunni, madhheb ya Imam Shafii. Ili kuepuka kuingia kwenye mizani ya kupata dhambi kwa kumdhania mtu
Mapokeo ya elimu niliyopatiwa mimi kabla ya kukizungumzia suala lolote basi niwe na ufahamu nalo. Ufahamu nitaupata kwenye kusoma. Kabla hujamzungumzia jamii fulani ipo hivi mimi nawasoma kwanza.
Kwangu huwa haitoshi nikisikia Sheikh fulani kasema hivi au kasema vile kuhusu jamii fulani ya watu. Kwangu nawasoma kwanza hao watu. Kwangu huwa inanitosha nikisoma vitabu vyao. Nitarudi kule kule pa awali! Lazima nitafute vitabu vyao nithibitishe kile kilichosemwa ni kweli au si kweli.
Baada ya hapo ndiyo natoka na msimamo. Kwangu elimu kwanza kisha ndiyo itafuata itikadi. Hivyo, nimebahatika kusoma miongoni mwa vitabu vya mashia.
Kwa sehemu ya elimu ya kuwajua Shia niliyoielezea kwa bahati mbaya umenidhania kuwa Hammaz ni Shia. Umetumia dhana! Hali ambayo kwenye dini inakatazwa kwa sababu unaweza kumdhania mtu kumbe yupo tofauti na kile ulichomdhani. Katika mlango huu unafahamu zaidi.
Kwa nia nzuri tu naweza kusema kwa kinywa kipana; Moja ya mapungufu mliyokuwa nayo Salafi (Answar Sunna) mtu akiwa tofauti na kile mnachokifahamu huwa mnadondokea kwenye dhana. Taswira yoyote itakayokuja kichwani mwenu mtampachika nayo.
Neno elimu kwenye lugha ya kiarabu lina herufi 3. Kuna ayn, lam na mim: Ayn; Mwanzo mwanafunzi anapoanza kusoma anakuwa "atushani", anakuwa na kiu sana ya kusoma. Kila kitu atameza.
Kwenye herufi lam hapa mwanafunzi anakuwa law wam. Hapa utamkuta mtu anakuwa mshindani, mjuaji, anataka kushindana na kila mtu. Na hii ndiyo Marhala mbaya sana!
Akishatoka kwenye lam anakuja kwenye Mim na anakuwa mutamakin. Hapa anatulia hawi na fujo! Anajua hii ni kauli ya Imam fulani madheheb fulani na dalili yao ni fulani. Anatulia.
Sasa ni nini maana yangu kuelezea hilo! Hakuna mahali ambapo nimepinga kuwa ushia haujatokana na Abdillah ibn Saaba. Hakuna mahala nimepinga!
Bali hoja ilikuwa ni kwa sababu nukta kuu ni uyahudi au myahudi basi hawa ni moja. Ikiwa kama nukta kuu ni uyahudi au myahudi swali litakuja hata Utawala wa Saudia asili yao ni uyahudi. Kwa msingi huo kama nukta ikiwa ni uyahudi au myahudi basi kwa kipimo kilekile anachopimiwa Shia ndicho kipimo hicho hicho apimiwe Saudia. Hii ndiyo ilikuwa hoja.
Sasa kama umekubaliana nayo ni sawa! Kama hujakubaliana nayo ni sawa! Kwa sababu sipo kwa ajili ya kumshurutisha mtu wala sipo kwa ajili ushindani. Hatua hiyo mimi nimeshaipita.
Jawabu langu nalikusanya kwa namna hiyo!