SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Tuweke kwanza pembeni ukweli kuwa huyu muuza nguo anayejiita Sandaland aliyewekwa front kwanza hajui kuvaa sasa sielewi inakuwaje anafanya biashara za nguo wakati anavaa kama Kibu Denis.
Twende kwenye mada kuu.....
Nikipitia kwa haraka jezi ya Simba iliyozinduliwa leo, kuna mambo mawili makubwa yaliyonishangaza.
Kwanza ni katika jezi nyekundu kwa nyuma, kama macho yangu hayajanidanganya nimeona maandishi makubwa ya 5 na 1. Sijui kama yalikuwa random. Niko tayari kukosolewa kama nimeona vibaya.
Pia, najua hili tayari ni lalamiko kwa wengi. Ni neno SANDA lililo kifuani mwa jezi. Mpaka nitakapoona hiyo brand ya Sanda ipo kwenye jezi ya timu ya taifa na ikakubaliwa na TFF, ndiyo nitaanza kufikiria kuwa hakuna nia ovu nyuma ya hili jina. Nadhani Simba haitakiwi kukubaliana na brand hii kwa sasa. Ni ama aondoe hilo jina katika jezi, abadilishe jina lake au mkataba wake uvunjwe.
Simba kama taasisi inatakiwa ifanye kazi na wazabuni ambao majina na shughuli zao hazihatarishi kwa namna yoyote ile ustawi wa brand ya Simba na sidhani kama brand ya Sanda inaendana na hili. Ukiacha ukakasi wa jina, pia inafungua milango ya wanasimba kukejeliwa na hiyo itahatarisha mauzo ya jezi. Tulivumilia "Sandaland" ambayo nayo kiukweli ilikuwa na ukakasi, ila huku alipofika kwenye SANDA siyo kabisa.