Naanza kupata wasiwasi na Sandaland kama mtengenezaji wa jezi za Simba

Naanza kupata wasiwasi na Sandaland kama mtengenezaji wa jezi za Simba

Simba club kubwa lakini bado inafanya mambo ya kishamba sana sidhani kama inatambua thamani yake aise.
 
Upumbavu huu.
Kwa hiyo kama gari ameweka special number ya SANDA ndiyo itufanye sisi tukubali kuvaa Sanda?

Hivi ukikuta bus limesajiliwa kwa jina " JENEZA unadhani litapata abiria?

Au liandikwe MORTUARY halafu lipate abiria!!?
Mimi mwenyewe nashangaa wanakuja na hoja nyepesi eti ndiyo jina lake au eti ameweka kwenye magari yake ya kifahari, kwa hiyo?

Kwahiyo kesho huyo Sanda akibadili jina lake akajiita "Yanga" basi Simba haitakuwa na budi bali kuweka jina hilo katika jezi? Aisee....
 
Sanda,,. Hata kama kila nafsi itaonja mauti lakin kuvaa Sanda ungali hai yataka moyo.
 
Iwe Sanda au iwe Sandaland bado hii sio brand ya vifaa vya michezo zikiwemo jezi...

Huu ni mradi tu kama miradi mingine, upo unique na una timeline kulingana na mkataba kati ya Simba na huyo Sanda...

Simba inahitaji jezi, hivyo ili kukamilisha habari ya kupata jezi ikatafuta mjanja wa kwanza ambaye ni mchuuzi Guangzhou aitwaye Fred, na sasa kuna mjanja mwingine aitwaye Sanda...

Kitu wanachokifanya Simba ni kuamua tu kuondokana na stress za wao kwenda viwandani kuweka order bila kupitia wachuuzi...
 
Zenye neno fila wanavaa na hawahoji, ila mtanzania wanamwekea uzito, yaani huyo mbumbumbu amzidi uchungu wa pesa yake sandaland aliyewekeza
FILA ina maana gani?
FILA Haina tatizo lolote kama hauna matatizo ya kuchanganya L na R.
 
FILA ina maana gani?
FILA Haina tatizo lolote kama hauna matatizo ya kuchanganya L na R.
Anajitungia hoja zisizo na kichwa wala mguu ili tu abishane
 
Mkuu usimlaumu sana jamaa huwenda nyie hamna pesa za kuchukua material t-shirt za bei nzuri huko china mkaamua mchukue za bei ya kati nyie watoto wa mujini 😎 mkaita ubaya ubwela sasa imekuwa ubaya ubwege Cc ephen_
Kwenye material sio issue sana,kaleta kulingana na uwezo wa wateja. Vipi kuhusu sanda? Ina maana hakujiuliza hata kidogo tu kama inaweza kumletea shida?
 
Tuweke kwanza pembeni ukweli kuwa huyu muuza nguo anayejiita Sandaland aliyewekwa front kwanza hajui kuvaa sasa sielewi inakuwaje anafanya biashara za nguo wakati anavaa kama Kibu Denis.
😂😂😂😂 akili za maskini bhana kwahyo ukiwa mfanya biashara wa nguo ujue kuvaa na ni kuvaa gani huko asikojua jamaa kwamba shati anavaa miguuni suruali kichwani au.....

unataka kuniambia leo anayefanya biashara ya samaki pale ferry ni lazima ajue kuvua samaki?

wabongo msiwe wajinga kwa kula ugali...... neno SANDA linamaana nyingi na usitake kuniambia ww tu mleta mada ndio una uchungu kuliko mwenye brand yake mpka kuona kakosea kuandika...

punguza chuki umaskini wako usiushupaze kwenye akili utapata ukichaa
 
Ata mkiwekewa VUNJA BEI ingefaa tu jezi yenu ni gazeti
 
Kwenye material sio issue sana,kaleta kulingana na uwezo wa wateja. Vipi kuhusu sanda? Ina maana hakujiuliza hata kidogo tu kama inaweza kumletea shida?
Kaka si jina lake ni sandalandi kajifupisha kajiita sanda ila naskia msimu huu ndio mkataba wake na Simba unamalizika
 
😂😂😂😂 akili za maskini bhana kwahyo ukiwa mfanya biashara wa nguo ujue kuvaa na ni kuvaa gani huko asikojua jamaa kwamba shati anavaa miguuni suruali kichwani au.....

unataka kuniambia leo anayefanya biashara ya samaki pale ferry ni lazima ajue kuvua samaki?

wabongo msiwe wajinga kwa kula ugali...... neno SANDA linamaana nyingi na usitake kuniambia ww tu mleta mada ndio una uchungu kuliko mwenye brand yake mpka kuona kakosea kuandika...

punguza chuki umaskini wako usiushupaze kwenye akili utapata ukichaa
Haendani na anachouza. Sina hiana naye na namtakia kila la kheri katika shughuli zake. Ni ukosoaji wenye nia ya kujenga, atanisamehe kama nimetumia lugha ya ukali, ni katika kuweka msisitizo tu katika hoja.

Vipi lakini, zile namba 5 na 1 haujaziona katika jezi nyekundu au hizo tutaanza kuzijadili lini?

Kwa kumalizia, wangapi wanafanya maamuzi kwa hisia na uchungu lakini yanakuwa siyo maamuzi sahihi hata kwao? Sishangai hoja yangu kujibiwa na baadhi mnavyojibu maana katika kuendesha biashara kisasa bado tupo nyuma saaana. Sanda katika lugha yetu siyo vitunguu, sanda ni nguo. Unapoihusisha na brand ya nguo automatically unasema nguo hiyo ni SANDA tunayoijua sisi!
 
Yaani mtu anaitwa KUMALIJA aamue kulifupisha jina lake kwa kuondoa herufi nne za mbele tuone ni sawa tu?

Kule Usukumani hili jina KUMALIJA lipo sana ila huwezi kuwasikia wamelifupisha maana wanajua madhara yake.

Sandaland ajiandae kuzivaa hizo jezi yeye mwenyewe. Shwaini!
 
Kwani Kumalija kifupi inakuwaje 😅😅😅
 
Upumbavu huu.
Kwa hiyo kama gari ameweka special number ya SANDA ndiyo itufanye sisi tukubali kuvaa Sanda?

Hivi ukikuta bus limesajiliwa kwa jina " JENEZA unadhani litapata abiria?

Au liandikwe MORTUARY halafu lipate abiria!!?
Sikulazimishi kuamini, ila mimi najua Mkurugenzi wa Sandaland (sio Sunderland) anaitwa Sanda Omary Yenga
 
Sikulazimishi kuamini, ila mimi najua Mkurugenzi wa Sandaland (sio Sunderland) anaitwa Sanda Omary Yenga
Kwa hiyo msimu ujao akiamua kutumia jina lake hilo la mwisho katika jezi ya Simba yote shega si ndiyo?
 
Usidhani wamekosema, wanataka attention. Hizo drama na wanajua wabongo mnapenda drama
 
Kwa hiyo msimu ujao akiamua kutumia jina lake hilo la mwisho katika jezi ya Simba yote shega si ndiyo?
Kama mkataba unampa uhuru wa kutangaza moja ya bidhaa zake, atakuwa sahihi tu. Hata akiamua kuitumia nafasi aliyopewa kwenye jezi kuitangaza GSM, ni sawa tu. Mkataba uheshimiwe
 
Kama mkataba unampa uhuru wa kutangaza moja ya bidhaa zake, atakuwa sahihi tu. Hata akiamua kuitumia nafasi aliyopewa kwenye jezi kuitangaza GSM, ni sawa tu. Mkataba uheshimiwe
Umeamua kujitoa ufahamu ila umesisitiza keyword hapo ni "mkataba". Na mimi hoja yangu ilikuwa mkataba wa aina hii kwa taasisi yoyote makini lazima uwe na vipengele vya kuilinda taasisi dhidi ya mabadiliko yoyote ya kiutendaji, umiliki au kisheria ya upande wa pili yanayoweza kuhatarisha ustawi wa brand ya taasisi. Nitashangaa sana kama vipengele hivyo havipo katika mkataba wa Simba na Sandaland.

Hivi leo GSM akiinunua Sandaland katikati ya mkataba wake na Simba ila akaiacha iendelee kujiendesha, unadhani mkataba utaendelea bila Simba kuwa na haki ya kuhoji au kuvunja mkataba? Hivi leo Sandaland katika biashara zake nyingine nje ya Simba ikiamua kupromote mambo yasiyo na maadili, unadhani Simba haitakuwa na nguvu ya kuvunja mkataba?
 
Back
Top Bottom