D2050
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 1,919
- 1,094
Sijui huko aliko kama amepata mwingine ukiacha wale aliokuwa nao,me nimechoshwa na kivuli hiki nataka kuwa huru tena.
Naona nawewe umepata mwingine unataka uolewe nae.ndio anaekufanya udai talaka
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijui huko aliko kama amepata mwingine ukiacha wale aliokuwa nao,me nimechoshwa na kivuli hiki nataka kuwa huru tena.
Asante mkuu, nina watoto wawili,kinachofanya nifocus kwenye talaka ni baada ya kuhitilafiana mwenzangu hakuona umuhimu wa kukaa kikao badala yake yeye na mama yake wakaungana kunishambilia Mimi kwa maneno,na kushauriana atafute m/mke mwingine na alifanya hivyo..kwa miaka hiyo miwili ameshaishi na wanawake watatu na kuachana nao...sioni kama kuna umuhimu wa kusuruhisha kwa sasa.
kwa hiyo issue ni mama mkwe ndiye tatizo kuu na si mumeo? uliwahi kuchukua hatua dhidi ya mama mkwe?....na unaweza kuthibitisha mbele ya watoa talaka kuwa mumeo ameshaoa huko aliko?
Ni Ndoa ya kanisani, mahakama haivunji Ndoa ya kanisa mkuu?lengo langu ni official divorce mkuu.
Hata kama ni ndoa ya kanisani, mahakama inaweza kutoa taraka though ni mlolongo mrefu kidogo unaohitaji uvumilivu. Issue yako ulishagaifikisha kwa viongozi wa kanisa? unatakiwa uanzie kanisani, huko watafanya process za kuwasuruhisha, ikishindikana sasa ndo watakupa barua ya kwenda mahakamani, mahakamni nako watawasikiliza mwisho ndio mahakama itaamua kama kuna haja ya kutoa taraka au la!
kwa kuwa upo peke yako unaongea hapa ndio utaonekana upo sahihi kabisa akija wa upande wa pili akitoa hoja sijui itakuwaje ndio maana wanasema ndoa ni kifungo wewe endelea upate taraka uleee matoto yasiyokuwa na malezi ya baba
Kizazi hiki!!!!Huwa napata shida sana kushauri watu wa aina yako (waliofunga ndoa kimyakimya halafu wakaenda kuhalalisha kanisani nafikiri unanielewa) Sasa kwa vile mlipata kibali kanisani hebu soma hapa: mathayo 19:6. Kwa andiko hili naamini hakuna kiongozi wa dini atakayekwambia achana na mumeo.
Nashukuru mkuu, cjaipeleka ndio naanza kuifanyia kazi ndio maana nikaomba muongozo mkuu.
Cjawahi kufanya chochote zaidi ya kusikiliza tuu, tatizo kwangu c o mama mkwe instability ya mume ndicho kinachoniudhi..cwezikuthibitisha coz cjui alipo kwa sasa na cjui anaishi na nani.hatuna mawasiliano kabisa mkuu
Naona limbwata ulilotumia limekwisha muda wake jamaa kakutema, sasa huo mzigo wa watoto wawili utamkabidhi nani maisha yenyewe haya, hata kama ndoa ni watoto sio uniletee, jiandae kufunuliwa na wanaume wapya kila mwaka mpaka uzeeni na ukome kutumia limbwata
Hali hiyo cjakuomba unisaidie povu linakumwagika hivyo...non of your business stay out of this.
Just be serious, hujaonyesha jamaa alikukosea nini, tangu mganga wenu sheikh yahya afariki mnahaha, mtoto wa watu ulikuwa unamtandika na vibuyu na hirizi sasa kazinduka, jichunguze vizuri,makosa ni yako dada, kuishi na mume ni kudra kwa ajili ya wachache,inawezekana hukupangiwa ndoa ila ulipangiwa kuchepuka
Naona limbwata ulilotumia limekwisha muda wake jamaa kakutema, sasa huo mzigo wa watoto wawili utamkabidhi nani maisha yenyewe haya, hata kama ndoa ni watoto sio uniletee, jiandae kufunuliwa na wanaume wapya kila mwaka mpaka uzeeni na ukome kutumia limbwata
Mkuu mbona humuelewi mdau miaka miwili watoto hawapati huduma ya baba na anachotaka ni official separation kwakua mpaka hapo hakuna ndoa.sasa ata asipokuwa na talala kwa sasa unaweza kusema ana mume? Ndoa ta kanisani inavunjika sana .Anza na kanisani katika baraza la usuluhishi then wara wa refer mahakamani.
Maana moja wapo ya sababu ya kuvunja ndoa ni kuterekezwa ambayo tayari ipo.mwenza kuanzisha familia nyingine ambayo tayari ipo.Sasa kama hawana mahusiano ya kimwili tena si ndoa ishavunjika?Tatizo la waafrica ni kupenda kuisha maisha fake.
I said non of your business, naanzaje kukwambia ilikuwa nn,ili iweje,? Pole kwasababu hicho ndicho unachojua chini ya jua,that's too bad.stay out of this plz
Nimeolewa miaka minne iliyopita na Nina watoto wawili,miaka miwili iliyopita tulihitilafiana na mume wangu tukatengana baada ya pale alisusa kuhudumia watoto kwa kilakitu ninaishi na watoto wangu bila msaada wowote kutoka kwake...
Naomba wakuu mniongoze katika kupata talaka ili nianze upya nikijua Niko huru kuliko kuishi kwa mashaka hivi kwa kivuli cha Ndoa ambayo haiexist. Msaada wenu Tafadhali.
What if mumewe kapewa limbwata katika sagula sagula yake na huyu mama ni innocent? Au what if mwanaumr ndo hajapangiwa ndoa na ndo maana ana achan na kila anaye ishi nae.
Sasa mbona unakuwa mkali? Wewe ni mkurya au? Now i know kwa nini nneachana, you are so harsh nad you wanted him to be out of (this)everything, your heart, sex, family finance and many more,now he is out, the only thing which remains with you ni kidonda ambacho ni mithili ya kansa,no divorce papers can cure it