Nabi kumtumia Baka kwenye mechi kutaipunguzia gharama Yanga mwisho wa msimu

Nabi kumtumia Baka kwenye mechi kutaipunguzia gharama Yanga mwisho wa msimu

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Ile dhana ya hakuna mchezaji mkubwa kwenye timu ya Yanga inainufaisha Yanga leo na hata kesho. Kumchezesha mchezaji huyohuyo kwenye mechi zote timu inapopata matokeo mazuri na timu kupata matoke mabaya kama mchezaji huyo asipopangwa kunaingarimu timu fedha nyingi kumbakisha kikosini mchezaji kama huyo.

Nabi anafanya vizuri kuwapunzisha wachezaji hata wale wanaojiona pangapangua lazima wacheze ili timu kupata matokeo. Panga pangua hii ya Prof. Nabi kutaisaidia Yanga kupunguza gharama kwa wachezaji na mawakala wao wanaojiandaa kujikweza ili kubaki Yanga.

Mtu pekee anaestahili kujikweza pale yanga ni benchi la ufundi na wachezaji wachache saaana wasiozidi 3.
 
Ile dhana ya hakuna mchezaji mkubwa kwenye timu ya Yanga inainufaisha Yanga leo na hata kesho. Kumchezesha mchezaji huyohuyo kwenye mechi zote timu inapopata matokeo mazuri na timu kupata matoke mabaya kama mchezaji huyo asipopangwa kunaingarimu timu fedha nyingi kumbakisha kikosini mchezaji kama huyo. Nabi anafanya vizuri kuwapunzisha wachezaji hata wale wanaojiona pangapangua lazima wacheze ili timu kupata matokeo. Panga pangua hii ya Prof. Nabi kutaisaidia Yanga kupunguza gharama kwa wachezaji na mawakala wao wanaojiandaa kujikweza ili kubaki Yanga.

Mtu pekee anaestahili kujikweza pale yanga ni benchi la ufundi na wachezaji wachache saaana wasiozidi 3.
Yule dogo nasikia kaanza mambo ya mla ugali na sukari
 
Kule kwa makolo wao star wao ni chama tu hata kocha anaweza kuondoka ila sio chama.
chama haguswi, atakaemgusa patachimbika. Hii inaonyesha kuwa pale Yanga sasa hakuna mtu anaeingilia benchi la ufundi hata kidogo. Mshindo Msolla asingekubali Aziz Ki na Job wasicheze na kupisha Baka na Sure boy au Mudadhir
 
Kule kwa makolo wao star wao ni chama tu hata kocha anaweza kuondoka ila sio chama.
Una mimba ya chama shougaaa angu na inakutesaa eeeh?? Kwann ikutese hebu itoe shostieee utakufa nayo bureeee.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] poleeeeeeeeeh
 
Kuna mawakala uchwara wanadhani wachezaji wao watahitaji mabilioni ya fedha ili kuongeza mikataba, Prof Nabi ameamua kuwapunguza gharama Yao kwa kuwasheka kwenye mbao ndefu viwanjani na timu inapata matokeo viiiileviiiilee!!
 
Kazi yenu ni kuzushazusha tu sijui mnapata faida gani? Job kaongeza mkataba juzi tu lakini mnavyopenda kusikia mabaya ya Wachezaji wa ndani mnaibuka na uzushi kama huu. Job hawezi kurudia makosa ya Feisal kuanzisha mgomo usio na faida katika carrier yake.
 
Job anakuja Simba
 
Job anakuja Simba
Nabi ameonyesha kuwa hata aondoke nani yanga inakuwepo tu. Siku alipoondoka Saido kimtindo kuna tuliojutia sana kama vile Yanga imekwisha, siku alipoondoka Fei toto siku 2 kabla ya mechi na Azam watu wakasema mamamamamamama weeeee tumekwisha!!!. Hebu siku shabalala, au chama au kanoute apate mafua na kupiga chafya tu uone aina mbalimbali za miharisho.
 
Kwa style hii ya Nabi hakuna mchezaji atavimba saana wakati wa kuongeza mkataba wake kama vile anavyovimba Clotous Chama, Hinonga, au kanoute kule upande wa pili.
 
Si sahihi kutumia ubora wa Nabi uongozi kuwashusha thamani wachezaji wa ndani ( locals), mbona wachezaji wa nje wanalipwa vizuri, kwa nini mnajaribu kuwakazia wachezaji wa ndani na wao wakitaka maslahi mazuri. Dickson Job ana mchango kwenye mafanikio ya Yanga, anastahili kupata maslahi mazuri, kuomba maslahi mazuri sio kosa, mtaharibu hicho kikosi sababu ya janja janja za kijinga.
 
Hakuna mtu amesema watakaoshindwa kupandisha mabega yao juu ni locals tu, angalia sana mkuu hoja zako. Hebu niambia Aziz Ki, Morrison, Tusila, na Doumbia. Nani kati ya hao anaweza kuikazia huku Yanga wakati wa kuongeza mikataba yao walipwe mapesa mengi zaidi?
 
Tayari wanalipwa pesa nyingi, wao watataka ku renew tu mkataba huo huo, Aziz Ki anakula 23m wakati Fei Toto anapata 4m, unategemea atakuwa na furaha hapo ? Dickson Job anakula 2m huko halafu Doumbia anakula karibia 10m, unategemea Job atakubali kusaini mkataba huo huo tena ? Walipeni wachezaji mishahara kutokana na kazi zao na sio kutokana na uzawa au ugeni wao.
 
Kama mchezaji ana uhakika kuwa Kuna timu inaweza kumlipa 12m badala ya 2m anazolipwa Yanga hata Mimi namshauri asikubali kuongeza mkataba mpya na Yanga, aondoke TU baada ya mkataba wake kufika ukingoni au hiyo timu iende Yanga ikauziwe mchezaji huyo
 
Back
Top Bottom