Izy_Name
JF-Expert Member
- Apr 9, 2020
- 772
- 1,733
Nabi rasimi kathibitisha kuwa hatakuwa pamoja na kilabu ya Yanga kwenye mechi yao dhidi ya TP-Mazembe nchini Kongo katika mchezo wa marudiano wa shirikisho la Afrika.

Kumekuwa na sintofahamu na mashabiki wengi wa soka wakijiuliza juu ya kumkosa kocha mkuu wa yanga katika mchezo huo muhimu.
Baadhi ya vyanzo vya habari visivyo aminika vilieleza kuwa “Kocha mkuu Nasreddine Nabi ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Mazembe kwa sababu za Kifamilia. Mchezo huu ni muhimu sana kwetu kwa sababu malengo yetu ni kuwa vinara kwenye hatua hii ya Makundi”.
Tukiachana na habari hizo za upotoshaji Nabi amezungumza mbele ya waandishi wa habari na kufafanua nini kilicho nyuma ya pazia kitakacho mfanya asijumuike pamoja na kilabu katika mchezo huo wa marejeano nchini Kongo.
"Nilitamani sana kwenda na timu yangu Lubumbashi,unajua malengo ya klabu yalikuwa sawa na yangu kwamba tushinde ili tuiongoze kundi lakini bado naamini tunaweza kufanikisha kwa kuwa kila kitu kitakuwa chini ya Kaze ni mtu sahihi tu kama mimi," alisema Nabi na kuongeza kuwa;
"Kwangu kuifunga mara mbili Mazembe ilikuwa ni kiu yangu kubwa lakini nawaamini wenzangu wataweza tu bila mimi,mambo mengi tulishayafanya hapa,hata viongozi wangu walipambana sana ili nisafiri lakini imeshindikana.
"Tunataka sana kuongoza hili kundi kwa faida ya hatua ya robo fainali nawaamini sana wachezaji ni wangu na wasaidizi wangu naamini watashirikiana vizuri na Cedric,Mimi nitakuwa nawasiliana nao pia kwa simu siku ya mchezo.
Nabi aliongeza tayari alishaanza taratibu za kupata pasi mpya ya kusafiria kutoka Ubelgiji anakoishi lakini muda haikutosha na kwamba Sasa anarudi tena nchini humo kuhakikisha anaipata haraka na mapema zaidi kabla mikiki mikiki haijaanza.
Alisema mabosi wa Yanga wamemtaka arudi Ubelgiji haraka kuhangaikia pasi hiyo kabla ya safari ijayo ya hatua ya robo fainali kutokana tayari Yanga imeshafuzu hatua hiyo hivyo basi ni muhimu na uwepo wake utakuwa na maana kubwa katika mechi zifuatazo za robo fainali.
"Narudi Ubelgiji leo (jana), unajua kule kupata pasi mpya unahitaji muda zaidi, nilishaanza hizo taratibu niliporudi kule wiki moja iliyopita lakini muda haukutosha, klabu imetaka nirudi haraka nihakikishe naipata nyingine.
CHANZO