Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Nabii Mussa Richard Mwacha Maarufu kama Kuhani Musa, amesema kuwa Tanzania imekuwa kitovu cha amani barani Afrika, na hivyo kuwa kimbilio kwa watu kutoka mataifa jirani wanaokumbwa na machafuko. Ameeleza kuwa mara nyingi ndugu zetu kutoka nchi kama Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekuwa wakikimbilia nchini Tanzania wanapokumbwa na matatizo, ambapo wamekuwa wakipokelewa na kuhifadhiwa katika kambi maalum.
"Leo tukianza sisi wenyewe kugombana na kubaguana, tutakimbilia wapi? Hatuna sehemu nyingine ya kwenda," alisema Nabii Mwacha. "Tanzania imekuwa kimbilio kwa wengi, tusimchezee Mungu ambaye ndiye mfalme wa amani."
Katika wito wake kwa wananchi wote, bila kujali tofauti za kidini au kijamii, Nabii huyo amehimiza umuhimu wa kudumisha mshikamano na kulinda amani ya taifa. Amesisitiza kuwa Tanzania ni nchi iliyobarikiwa na Mungu kuwa chanzo cha ukombozi kwa mataifa mengine ya Afrika, na kwamba amani ya nchi hii haipaswi kuvurugwa kwa sababu yoyote ile.
"Amani tuliyo nayo ni zawadi kutoka kwa Mungu. Tuitunze, tuilinde, na tuienzi," alisisitiza Nabii Mwacha.
Mwito huu unakuja wakati ambapo dunia inakabiliwa na migogoro ya aina mbalimbali, na hivyo kuweka msisitizo mkubwa kwa Watanzania kuendelea kuishi kwa upendo, mshikamano na heshima kwa kila mmoja.