Nabii Clear Malisa ni nani?

Nabii Clear Malisa ni nani?

Jamaa anaona sana. Alishahahi kuielezea historia ya familia yetu vizuri sana na Wala hamna mtu Dar anatujua vyema kiasi Cha kumpa habari zangu hizo, na alinipa tote hayo siku ya kwanza tu nilipokanyaga kanisani kwake
Kwa nini mnadanganywa kirahisi namna hiyo?

Hayo ni mapepo ya utambuzi,

Mtu mwenye mapepo hayo anaweza kukwambia kila kitu juu yako na akalenga mule mule!
 
Miaka Kama mitatu iliyopita nilialikwa kanisani kwake ..kwangu alichemka mazima eti ananiambia "kazini kwako wiki ijayo boss wako atakupandisha cheo kikubwa" halafu akaniuliza umeajiriwa nkamwambia hapa nimejiajiri akasepa zake kwa mtu mwingine ..NAMWONA MSANII SANII SANA hata kipindi kile Cha corona imeanza akasema itaisha Mwezi ujao....inshort ni Nabii shillah type ..mpigaji tu wa mjini usiku anashinda sinza kwenye masaloon anapiga story na masela
 
Jamaa anaona sana. Alishahahi kuielezea historia ya familia yetu vizuri sana na Wala hamna mtu Dar anatujua vyema kiasi Cha kumpa habari zangu hizo, na alinipa tote hayo siku ya kwanza tu nilipokanyaga kanisani kwake
Hakuna kitu kama hicho, huwa wanakuweka mezani wanakusoma kama ramani, wanajua mipaka yako na vyote ulivyo navyo.

Mara nyingi wanatumia watu wako wa karibu, yuko tayari asafiri umbali mrefu kwenda kupata habari zako.

Hivi hao wake zenu walivyobadilika wanawezaje kushindwa kukuelezea kwa nabii.

Hao ni sawa tu na yule mama wa huko kando ya ziwa
 
Nabii Clear Malisa alibebwa na malaika hadi Zimbabwe vijijini kabisa kufanyiwa impartation, Kisha akarudishwa bongo na malaika
Hakuna kitu kama hicho, huwa wanakuweka mezani wanakusoma kama ramani, wanajua mipaka yako na vyote ulivyo navyo.

Mara nyingi wanatumia watu wako wa karibu, yuko tayari asafiri umbali mrefu kwenda kupata habari zako.

Hivi hao wake zenu walivyobadilika wanawezaje kushindwa kukuelezea kwa nabii.

Hao ni sawa tu na yule mama wa huko kando ya ziwa
 
Manabii wa uongo wamejaa kila aina wanafanya miujiza na ishara nyingi na za ajabu nao watawadanganya wengi

Mathayo7: 15 “Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali.

21 “Si kila mtu anayesema, ‘Bwana, Bwana,’ ambaye ataingia katika Ufalme wa mbinguni ila ni wale wanaofanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Siku ile itakapofika wengi wata niambia, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii na kufukuza pepo kwa jina lako; na kufanya miujiza mingi ya ajabu kwa jina lako?’ 23 Ndipo nitawaambia wazi, ‘Sikuwafahamu kamwe. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!
 
Pepo wa utambuzi ni nani?
Wanatumia pepo la utambuzi kubashiri mambo yajayo na watu wana amini .... kama siyo msomaji wa biblia nikisema pepo la utambuzi itqkuwa kitendawili .... kasome karama za roho mtakatifu ...ndipo uje hapa
 
Back
Top Bottom