Pre GE2025 Nabii Edmund Mystic: Watanzania epukeni mashinikizo yoyote yanayoweza kuhatarisha usalama wa nchi kuelekea uchaguzi mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Watanzania wametakiwa kuepuka mashinikizo yoyote yanayoweza kuhatarisha usalama wa nchi, yakiwemo maandamano, hasa wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Rai hiyo imetolewa na Nabii wa Kanisa la Heavenly Image Manifest (HIM), Nabii Edmund Mystic, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu mkesha mkubwa wa kuliombea Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan, na uchaguzi mkuu ujao.

Mkesha huo unatarajiwa kufanyika Februari 28, mwaka huu, katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, ukihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.

"Tumeona mwaka jana jinsi hali ilivyokuwa nchini Kenya baada ya machafuko kutokea. Watumishi wa Mungu walihubiri kuhusu hatari hizo, lakini wengi hawakuzingatia. Sisi kama Watanzania, tunapaswa kutambua kuwa usalama wa Taifa letu ni jukumu la kila mmoja wetu. Ni muhimu kuepuka shinikizo lolote linaloweza kuleta machafuko na sisi viongozi wa dini tunapaswa kusimama imara kuliombea Taifa," alisisitiza Nabii Edmund.
 
Unafiki utatuua,
Badala wajibu hoja za lisu wanakuja na mbamba za kizamani
 
Kila mtu ni nabii siku hizi

Wataanza kutupigisha short very soon
 
Muendelezo wa CCM na vibaraka wao kueneza Propaganda za kuwapumbaza watanzania ili waendelee kuwa wajinga.
 
Ana shida gani wakati chanzo chake cha mapato hakikatwi kodi.
 
Kuna chama kimemkabidhi kichaa madaraka, kitajutia dakika za jioooooni!, wakati mambo yashaharibika.
 
Exactly huyu nabii ni makuu
Usimtusi, utalaanika,hujamwelewa,

Anawaambia mamlaka wasikize HOJA za TUNDU Lissu na kuzijibu Kwa Amani Ili tusiende huko kwenye maandamano.

Maana ukiangalia hapo, anayehatarisha Amani, ni wale wanaokumbatia tume iliyopo inayobariki kura fake kuingia kwenye Sanduku la kura kulinajisi.
 
Mkuu me ni bingwa wa kuelewa nimekuelewa.
 
Kumeanza kukucha.tunawasubilia wengine wa hivi kujitokeza mpaka October tutaona Mengi yasiotakiwa kuonwa
 


Huwezi kumpangia Mungu. Kama kuna Haki fujo zitatoka wapi? Kama hakuna Haki huwezi kuepuka fujo, maandamano na michafuko. Wakulaumiwa ni wale wanaopindisha haki. Yaani Watanzania watakuwa wajinga kukubali kuibiwa na kulazimishiwa watawala ambao hawajachaguliwa. Hakuna Mungu wa hivyo. Kama anapenda nchi aweke haki mbele kila kitu kitakuwa powa
 
Mpumbavu mmoja,kwa hiyo kwa akili zake mambo hapo Kenya yapo kama yalivyokuwa kabla ya maandamano ya mwaka jana?

Ujinga tu aridhike na anavyowaibia wajinga asitake kuwageuza hata waiotaka ujinga wake kuwa wajinga wa siasa.
 



View: https://youtu.be/qrQOTjDJUXM?si=Sh2PCfzzlRmjPrAeKuna manabii wa kila aina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…