Dhambi hii ya watumishi kula kondoowao imeanza kipindi cha nyuma sana, Daudi alijikuta kwenye mtego wa kumtafunamke wa mpiganaji wake Uria mhiti, na baadaye dhambi hiyo ikapelekea mauwajiyake askari huyo shupavu. Pamoja na uhusiaono mzuri wa Daudi na Mungu badoshetani aliweza kupenyeza hiyo nguvu ya kukamata akili ya Daudi akiwamapumzikoni na kuitenda dhambi hiyo bila ya uoga wowote. 2samweli 11
Mungu hakufurahiswa na tendo hilo naakamua kumpa adhabu hii hapa chini kwenye sura ya 12;9 na kuendelea.
9 Kwanini umelidharau neno la Bwana, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? UmempigaUria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyokwa upanga wa wana wa Amoni.
10 Basi,sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau, ukamtwaa mkeweUria, Mhiti, kuwa mke wako.
11 Bwanaasema hivi, Angalia, nitakuondokeshea uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaawake zako mbele ya macho yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zakombele ya jua hili.
12 Maanawewe ulifanya jambo lile kwa siri; bali mimi nitalifanya jambo hili mbele yaIsraeli wote na mbele ya jua.
13 Daudiakamwambia Nathani, Nimemfanyia Bwana dhambi. Nathani akamwambia Daudi, Bwananaye ameiondoa dhambi yako; hutakufa.
14 Lakini,kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za Bwana nafasi kubwa ya kukufuru, mtotoatakayezaliwa kwako hakika yake atakufa.
15 NayeNathani akaondoka kwenda nyumbani kwake. Basi Bwana akampiga yule mtoto ambaye mkewe Uriaalimzalia Daudi naye akawa hawezi. Kiufupi mtoto huyu alikufa.
Nini nataka tujifunze kupitia mfano huu.
Kama kweli tuna mwamini MUNGU natunakili yupo, hakuna namna tutakwepa kuwa chini ya viongozi wa dini, yaani wachungaji, wainjilisti, maaskofu, mitume,manabii na nk. Kwa sababu mfumouliowekwa duniani ni wa kuongozwanakuongozana. Mungu anaweka maarifa kwa watu wachache wawafundishe wengine, ilekutengenezamfumo wa kutegemeana na kuheshimianaambazo ndizo nguzo za jamii ya aina Fulani kuisha pamoja.
Ukikataa kuwa chini yao, huwezi kupata sehemuya Mafanikio ya kimwili na kiroho ya halalikwani baadhi ya mambo kimsingi yamefungamanishwa na uwepo wao
2 Mambo ya Nyakati 20 : 20 Wakaamkaasubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwawakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji waYerusalemu; mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waamininimanabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.
Kwani tafsiri za MUNGU huja kwa wakati mwafakakupitia kwa watu wake walio na muda naye, na ndiyo maana aliamuru watumishiwatumie muda mwingi kumtafuta wakati wengine tunasaka matonge, ili nasitukapate walicho ambiwa wakiwa katka haki na utulivu wa kumtafuta MUNGU nawatuelekeze nasi tutekeleze na dunia isonge mbele.
Hii haimaanishi mtu hawezi kumtafuta MUNGU, lakini ni wangapiwana muda huo kama sio mpaka shida iingie ndo akufunge siku tatu kavu naikishaisha baada ya miezi miwili uko kama kawaida?
Kwa mantiki hiyo swala la uongozi wadini /dhehebu ni muhimu na haukwepeki, na ndio maana MUNGU hakumuondoa Daudibaada ya dhambi yake ila alimpa adhabu ambay o haiukumpata yeye tu bali hatauzao wake, wewe unayedhani utakwepa hili sio suluhu utaathirika tu ilimradiunamapenzi mema na unamtafuta MUNGU, ukitaka kukwepa mtumikie shetani asilimiamia, kwa sababu hata ukisikia habari mbaya kuhusu JEHOVA hutaumia moyo.
Wakati mwingine huwa nashangaa sana nasijui upofu huu unatoka wapi, Mkatolika anajiona ni bora kuliko Mlutheri hatakinyume chake pia, au mpentekosti ni bora kuliko mkatoliki hata kinyumechakepia, wakati wote wanamtafuta MUNGU huyohuyo na wanatumia muongozohuohuo(biblia) na wanaamini jahazi likizama kwa mwenzake yeye yuko salama, bila kujua adui wao wote niyuleyulena anafanya mashambulizi bilakujali wewe wa wapi. Bila umoja kipigo kipo palepale bila kujali dini yako
Tujikumbushe, mapadri na makadinari wanaskendo nyingi za ngono na kuzaa wakati hawatakiwi, je katolika haifedheheshi nahilo na kama we ni mkatoliki unakwepa hapo?, wakatolika wameacha kumwabdu MUNGUkwa sababu ya uovu wa viongozi wao? Wachungaji wa Kilutheri , kimoraviani na nkwana skendo hizo hizo, je wameacha kuenda makanisani, leo hii walokole nao wamo humohumo, sasa niambieatakwenda wapi ambapo pako salamaa? Au kila mtu awe na dini yake nyumbani kwake?
Mtu yeyote anayekwambia hamia mahali furani anamaarifa madogo na hajaua vita yetu sio yadamu na nyama. Maarifa hutafutwa popote matumizi ya maarifa ndio hufuata eneomaalumu, tafuta maarifa kokote komboa watu wa nyumbani, kanisani au nchinimwako. Usikubaliane na hoja nyepesi kuwa hapa ndo pa asili au hapa papya,sheteni alikuwepo kabla hujazaliwa, ishu sio upya au uasiliishue ni mkaribieni Mungu nae atawakaribia mpingeni shetani shetani nayeatawakimbia
Shetani anajua Mwenye maarifa ndio aduinamba moja hivyo watumishi wanawindwa zaidi kuliko waumini,26:31 Kisha Yesu akawaambia, "Usiku huuwa leo, ninyi nyote mtakuwa na mashaka nami, maana Maandiko Matakatifu yasema:`Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika. Huwapiga hao ili waumini watawanyike, na kwasababu ya maarifa kidogo yawaumini hutawanyika na kuwa mawindorahisi kwa adui.Lakini pia tusisahau aliyetongozwa si mke wa mtu na ni muuminianayejua la kufanya? kwanini asiilinde imani yake kwa kukataaa? wkati anajuaakifanya hivyo anatuharibia wote kama waamini MUNGU, kwa sababu matusi yakekutoka kambi ya adui ni yetu pia.
Nashauri waamini tutumie vizuri silaha tulizo nazo, ogopa kupigana kwa kumsaidia adui,watumishi wako hatarini kuliko unavyodhani wanahitaji kuombewa na kulindwa kiimanina kimaumbile, ukimkatalia wewe na kumelekeza ipasavyo umemlinda. Lakini piatukue tumeabudu miaka nenda rudi mbona hatuendi mbele? Tufike mahali Tuanze kulachakula cha watu wazima, tukawasikilize watumishi na kisha tujenge imani na tujipiganie kwa mambo menginemaana imani huja kwa kusikia na kisha kuweka kwenye matendo. Sio kilawakati kuombewaombewa tu, jililieni wenyewe kwa maarifa mliopewa, mtapunguza fursa za kwenda kwenye ofisi za watumishi ambazo wakati mwingine ndio mitego.