Nabii kiboko ya wachawi, naona anafanya maigizo

Mwambie Nabii nina million 100 amfufue kuna mzee mmoja anilipe hela yangu tu halafu yeye Nabii atajua la kumfanya huyo mfu.

Akili za masikini ndio hufikwa na hawa manabii mwenye lishe bora hawezi kuwaamini hawa wachawi wa mchana.
Daah,umetoa wazo zuri,kama vipi twende zetu Buza tukamtafute atufufulie mdaiwa Sugu,,,kwenye hiyo mia mie anipe ten percent ya udalali
 
Hayo unayoyasema na Yale ya Mwamposa Kuna tofauti Gani?
 
Daaah..... Elimu kweli ni kitu muhimu. Mwandishi hana tofauti na huyo nabii. Anaandika pumba na hakuna anachoeleweka kama anasimulia watoto wenzie huju akicheka cheka. Kwa nini hampendi kuwa na akili?
Uliadimika bro humu JF. Vipi bro wake na mke wake wanaendeleaje? Yule mtoto wa miujiza wa bro wako anaendeleaje?
 
Ni nani huyo? Kuhani Mussa ama?
 
Hawa manabii wa uongo waabudu mashetani watakokota wengi kuzimu. Maana wengi hawana muda wa kumtafuta Mungu binafsi. Imeandikwa, mjue sana Mungu ili uwe na amani ndipo mema yatakapokujia. Wengi tumekuwa na masikio ya utafiti, wengi husikiliza mafundisho ya mashetani na maagizo ya kibinadamu. Wengi wamedakwa kwenye hizo cult bila hata kujijua. Wengi wanapotea kwa kutojua maandiko wala uwezo wa Mungu, wengi wanaangamizwa kwa kukosa maarifa. Mungu atusaidie sana.
 
Joannah wewe si umeokoka lakini
 
Si kwq ubaya ila hilo swala la manabii ndio jambo pekee linatofautisha Uislam na imani nyingine katika swala zima la kuabudu.

Kwanza katika uislam hutokuja kusikia kuna nabii yeyote, ilishapigwa full stop kuwa Nabii wa mwisho alikuwa ni Muhammad S.A.W.

Katika uislam kuna universal praying module. Haijalishi unaangukia wapi duniani, hutoshindwa kufanya ibada hata kama hujui lugha ya eneo husika.
Sasa kwingine utasikia kuna madhehebu ndani ya madhehebu, kuna kanisa ndani ya kanisa.

Kila 'nabii' anaekuja anaanzisha kanisa lake na hilo linaendeshwa kwa misingi yake yeye, sio ya Mungu kupelekea waumini wa hilo kanisa hawaendi kumuambudu Mungu bali kufuata ibada ya nabii.

Uislam uliondoa system ya udalali baina ya mwanadamu na Mungu wake. Huwezi kusikia muislam anaenda kuomba sheikh afikishe maombi yake kwa Mungu. Kama ni kuombewa dua basi wote wawili sheikh na anaeombewa wote wanamuomba Mungu bila yeyote baina yao kujitwika uwakilishi ama uwakala wa Mungu.

Kubwa na la umuhimu zaidi ni uislam kutoruhusu kitabu chao kubadilishwa/kuboreshwa kwa njia yeyote ile. Q'uran toka ilipoanza kutumika mpaka leo hii hakuna maboresho hata ya herufi yaliyofanywa mpaka leo.

Binadamu tumeumbwa na ubinafsi wa kupenda sheria na kanuni ziwe na manufaa kwa yule mtunzi.
Kuruhusu kitabu kimoja kifanyiwe marekebisho kumefanya kuwepo na mabadiliko mengi ambayo hayakuwepo kwenye original version, yote kwa maslahi ya waboreshaji.

Kuna wakati mafundisho ya biblia na Q'uran yalifanana kwa karibia kila kitu, lakini mpaka leo hii kuna version za biblila lukuki.

Sio dhamira yangu kukandamiza dini yeyote ila ifikie wakati binadamu tujifunze kuongea na Mungu wetu directly. Hakuna anaejua madhila/shida zako zaidi yako wewe mwenyewe hivyo ni busara zaidi kuongea na Mungu directly pasi kutumia binadamu mwenzio ambae mwenyewe ana mapungufu yake ya kutosha pengine kuliko hata ya kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…